Ninapingana na Kauli ya "Tutaendelea Kupiga Kelele"

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Nimekuwa nikisikiliza nukuu mbali mbali za wanasiasa na wanaharakati wenye kiu ya kutaka mabadiliko ya kisiasa, utawala na uchumi. Wengi wanapenda kutumia maneno "tutaendelea kupiga kelele mpaka kieleweke" au "tutaendelea kupiga kelele mpaka mmilika wa kagoda ajulikane".

Na hii siyo siri. Hata Dokta wangu, president wangu, Dr. Wilbroad Peter Slaa huwa mara kwa mara anatamka maneno haya.

Mimi siyapendi kwa sababu kuna msemo wa wahenga "kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji". Itafika mahali hata mtu anazungumza jambo la maana kuhusu serikali na watawala akapuuzwa kwa sababu watasema "anapiga kelele tu...hana lolote"

Wataalamu wa lugha naomba mtupe namna nzuri ya ku-phrase maneno hayo ili wanaharakati wetu wapate maneno sahihi yenye vionjo vya kuwafanya mafisadi washituke pale yanapotamkwa.

Diyelelwa?.
 
tutaendeleza harakati hadi serikali ya kidhalimu imesalimu imeng'oka!
 
Hata kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala.

Tunaweza kusema......Tutapinga jambo hili mpaka tupate suluhisho au matokeo yake.
 
Back
Top Bottom