Habari za leo ndugu zangu,
Katika maisha tunapitia mengi sana lakini yapo mengine ni magumu mno kuyafanyia maamuzi.
Katika pitapita zangu na kuzunguka mikoa mbalimbali bahati mbaya nilijikuta nawazimikia wanawake wanne katika vipindi tofauti.
Mbaya zaidi wote wananipenda pia na wote wanasifa zile nazozihitaji.
Sasa muda wangu wa kuoa umefika. Nahitaji kuoa. Lakini cha ajabu kufanya maamuzi imekua ni ngumu sana. Na nzuri zaidi wote hawajuani
Jamani nipeni mbinu nifanyaje ili nichukue maamuzi chanya.Namimi huwa siachi mwanamke kabisa, nina huruma ile mbaya.