Ninawaza kugombea jimbo HAI 2015

kimboka one

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2010
Posts
734
Reaction score
85
Wadau sijasubiri niseme wazee wameniomba,ila ni nafsi yangu sasa imejiridhisha kuwa wakati umefika nami sasa nirudishe nguvu walizotumia watu wa nshara,uduru,lyamungo,masama,narumu,mronga,lambo,kisereni,mkweseko,uswoa,mkwarungo nk. kwa kunielimisha vya kutosha.ni zamu yangu sasa kuwaongoza kuijenga nchi yetu na kudai haki zetu kwa pamoja.

si kwamba Mhe Freeman ameshindwa kazi la hasha.ni kumpa nafasi aweze kufanya kazi zake ndani ya chama katika ngazi ya taifa.

wakati ukifika nitawakumbusha hapa jamvini,kwa kuja na utambulisho rasmi na sababu za mimi kuamua hilo.

najua mtapenda kujua ni chama gani? ni nani? ila muda ukifika yote mtajua.
 

Mkuu wangu badala ya kupiga porojo hapa JF ungeenda huko HAI kusaidiana na wananchi ktk kazi za maendeleo
 
Wewe mwenyewe hujiamini nani atakupa huo uongozi maana kama unajiamini ungeingia na ID Name sahihi lako la kiserikali wewe unaingia na ID za KiJF, embu tuondokee hapa usituletee ukomedi wako hapa
 
kwanza kabisa ni kutumia aridhi yetu ndogo vizuri,hasa milima na kwa hakika mlima kilimanjaro kwa aridhi yetu ni ndogo sana,tazama tuna.
1. Hekta 46,506 (46%) zinafaa kwa kilimo

2 Hekta 14,154 (14%) ni eneo la misitu

3. Hekta 13,143 (13%) ni eneo la miamba na

4.Hekta 27,297 (27%) ni eneo lifaalo kwa malisho ya mifugo.

utagundua hatuna aridhi ukilinganisha na mikoa mingine.
 

unaleta data unajifanya magufuli enhe?haya mito inayotiririka Hai ina lita ngapi za ujazo?ng'ombe jimboni hai ni wangapi?madume mangapi?majike mangapi?wenye mimba wangapi?na wanakula majani kilo ngapi?mbu wanaosababisha malaria ni wangapi jimboni Hai?jibu hayo kwanza kwa uchache
 
Sahau kupitia gamba upite hapa Hai,kamuulize fuya what happened. Leta sera zako hapa jamvin tuzichambue.
 
Very simple ila masharti yafuatayo uyatimize
1) uwe unatokea kaskazini mwa tz
2) uwe na undugu wa karibu na mtei
3) uwe na mtaji na magari kama mafuso au maloli yenye uwezo wa kukodishia cdm kipindi cha uchaguzi
4) uwe m..st.. safi
5) uwe mvumilivu hadi pale mbunge wa sasa atakapochoka au ku...ki (inshort ile safari ya kila mtu)

Nakutakia kila la kheri
 
Unakaribishwa sana kugombea Hai maana hata NAPE nae bado ana wazo hilo hilo pale Ubungo.
 

kumbe hai ni mkoa?
 
Elimu ya kutosha kwako ni ipi?
 


mkuu wa mkoa wa Hai anaitwa nani?
 
kwani kuwasaidia wananchi wa hai mpaka uwe mbunge? braza kumsupport Mbowe katika harakati zake Hai ni kuwaletea wananchi wa hai maendeleo!
 
keleuwiiiii
 

Fuya Kimbita alikuwa mbunge wa Hai. je alikuwa na undugu na Mtei?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…