Ninavyowakumbuka marehemu Dr. Judith Kahama na Dr Meshark Massi

Ninavyowakumbuka marehemu Dr. Judith Kahama na Dr Meshark Massi

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
2,205
Reaction score
2,707
Ninavyowakumbuka marehemu Dr. Judith Kahama na Dr Mehark Massi.

Madaktari hawa wote ni marehemu DR. Judith Kahama alifariki terehe 6 Julay wakati Dr.Meshark Massi amefariki jana usiku katika hospital ya mhimbili.

Ninawalilia sana maana ninawafahamu kwa karibu sana,

Dr. Judith Kahama:
Binti wa waziri wa mwanzo wakati wa uhuru Sir. George Kahama, alikuwa jeshini Makutupora mwaka 1980-1981 operation Tija chini Mkuu wa kikosi Lt.col Edimund Mjengwa na optio Major. Lyanga. Inasemekana marehemu aliondoka na mkuu wa kikosi Lt.col Mjengwa kwenda Kigoma kwenye sikukuu ya wakulima kitaifa iliyofanyika huko na waliondoka kwa ndege inaelekea Marehemu alikuwa na uhusiano mzuri na mkuu wa kikosi huyo, mkuu wake wa mafunzo Major LYANGA alimind kitu hicho, unajua alichokifanya aliitisha rollcall ya kikosi kizima mishale ya saa 2 usiku rollcall yenyewe ilikuwa ya kichwa hadi kichwa na ikabainika kuruta Judith Hakuwepo kwa maana ingine ilikamatwa redhanded hayupo, basi kesho yake kweye daily order ikasomeka Judith ni mtoro na hatamaliza jeshi ataendelea kwa wiki mbili zaidi, Col Mjengwa aliporudi nae kwenye daily order akaiquash hiyo adhabu nakumbuka aliandika hivi nanukuu "Kulingana na judhuu mimi mkuu wa kikosi nina uwezo ninaifuta adhabu ya kuruta wote walioamriwa wasimalize jeshi na kwamba wamalize pamoja na wenzao".

Wakati tif ya mkuu wa kikosi na optio wake ikifanyika jeshini Makutupora Dodoma nako kulikuwa na tif jingine kati ya baba wa marehemu Judith Sr. George Kahama na mbunge wa Dodoma mjini Padri Severino Supa nao pale Dodoma palikuwa hapatoshi ikumbukwe Sir George Kahama alikuwa ndiye Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usitawishaji makao makuu (CDA) wakati huo akina Aden Rage Mbunge wa Tabora na wenzie ndio wakati wao wa wizi uliokubuhu pale CDA mambo yakawa hayaendi basi mbunge ikabidi achukue hatua ya kuwalipua kwa kuandika kitabu kilichoitwa-Madhambi ya CDA.

Mungu aiweke roho sehemu mahali pema peponi.

Dr. Meshark Massi:
Huyu ninavyomkumbuka ni ile scandal iliyomkuta pale hospitali ya mkoa Dodoma wakati yeye akiwa ndio mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma miaka ya 90, miaka hiyo ajira zilisitishwa kada za chini zote idara ya afya, basi alitokea dada Fulani tapeli aliwadanganya kuanzia afisa tawala mkoa Mama Senyagwa hadi Dr Massi eti yeye huyo dada ni Daktari bingwa wa upasuaji yaani Surgion, kumbe alikuwa changu doa tu na bwana wake ni muuza chips, basi dada huyo wakamwajili kama dakitari bingwa akawa mpaka amnaingia theatre, siri ilivyobumburuka ilimpa shida sana Dr. Massi kutoa maelezo ikabidi ahamie Mkoa wa morogoro kwa wadhifa huo huo.

Col Mjengwa:
Yuko Tegeta anapigania afya yake

Mojor Lyanga:
Ni marehemu ajira yake jeshini ilikoma kimaajabu maajabu tu

Dr, Judith Kahama:
Ni marehemu kabla alikuwa DMO Ilala kabla ya kuwa mganga mkuu wa mkoa DSM

Dr. MASSI:
Alifariki jana hospitali ya Muhimbili

Yule dada Tapeli sijui alikoenda

Padri Supa:
Aliasi upadri yuko mtaani anaishi nyuma ya Tembe Chinangali Dodoma

Aden Rage:
Eti mbunge wa wanyemwezi wa mjini Tabora eti wanyawezi wakaona mbunge ni Rage.

Mama Senyagwa:
Amestaafu yuko Mkoani morogoro ila nasikia senyagwa amemtelekeza yuko kijiji cha Mseta walaya ya Kongwa aliwahi kuwa mbunge wa pale ila juzijuzi amehama CCM na kuhamia CHADEMA pale kibaigwa.

Ebaeban
Tel.Aviv.
 
Aisee una kumbukumbu sana mkubwa maana story za over 20 years unazinyaka kwa sana!! Asante, nime connect the dot vizuri!!!!!! Pole sana Pro. Maro . Mungu akujalie afya iwe njema na hongera kwa kuishi na mkeo kwa miaka yote hiyo!!! Ndoa ni kuvumiliana!!!
 
Safi sana kutujuza hata kwa uchache juu historia na tulikotoka!
 
Aisee una kumbukumbu sana mkubwa maana story za over 20 years unazinyaka kwa sana!! Asante, nime connect the dot vizuri!!!!!! Pole sana Pro. Maro . Mungu akujalie afya iwe njema na hongera kwa kuishi na mkeo kwa miaka yote hiyo!!! Ndoa ni kuvumiliana!!!
mkuu no name calling! lazima ule ban
 
Pumzikeni kwa amani wote mliotangulia mbele za haki,
poleni sana wafiwa wote.

........Ni alivyomfahamu yeye
akataka na wengine tumfahamu kidogo
pole doctor Riwa pengine itakuwa imekugusa.

Sijakuelewa 'hadithi' yako inalenga kutueleza nini kuhusu dada yetu Dr Judith.
 
Kwenye hii topic, nimekumbuka hiyo skendo ya "Dakitari" tapeli Dodoma wakati huo tunaipata kupitia RTD
 
Mkuu chinangali hakuna nyumba ya Tembe, labda unaongelea zamani sana au chang'ombe.
 
Sijapenda.... Inaonekana kama si elimu, basi ungekua mchawi
 
pole doctor Riwa pengine itakuwa imekugusa.

Nimeuliza tu anieleweshe..maana kila mtu anelewa lake hapa, na wengine mpaka wanampa pole mwalimu wangu Dr Maro. Ndo maana namtaka muanzisha uzi ebaeban atuambie anajaribu kutoa ujumbe gani!?
 
Last edited by a moderator:
Sijakuelewa 'hadithi' yako inalenga kutueleza nini kuhusu dada yetu Dr Judith.

Ni hivi mkuu, kwa watu walioenda JKT enzi hizo watanisaidia, rollcall zilikuwa zinafanyika ngazi ya kombania tu tena mchana kweupe. Vile vile kuna aina ya milio ya burglar mfano kushusha bendera ina mlio wake,na pia kuna mlio wa hatari, sasa kikosi kuitwa usiku master parade kwa mlio wa hatari ilitusitua sana wapiganaji tukajiuliza kimetokea nini cha hatari ? Hatari zenyewe ni kama bunduki imepotea au mpiganaji ameuwawa uraiani n.k.

Sasa kuhudhuria master parade isiyoyo kawaida usiku na kwenda kugundua ni kwamba Kuruta Judith Kahama ndie aliyekuwa anatafutwa kila mtu aliyehudhuria alifyonya mdomo , Judith kuwa hayupo ndio apigiwe burglar la mlio wa hatari ? Sasa juzi kusikia Dr Judith amefariki ndo nika recall siku ile, ili wanzengu wanablog waliokuwepo siku zile tumukumbuke marehemu kwa hilo.
 
RIP soul of DrJudith and Meshark
Know Dr Mmassk for quite so time mzee wa soda...!!
 
PIP Dr Meshak Massi, alikuwa mganga mkuu wa Mkoa wa Mwanza hadi alipostaafu, Tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi, Bwana alito Bwana ametwaa jina lake liabidiwe.
He was such agood friend to all of us at Mwanza Regional Secretariat
 
Naona amesema hapo juu,
mwelewe tu doctor
ujue hadi kufikia kusema hivyo ebaeban ana lililomgusa miaka hiyo,
ila tuache wapumzike kwa amani kwanza.

Nimeuliza tu anieleweshe..maana kila mtu anelewa lake hapa, na wengine mpaka wanampa pole mwalimu wangu Dr Maro. Ndo maana namtaka muanzisha uzi ebaeban atuambie anajaribu kutoa ujumbe gani!?
 
Last edited by a moderator:
Dr Judith alikuwa kama changu flani hivi kabla hajaolewa, anyway RIP.

RIP Dr Massi!!

Ebaeban, Mjengwa anaumwa nini??
 
Dr Judith alikuwa kama changu flani hivi kabla hajaolewa, anyway RIP.

RIP Dr Massi!!

Ebaeban, Mjengwa anaumwa nini??

Unataka kutuambia ndiye chanzo cha tatizo na si Prof. au?
 
Sijapenda.... Inaonekana kama si elimu, basi ungekua mchawi

Mchawi vipi mkuu?Mambo yaliyonyuma ya pazia mengine huwa yanatisha na huwezi amini mpaka uone mwenyewe, katika uzi huu hamna hata nililoongeza chumvi, ni kweli yametokea mfano Padri Severino Supa,ana Ph.D tangu mwaka 1962, na alikuwa mbunge Dodoma mjini kwa takriban miaka 15, sasa mtu mwenye Ph.D tangu 1962 unamkuta kavaa nguo kiunoni halafu anakaa nyumba ya tembe na anafukuza kuku utaacha kushangaa? Kutokana na ugomvi wake mbunge huyu na Sir. George Kahama ndo uliacha tumjue haraka Melehemu Judith pale JKT Makutupora.

Kama mimi ningekuwa mchawi kama siyo elimu basi wewe ungekuwa mgawa ngekewa kwa wachimba madini kama siyo elimu.
 
Kama unamshangaa Padri Supa ebaeban basi utamshangaa zaidi Rais wa Sierra Leone Mh. Valentine Strasser alikuwa rais na ni mwana sheria amesomea majuu lakini mambo yakampindia mwisho wa siku sasa anaishi Grafton Mashariki ya Freetown anaishi na mama yake anakunywa pombe za mapipa nazo anadowea tu harafu ni graduate wa law, saa ingine ni omba omba mitaani kama malehemu Matonya, kwa hiyo tusishangaane.
 
Dr Massi aliingia theatre kumzalisha dada yake baada ya madaktari kushindwa! Alifanikiwa kuokoa maisha ya dada yake na mtoto!
 
Back
Top Bottom