Ninampinga Bashe kuhusu TTCL kama ifuatavyo

Ninampinga Bashe kuhusu TTCL kama ifuatavyo

Hapa ndipo mlipopumbazika employee karibu wote wa public sector. Unasema nimekuja na unrealistic idea ya outsource. Upumbavu wako hapa ni kutokana na watu wa serikalini kudhani mnayofanya ndiyo realistic idea na tunayosema is unrealistic.

Nilichowaumbua na ninachodhani ni kwamba huko serikalinimmejazana manyumbu tu vilaza fulani. Ningekuheshimu kama ungesema ni unrealistic practise kuliko kusema ni unrealistic idea kwa sababu ninachoseam was a practiced case na si idea tena.

usingekuwa mpumbavu wa kutoafiti basi ungegundua kwamba nilihokieleza ndicho kinachotokea katika private sector na nyinyi mnaojifanya thinktnk ya public sector hili liliwapita.

Kifupi ni kwamba sikuleta, sijaleta na sintafikiria kuleta idea yoyote. Nilichosema ndicho kiko katika practose ya private sector and it diong just fine wakati nyinyi public sector naumbuka kuonekana ni watu wa "yes man" na kwa hakika ni kwamba mmepitwa na wakati.
Nenda VODACOM, AIRTEL, TIGO uone karibu asilimia 80 imekuwa "outsourced" tena zaidi ya miaka kumi iliyopita ndipo mgundue kwamba "private sector ilishazinduka miaka 11 iliyopita kuhusu outsource wakati mnaojifanya wataalamu wa serikali mlishapitwa na wakati huenda mlikuwa mnazingatia posho na imprest na sasa mnaaibika.

Kama hujui "outsource ni nini, basi uliza VODACOM, AIRTEL, TIGO ni nini kisha uliza NSN, EROLINK, HUAWEI ni nini na ndipo tuje tuongee pamoja.

Ndugu zangu mlioko serikalini poleni sana. Nina hakika walioko private sector wanajua ninachoongea.

Ningekuwa na uwezo au ningeweka sheria kwamba hutakiwi kufanya kazi serikalini hadi uwe umepitia private sector kwa miaka 20 kuliko kuleta ndo zisizotekelezeka kama zako na washabiki wako.

Poleni sana wafanyakazi wote wa serikali kama wote wana mawazo kama yako


Hivi unaanzaje kumjibu mtu kama huyu maana humo naona matusi, kebehi na kejeli tu.
alafu mtu mwenyewe empty kabisa hakuna anachokijua na kukiamini.
Pole sana kijana!
 
Mkuu nilifikiri utakuja na majibu ya kunifanya nielewe vizuri naona unakuja na hasira bila issues. Siko serikalini na hiyo model ya voda nk siyo outsourcing! Nenda HR department watakuelezea nini kinafanyika. Nilichokoza mada ili ufunguke zaidi na kutoa maelezo yenye evidence ya kisomi kuwa hii model unayosema iko supported na maandishi katika governance au HR structure na siyo hisia. Badala ya kujenga hoja yako naona imekuwa argument ya jambo usilolijua. Sijaona hoja zaidi ya kuwa na matusi na kuwa defensive. Mwanzo nilifikiri ninaweza kujadiliana na wewe na kujenga hoja za kitetezi ili tufaidike.hata hivyo nimegundua ni mtu wa aina gani ninayebadilishana nae uzoeefu. Kwa kifupi ume conclude hii siyo mada ya level yako. It is beyond your knowledge na mimi sitaki nibishane na wewe Kwa kitu usichokijuwa. Nimekuelewa. By the way when not realistic can not be practised.


NI dalili za Ujinga na kutokuelimika!
majigambo, matusi, kebehi za nini kama unajua unachokisimamia na kukiongea ?
 
MImi ndiye niliteleta thread hivyo jibu contents za thread. Ila ninafurahi somo lilivyowakuna na mnavyojikanyaga kupindisha mada na kuchomeka maneno ya matusi wakati sikuweka tusi hata moja.

Philosopy ya matusi na kejeli ni baada ya kushindwa kutoa hoja halisi. Jibu hoja yangu ili ujibiwe yako kama ipo vilevie lakini kama ni kejeli hutajibiwa.

Alafu analaumu wenzie kwa matusi, wakati yeye ndiye kinara.
 
Msiojua neno "oustourcing" bahati yenu ni kwamba tunaandika humu kwa ID za bandia lakini fahamu kwamba ni aibu isiyoelezeka kama ungekuwa umeandika jina lako halisi halafu wote mtandaoni tunakuona katika Tanzania ya leo hujui maana ya "outsourcing".

Ndiya maana mwenzako nimempa pole kutokana na ulimwengu anaoishi hadi asijue "outsource level" tuliyofikia Tanzania.

Na wengi wenu mnaodiriki kusema hamjui "outsourcing" nahisi ni wafanyakazi mlioko serikalini maana hata cooments zenu zimekaa kiserikaliserikali na kama ni hivyo poleni sana.

Kwa sababu mada ni TTCL kama hujui "outsourcing" tafuta mfanyakazi yeyote wa kampuni za simu unazozijua hata kama ni wa ngazi ya chini kabisa, atakufundisha nini maana ya "outsourcing".
Acha mbwembwe za kijinga, eti mtu asipojua outsourcing ni aibu! Unaonekana ulipoteza muda kuhesabu madarasa, vidato na graduation ceremonies lakini hukuelimika. Mimi siijui hiyo 'outsourcing' yako na wala si aibu kwangu. Nimeishi Europe kama mwanafunzi kwenye hao wazungu ambao wameendelea ktk nyanja zote hawana huo upumbavu wa kumuona mtu asiyejua kijisehemu cha field fulani kuwa ni aibu.
 
Acha mbwembwe za kijinga, eti mtu asipojua outsourcing ni aibu! Unaonekana ulipoteza muda kuhesabu madarasa, vidato na graduation ceremonies lakini hukuelimika. Mimi siijui hiyo 'outsourcing' yako na wala si aibu kwangu. Nimeishi Europe kama mwanafunzi kwenye hao wazungu ambao wameendelea ktk nyanja zote hawana huo upumbavu wa kumuona mtu asiyejua kijisehemu cha field fulani kuwa ni aibu.

Kutojua "outsource" katika ulimwengu wa sasa kwenye management ni aibu.
 
Kutojua "outsource" katika ulimwengu wa sasa kwenye management ni aibu.
images
 
NI dalili za Ujinga na kutokuelimika!
majigambo, matusi, kebehi za nini kama unajua unachokisimamia na kukiongea ?

Poleni sana wenye mawazo kama yenu. Hivi mnafahamu kwamba mnaongelea mtu ambaye ni kama maiti kwani TTCL tayari ni kama maiti na hizo management models zenu sijui mnampelekea nani na zilishindwa nini.

TTCL ninayoiongelea na Bashe anayoingelea si sawa na TANESCO ambayo haina competitor. Unapoleta hoja kuhusu TTCL unatakiwa kukumbuka kwamba TTCL imezungukwa na washindani katika kila sekta na washindani hao hawatishiki na kuwepo kwa TTCL.

Lakini ukumbuke kwamba ujinga na uzembe wa TTCL na washabiki wake ndiyo ulioifikisha hapo ilipo. TTCL imepewa leseni ya kuendesha Mobile company mnamo June 30, 1999.

Hii mana yake ni nini? Maana yake wasingekuwa wapiga porojo ingekuwa ndiyo kampuni kubwa ya mawasiliano yote nchini, hizi AIRTEL na VODACOM na leo HALOTEL zingepata taabu sana kuwepo.

Miaka hiyohiyo ndani ya TTCL walitoa wazo wawe na data network. Kama kawaida yao wakapiga porojo zilezile private sector wachangamkia data na wakati TTCL inakurupuka toka usingizini kuanzisha SIMUNET tayari market iko exhausted.

Kumbuka mwaka juzi tumejadili kufilisika kwa TTCL.

Hivyo, tunajadili kampuni iliyofilisika katikati ya kampuni zilizofaulu zikaizidi. Kampuni iliyofilisika haiwezi kuwa model kw alolote labda kama unataka kufanya research kwa nini kampuni huwa zinaanguka tena hasa za serikali. Ni kutokana pia kuwa na ubishi wa namna hii.

Kama ni ujinga basi ni nani alikuw mjinga kwanza kwa kuachia nafasi zikaja kampuni tele za mawasiliano zikakupiteni na sasa mnachechemea badala ya kuwa giant telecommunication provider.

Huwezi kuanza kufikiria models za "treasury registrar" au "minister", wakati wenzako huku hata Managing Director ameona kuendesha likampuni likubwa ni taabu na wote wameingia kwenye "outsource model".

Hivyo, tunpotoa mawazo kama haya, tunaangalia uzoefu kwamba mkienenda na huo mwenendo TTCL isitarajie kuchomoka kwenye bonde la tope ililozama kwa miaka tele.
 
  • Thanks
Reactions: NOD
Kaka REDEEMER,

Afadhali umeiona. Unajua Bashe anawazidi wengi bungeni na humu JF kwa kigezokwamba ameshiriki mfumo wa biashara kabla hajaenda bungeni. Kumbuka amekuwa Director wa Media moja kwa muda mrefu na akiongea inabidi uwe umeenda shule kwelikweli kupangua hoja yake.

Ona hata wanaochangia wanaishia tu kusifia bila kwenda ndani.

Wewe umeona hiyo point na mimi naongezea kwambaBashe haja-study vitu vingine katika business system. Hukohuko kwenye private sekta bado kuna ugomvi mkubwa kwamba nani awe mwajiri hasa kama institution ina discipline nyingi.

Tatizo la appointment liko kote na linatokana na utata kwamba ni nani anapaswa kutoa appointments. Kampuni nyingi zilipoingia hapo nchini zilikuwa zinaweka director wa kila department anakuwa executive director na anakuwa na decision kwenye board. Baadaye Chief Executive (CEO) wakaona hiyo inawapunguzia nguvu maana Managing Director (MD) anajidhani ni mkuu wa kampuni lakini akiingia kwenye board na executive directors wenzake anaweza kuzidiwa hoja na finance director au operations director.

Wapo wanaoamini kwamba kwa sababu fedha ndiyo inayoendesha kampuni au taasisi basi mkuu wa fedha ndiye anayepaswa kuajiri. Hii ndiyo concept ya Bashe. Wapo wanaoamini kwamba Operations Director ndiye anatakiwa kuajiri watu wake na hasa kama kampuni kama TTCL ina section ya professional duties.

Mzozo huu umekuw ani mkubwa kiasi kwamba ma-director wamekuwa wakitunishiana misuli kwenye board na ilipofikia hatua hii wakaona mbinu ni kuvuja kampuni kidogokidogo kuifanya iwe na “outsource”.

Yaani department inavunjwa na kuwa kampuni binafsi na huko inakuw ana director wake. Department ya Sales nayo inageuzwa kwa kampuni binafsi inakuw ana director wake. Department ya Marketing inafanyw ahivyohivyo na inakuwa kampuni na director wake.

Hivyo, kwa nje unaona kwamba ni kampuni moja lakini kumbe ukweli ni kwamba ndani yake kuna “outsurce” nyingi tu. Hii ni “outsource” usichanganye na “subsidiary”. Maana “subsidiary” ni kampuni ndogo bado inamilikiwa na kampuni mama.

“Outsource” ni kampuni nyingine kabisa. Natoa mfano mdogo unielewe. Zamani kampuni zote zilikuwa zina section ya ulinzi au usafi. Siku hizi ulinzi siyo section au department bali ni kampuni kabisa inajitegemea na ina director wake. Ndiyo hizi security companies.

Usafi nao ni kampuni inajitegemea ndiyo hawa akina “Global Trotters” na ndiyo inayoajiri hawa mabinti wanaopiga kelele ovyo kwenye lift za majengo mengi marefu. Hawa ni wafanya usafi wameajiriwa na kampuni ya usafi.

Hivi ndivyo ilivyo sasa hivi.

Inaelekea TTCL bado imelala na mfumo ule wa “monolith company” yaani Managig Director anasimami kila kitu na board inamsimamia na kuna kamouni moja tu.

Dunia sasa hivi haiku hivyo. Ule ugomvi wa madaraka niliousema umeifikisha dunia hapa. Na isingekuwa ku-split katika “outsource” ni wazi kungekuw ana ugomvi ni nani mkubwa na ni nani aajiri.

Mkurugenzi wa fedha ana idara yake na watu wake wa fedha ataambiwa ajiri watu wa idara yako tuachie mambo mengine sisi. Hivyo huwezi kusema per se kwamba mhusika na fedha kama “Treasury Registrar” ndiye awe mwajiri kwa sababu ni msimami kama anavyosema Bashe.

“Treasury Registrar” anaweza kuona “financial position” ya kampuni . Lakini “financial position” inatokana na vitu vingi. Unahitaji professional experts wazuri na yeye hawajui anawajua wallet waliomaliza mambo ya accounts. Hajui customer care wazuri au hajui kabisa hata customer care ni nini na hawa ndiyo wanaokutana na wateja.

In fact mimi kama mteja wa TTCL au kampuni yoyote mtu wa muhimu kwangu ni Customer Care maana ndiye ninayemalizana naye kwa mambo mengi.

Hivyo, kampuni haiendeshwi kwa kuzingatia mtaalamu wa pesa vinginevyo mtu ambaye hakusoma accounts asingeweza kuanzisha kampuni au kuendesha kampuni.

Ninakubaliana na Bashe kwamba ni tatizo kumuweka Waziri awe appointing officer lakini ninakataa solutionyake kwamba appointing officer awe “Treasury Registrar”.

Kuna option ameiweka lakii hakuisema sana. Kwamba hizi position ziwe competitive yaani zitangazwe na zigombaniwe. Naposema hivyo anamaanisha position za board members. Ukitaka kuwa board member basi nafasi itangazwe na tugomee mimi na wewe.

Unaweza kudhani ni sahihi na rahisi lakini tuuchambue mfumo huu. Hivi kweli hapo Tanzania watu wanajua na kufuatilia mambo yanayofanywa na bodi zetu? Bashe kasema vizuri kwamba kuwe na quarterly report yaani ya miezi mitatu na si ya miezi sita kama inavyopendekezwa kwa TTCL.

Lakini hata kama kungekuwa na monthy report turejee kwenye swali la mwanzoni, je kazi za bodi nyingi ni nini? Swali hili jibu lake ni moja kote seikalini na kwenye private sekta kwamba kazi za board mara nyingi ni kama hakuna. Inawezekana kabisa kuendesha kampuni yoyote ya sekta binafsi au sekta umma bila hata kuwepo na bodi ya wakurugenzi.

Bodi ni kikao kinachokaa sanasana wiki nzima wakati kampuni huendesha shughuli zake kila siku. Wengi huwa hawana uelewa wa shughuli za kampuni wakati biashara inahitaji ubuinifu wa kila dakika.

Hivyo mwenye kuelewa mambo mengi ya kampuni ni executive director yaani Managing Director na executive director wenzake. Hawa wanaokuja kucnywa chai kwenye kikao cha bodi ni vigumu kupinga hoja za Executive Director labda tu awe si mwadilifu na fisadi. Lakini kama ni muadilifu board members watakuwa wanapiga usingizi kama bungeni hawana la kumpinga maana yeye ndiye anayeendesha na anajua challenge zinazozaliwa kila leo katika sekat tena challenge zingine hazikuonekana mapema na bodi.

Hivyo mfumo huu ndiyo ubovu wake, bado tunaamini sana uwepo wa bodi. Ni mfumo huuhuu umefanya bodi zifukuzwe na zitaendelea kufukuzwa au kutumbuliwa kila leo kwa sababu biashara ya kampuni ukweli ni kwmaba haimo mikononi mwa bodi bali imo mikononi mwa executive directors yaani Managing Director na executive directors wake.

Tena hata nawa wamechoka siku hizi na nimesema kwamba wame-split kampuni na kugawa kazi katika vikampuni vidogovidogo vinavyoitwa “outsource”. Ndiyo hawa akina EROLINK, HUAWEI nk.

TTCL au hata TANESCO ikubali na iendane na hali ya sasa. HUwezi kuwa na kampuni kubwa imesamba anchi nzima ukaweza kui-manage hata kama inasimamiwa na Waziri anachokipinga Bashe au hata ikisimamiwa na “tresures registrar” anavyopendekeza Bashe.

TTCL na TANESCO zinatakiwa kuwa split na kampuni ndogondogo zifanye kazi kama makampni makubwa yote yanavyofanya kwa miaka zaidi ya kumi sasa.

Kingine alichojisahau Mheshimiwa Bashe ni pale anaposema nafasi za bodi au hata ukurugenzi ziache kuwa appointment ziwe zinatangazwa. Nimeshasema ni wazo zuri lakini anakosea kusema eti “private sector” wanafanya hivyo.

Ndugu zangu JF, hebu niambien ni kampuni gani ya binafsi ilishawahi kutangaza nafasi za “u-director” au nafasi za “board members”? Mimi binafsi sijawahi kusikia na kama ni uzembe wangu nikumbusheni.

Ninachojua watanzania wengi hawajawahi kuwa na cheo hiki cha “director” hukohujo kwenye “private sector”. Chagua kampuni kubwa za wawekezaji nchini na uniambie ni kampuni ngapi zina “Managing Director” mtanzania. Hakuna.

Lakini kampuni hizohizo utakuta zimeweka “Board Chairman” mtanzania, tena mwanasiasa, kitu anachokikataa Bashe. Spika mmoja wa Bunge aliwahi kuwa “Board Chairman” kampuni moja kubwa hapo nchini hadi aliposakamwa kuhusu "u-board member wake" akawajibu wanaomsakama kwamba “wana wivu wa kike”.

Huyu ni mwanasiasa na nafasi yake huko haikutangazwa kwala ugombewa bali aliitwa na kupewa kwa vigezo viijuavyo hiyo kampuni na kampuni kubwa sana hadi leo ipo. Na iliendelea na mtindo huohuo wa kupata wanasiasa kuwa "ma-Board Chairman".

Lakini tujiulize. kkwa nini hawa kampuni binafsi kwenye Board wanaweka watanzania lakini executive director hawathubutu kuweka mtanzania?

Mtokeo yake hakuna mtanzania unayemsikia kuwa ni “Managing Director” kwenye hizi kampuni binafsi.

Sababu nimeshaisema nayo ni kwmaba bodi nyingi ni kama rubber stamp tu ni kama hazina kazi kwani kazi kubwa wanafanya executive directors yaani Managing Director, Finace Director au Operations Director.

Na siku hizi kazi zinafanywa na "oustsource companies" wanawekeana KPI agreement maisha yanakwenda.

Hivyo ukiwadanganya watu kwamba kwenye bodi za kampuni biafsi kuna watanzania wenzenu na sisi tunapofuka kama wajinga tukijidhani eti watanzania nao tuna maamuzi katika kampuni binafsi kumbe ni change la macho.

Hivyo, hata huko private sekta anakokusifia Bashe bado kuna uozo uleule kwamba appointments bado ni za kuteuliwa kama serikalini wala hakuna interview au tangazo lolote.

Ongezeeni mnayoyajua tukijua tunajadili hatima ya shirika letu TTCL na mengine
-------------------
jidanganyane kuwa kuna kampuni ya biashara inayomilikiwa na serikali inaweza kushindana kwenye soko, hii sinema ya miaka miwili hii tutaiona sii zaidi ya miaka miwili ijayo. no way
 
jidanganyane kuwa kuna kampuni ya biashara inayomilikiwa na serikali inaweza kushindana kwenye soko, hii sinema ya miaka miwili hii tutaiona sii zaidi ya miaka miwili ijayo. no way

Heri yenu mnaoelewa.
 
Mkuu DubiriJibu here is what you need to know:
In a bid to cut operational costs while growing their business, companies these days rely on outsourced help. Outsourcing is an arrangement where a company delegates internal roles or services to a third-party firm. The setup differs from one company to another, depending on their needs and goals.
Below are the five common outsourcing models.

  1. Staff augmentation
Not all companies hire outsourced help so they can push some tasks off their plate and focus on other more important things. Sometimes, companies outsource because they need more skilled people but don’t necessarily need their services full time, or don’t have the resources to pay for it. This is where staff augmentation comes in. This model is usually used when a company decides to offer add-on services that they currently lack, e.g. support services for market expansion.

  1. Project-based outsourcing
As the name suggests, project-based outsourcing applies to companies with one-off or irregular projects. Often, these projects are of low to medium complexity and have well-defined requirements and deliverables. Companies outsource these projects so they can have a dedicated team to take on the job, causing little to no disruption to their regular operations.

  1. Out-tasking/Contracting
This approach involves the transfer of a specific process or service from a company to the outsourcing partner. Out-tasking engagements are best for business owners who wish to keep control over the process being outsourced. It may involve licensing, wherein the buyer obtains permission to use the other company’s intellectual property, or contracting, wherein the external supplier performs a set of tasks or manages a group of processes for the buyer. Contracting is somewhat similar to staff augmentation in that labour is used on an hourly, daily, weekly, monthly or yearly basis.

  1. Managed services
Managed services refer to the proactive management of backend office functions or infrastructure by a third party on behalf of a company. In other words, a managed service provider (MSP) assumes all ongoing responsibility for handling, monitoring and problem solving for selected business functions. Managed services are common for IT functions, but this may also include outsourcing of HR activities, daily operations and production support.

  1. Offshoring
In this outsourcing model, a company locates its own dedicated resources in another country. A good example of this are Australian companies relocating their contact centres in the Philippines. This allows them to leverage top talents at a relatively lower price, while maintaining control over their process and service delivery. Offshoring also allows companies to get closer to their clients and to gain access to new market opportunities.

Conclusion
Choosing an outsourcing model that fits your business can give you the flexibility and capability to achieve your goals and sustain your growth over time. More importantly, the success of an outsourcing project depends on the third party you work with – so choose only the best outsourcing partner.
 
Mkuu DubiriJibu here is what you need to know:
In a bid to cut operational costs while growing their business, companies these days rely on outsourced help. Outsourcing is an arrangement where a company delegates internal roles or services to a third-party firm. The setup differs from one company to another, depending on their needs and goals.
Below are the five common outsourcing models.

Mkuu,

Thanks for the post ninayajua yote hayo. KWa kifupi mimi binafsi niko kwenye "outsource" ninaongea kitu practical to me.
 
Mkuu hapo umejibu kama great thinker bila mihenuko! Tunaweza kuendelea na mjadala.

Thanks for the post ninayajua yote hayo. KWa kifupi mimi binafsi niko kwenye "outsource" ninaongea kitu practical to me.[/QUOTE]
 
jidanganyane kuwa kuna kampuni ya biashara inayomilikiwa na serikali inaweza kushindana kwenye soko, hii sinema ya miaka miwili hii tutaiona sii zaidi ya miaka miwili ijayo. no way
Really? Rafael Defense Systems (Israel), BBC (UK), SA Airways (RSA) to mention a few

List of government-owned companies - Wikipedia

Tatizo sio nani ni mmiliki bali ni jinsi Kampuni/Shirika linavyoendeshwa. Hilo ndilo tatizo la msingi na sababu kama hizi zako ni vichaka vya kujifichia vinavyopaswa kutiwa kiberiti!
 
  • Thanks
Reactions: NOD
Back
Top Bottom