Ninavyoimudu ndoa ya Wake Wawili

Mimi pia huwa siwaelewi kabisa kwa hili. Wanaipinga polygamy kuliko hata kuchepuka nje
 
Siamini katika mgawano wa mapenzi..ila ni vyema kujichagulia kinachokupa furaha na amani kuliko kua mnafiki

Ukiongeza watatu ulete mrejesho mkuu

Kila la kheri
 
hebu
hebu chunguza vizur kati ya hao wenye mke mmoja na wenye wake wengi ni wepi wachepukaji konki. acheni kuhusisha mambo ya Mungu na tamaa zanu wenyewe, huyu mwenyewe sio mkristo hakuna mkristo wa design hio.
 
Huu uzi ukiutafakari unaona uko na ajenda pana ndani yake (upotoshaji) nikusahihishe
- kanisani hukushikwa shati kwenda kutoa sadaka ungekua unakaa tu na hakuna mtu anaekulazimisha na pia kwa taarifa yako kanisa halikua linategemea sadaka yako
- kanisani huzuiwi kuoa wanawake wengi ila unafundishwa maandiko ni maamuzi yako kuyafuata ama kuyaacha
-hizo ni tamaa zako tu, nina mke mmoja miaka 3 sasa na sijawahi kuchepuka na wala sitawahi kuchepuka
- mtu hujalibiwa kwa tamaa zake
-hulazimishwi kuwa mkristo ni maamuzi yako unaweza hata kuwa muislam na hakuna atakae kufuata.
-huu uzi upo kwa lengo la kuipotosha imani ya kikristo maana ninaamini ni wewe mbwa mwitu aliejivika ngozi ya kondoo
 
Mkuu sikushauri uwaweke sehemu moja, wanawake hawajawahi kupendana kamwe, usione wanachekeana, watakuja kufanyiana mambo hutoamini macho yako... Nna ushuhuda wa hili nalokwambia... Miaka fulani zamani kidogo rafiki yangu alifanya hicho unachokisema na aliamini hivyo unavyoamini, siku moja Bi mdogo akiwa mjamzito, wakiwa wanaongea kwa Furaha tu na Bi Mkubwa, Bi Mkubwa akachemsha maji kisha ghafla akamwagia Bi mdogo, yeye na mimba yake alifariki baada ya siku 2.
 
Ona msadukayo huyu umeandika ugolo tu, wewe utaweza kushea rungu wewe?
 
If you don't know something you better ask na sio kuongea blah blah blah za kilevi levi
 
Duuuh ngoja ngalatia niongezee mmoja mana hakuna namna kuacha kuchepuka kugumu
 
Yaani wake wawili tu tena miaka mitatu tu unakuja kutamba mbele za wanaume, hata watoto bado kupatikana tayari unajigamba eti umewamudu.... bure kabisa.
 
umeongea point kubwa sana.hakuna mahali katika dini zote mungu amekataza usioe wake wawili au zaidi

Sio lazima Mungu aseme kila kitu ndio iwe katazo au ruhusa. Vitu vingine wewe mwanadamu unajiongeza na ndio maana umeumbwa special sana( KWA SURA NA MFANO WA MUNGU) na umepewa utashi.

Kama Mungu alimuumba Adam akampa Eva awe mke wake unashindwa vipi kujiongeza hapo na kuona kwamba mke ni mmoja tu? Haihitaji Mungu aseme hapo

Tamaa na uzinzi ndio vinatufanya tuhangaike, mara wake wawili mara wake wanne mara michepuko. Kwani huyo mke wa 2 anakupa kitu gani special ambacho mke wa 1 hakupi?

TAFAKARI
 
My freendiii acha kabisa huo mchezo...waislam wenyewe ishu za wake zaidi ya mmoja na wao wanapuguza siku hizi naona... usije amini hata siku moja kwamba mwanmake ana furaha kushare mb** na mwanamke mwengine.. we tarajia kitu kimoja tu...utakufa wewe au mmoja wao..bro watalogana tu ilhali hao sio dini yao kupokea hayo..na shida watapata watoto. Na pia hivi unadhani siku 4 au 3 za kuwa na mwanamke utamridhisha mkuu? We jua unasaidiwa tu... jikinge na magonjwa... halafu maisha yenyewe magumu unakidhi vipi mahitaji ya wanawake wawili? Kweli tamaa yako ya mwili imekufanya na uache kabisa hadi kuabudu? Kijana kifo chako Mungu atakifanya cha mfano. Rudi tubu kwa mwokozi wako...unalalamika kutoa sadaka 9 kwa Mungu wakati hulalamiki kujenga nyumba mbili kwa wanawake wawili? Leo matakwa ya binadamu mwenzako yako juu zaidi ya muumba wako anaekupa uhai? Doh ...nimetetemeka mzee....tutaja hadithia stori zako bwana Mungu atapofanya yake bro
 
Babu yangu Mzee Mbuna alikuwa ameoa wake watu kimila hali hii ikapelekea babu yangu Mdogo Francis akose kusomea upadri kwa sababu alikuwa analelewa na huyu babu yangu mimi hivyo kanisa lilimtenga babu mubwa na kupelekea huyu mdogo kokosa sifa ya kusomea upadri pale Kasita kwa wale wanaopajua Kohelanga ,Morogoro.

Katika wake zake watu kila mmoja alizaa mtoto mmoja kati yale watoto watatu wawili walisilimu wakawa waislamu ila mmoja mpaka leo yupo kwenye dini yake ya asili. Kati ya waliosilimu mmoja wapo ni baba yangu mzazi , babu yangu mdogo baada ya kusimamishwa ile shule ya upadri na yeye aliamua kusilimu hadi anafariki alikuwa muislamu na alikuwa ameoa wake wawili.

Mila zetu zilikuwa nzuri sana tulikuwa hatuna limitation kwenye issue za kuoa bahati mbaya hawa waliojipa utakatifu na kuita mila(dini zetu za asili) zetu ni ushenzi wametufikisha hapa tulipo leo.

Tunachukiana na kubaguana kisa dini iliyoletwa na eidha mzungu au mwarabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…