Ninalaani vikali udhaifu wa Kiti cha Spika na aibu ya Taifa letu

Mwanakijiji kama ulivyosema kiti cha spika ni dhaifu na siwezi kuongeza kwa maelezo yako maana yanajitosheleza bali itoshe kuongeza kuwa mimi naomba tuwaunge mkono wabunge wa upinzani walioko pale bungeni. Tuwe na joint project kuanzia na kuendelea ambayo iwajumishe great thinkers wa jukwaa hili na wasomi wetu wote, wanasheria, vyama vya taaluma, wanaharakati na watu wote katika umoja wao. Tutumie kila njia (channels at disposal) kuhakikisha spika na makamu wake wanapata ujumbe in black and white kuwa wanachokifanya is boomerang kwao na wenzao CCM.

Na tuendelee kushinikiza na kushauri katika mchakato wa Katiba Mpya ingawa unaonyesha kubakwa na kuibeba CCM kuwa spika lazima asitoke chama chochote cha siasa na afanyiwe usaili wa waziwazi kupitia chombo chenye masafa mapana kinachoonekana asilimia kubwa ya Tanzania ili tumpime. Na viwekwe vipengele vya kumwajibisha atakapoluwa anaenda kinyume cha sheria, kanuni na taratibu. Hii itatuondolea speaker king/queen kama alivyo wa sasa na amewaambukiza wenyeviti wa vikao vya bunge.

Ushauri kwa CDM tushawaona speaker na naibu walivyokuwa biased and prejudiced against you. Msichoke maana sisi tulio nje tunaangali utetezi wenu ulivyo na maslahi mapana kwa nchi. Mtu anasiamama kutetea usalama wa Taifa ambao tayari umetuhumiwa kuwa usiguswe, Kweli? Wananchi walikuchagua kwenda kuwa kama dodoki wa kumeza kitu bila kuchuja?

Kwa wananchi naomba tuamke na sheria hizi za watu kuwa hawaguswi hata kama wanahatarisha usalama wetu tuzikatae. Mbona zamani idara hii iliheshimiwa na ilikuwa haisemwi. Kwani hawakuwepo. Walikuwepo lakini walilinda usalama wetu sisi waajiri wao na ndio tukatunga sheria ya kuwalinda. Sasa mambo wamebadilika na lazima sheria hizi ziondolewe na wamulikwe
 
Napata wakati mgumu kupata ukweli wa mambo yanavyoenda katika bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Na mpaka sasa najaribu kutafakari ili kubaini kama nani hasa anasababisha vurugu zitokee bungeni. Binafsi naona kama naibu spika amekosa weledi wa kutumia kanuni nabadala yake kutumia hisia binafsi na hasa anapoacha kanuni zitumike kwa baadhi ya wabunge na hasa wa upinzani na kuacha wale wa chama chake watumie kanuni wanavyotaka. Naibu spika anaonekana kutokuwa na urafiki wa kauli za Tundu Lissu na hivyo kutaka kwa namna yoyote aweze kumzuia kuzungumza kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa kambi yake na inapotokea naibu spika kutotumia busara ya kumsikiliza kikanuni anapandwa na jazba na hivyo kuvuruga kikao cha bunge.
kwa maoni yangu mtu anayefanya bunge kuonekana kama lilivyo ni naibu spika kwani Mheshimiwa spika hata siku moja hajavuruga kikao cha bunge. Chuki ya naibu wa spika dhidi ya baadhi ya wabunge wa CHADEMA ndiyo inayomwongoza kuchukua maamuzi kama yaliyotokea jana kwa kufikiri kuwa anawadharirisha bali anawapaisha kwa sababu hoja wanazozitoa ndiyo mambo wananchi wanaona na wanataka yawe nami nikiwa mmojawapo. Viongozi wa bunge wamewaacha wabunge watetee vyama vyao badala ya kusemea wananchi. Ifike mahali mbunge yoyote akiwa anatoa hoja bungeni asiingize hisia zozote za kichama la kiti cha spika kitoe dira ya kinachotakiwa kuzungumzwa na kila mbunge. Vikao vyote naona wabunge hawazungumzii hoja zinazowasilishwa na serikali kila anayepewa nafasi anazungumza mambo tofauti na hasa kupigana vijembe na mipasho na hasa CCM na CHADEMA. CUF sijawasikia sana japo baadhi wanafanya kama wenzao. Ushauri aliotoa mzee LEIZER si wa kupuuza hata kidogo na hasa kwa wabunge wanaootumia hisia za kichama zaidi badala ya hisia zinazotokana na Matatizo ya wananchi. Na hapa siwezi kuacha kutolea mfano wa Mh. John Mnyika, mchango wake ulikuwa na data na hisia zinazotakiwa kuoneshwa na kila mbunge na si wengine kama Mwigulu Nchemba na Joseph Mbilinyi.
Naomba maoni yako juu ya hisia na Naibu spika dhidi ya hatua anazochukua kwa Tundu Lissu na hasa kikao cha jana tarehe 17/4/2013.
 
  • Thanks
Reactions: Awo
When the centre of gravity does not hold the falling is definitely not unexpected! It reminds me of the three books by the late Chinua Achebe which have been named as the African Trilogy which we used to join them together in school to make a sentence: "Things Fall Apart" because "The Arrow of God" is "No Longer at Ease." Naunga mkono hoja ... Kiti cha Spika kinalidhalilisha Bunge!
 
The trueth ni kwamba naibu spika kashindwa kuendesha bunge bila upendeleo kwani anataka wabunge wote wawe wanasema vizuri viongozi na ccm na ikitokea mbunge yeyote akiisema ukweli ulivyo kuhusu utendaji mbovu wa serikali naye anachukia akiwa ndiye mwendeshaji wa bunge.Naomba abadilike na apunguze chuki dhidi ya Tundu Lissu.
 
Chadema wameshaliharibu Bunge.

Hamad rashid aliongoza vizuri upinzani Bungeni. Mbowe uongozi wa upinzani Bungeni umemshinda...

Laumu wabunge wako kwa kukosa nidhamu, Spika ana kosa gani?

Kweli nyani haoni kundule, mkuu mbona na wewe unaporomosha matusi humu Jf? Unaonaje ukienda dodoma ukaungane na akina sugu?

Ni dhana ya nchi kutotawalika ndo inatekelezwa, watanzania tusikubali kamwe, tumuunge mkono Spika na naibu wake kukemea aibu hizi za akina Lissu na wenzake

mChaga na siasa wapi bwana

Ukiwa msomaji wa minyoo huwezi kukosa ugonjwa wa udini na ukabila.
 
Wewe ni ZeMarcopolo ni miongoni mwa mijitu mijinga katika nchi hii ambayi inaona mbunge wa CCM akitumia F word bungeni ni sawa kwa kuwa tu bwana wako Nape atakusifia na kukupa buku tani yako.

MMM kaja na hoja ya kujadiliwa wewe unaitumia kujikomba kwa bwana wako Nape, shame on you na uvivu wako unaokufanya ushindwe kufanya kazi za halali na kuishi kwa kujipendekeza. Pia walaumu wazazi wako kwa umaskini wao ndo wamekuingiza kwenye vicious cycle
siyo mjinga, yupo kazini - mjini hapa akale wapi? CDM hamna fungu.
 
Sitaki kuamini kuwa Naibu wa Spika hakumsikia Serukamba bali aliamua "kupotezea" Nataka kumuuliza Serukamba swali moja..hivi yeye hutamka maneno kama hayo mbele ya familia yake ? sitoshangaa jibu likiwa ni ndio, na nitaihurumia familia yake kwa hilo Ila ajue sisi wengine hatukubali maneno kama hayo mbele ya familia zetu au watu tunaowaheshimu. Na ametamka hivi baada tu ya Spika kuonya ukosefu wa nidhamu bungeni. SERUKAMBA AADHIBIWE..Ni vipi wengine wawe na nidhamu iwapo chama tawala ndio watakuwa vinara wa utovu wa nidhamu ? Ni vipi tuendelee kuliita bunge tukufu iwapo matusi mazito yanatamkwa ndani yake ? atafanywa nini muumini wa dini yeyote atakayetamka neno chafu kama hili ndani ya nyumba ya ibada ? Spika onyesha uungwana kwa kumuadhibu Serukamba..
 
never expect anything good to come out of this parliament which is constantly steered by personal vendettas, party standups abd manifestos and purely favouratism!!
 
Chadema wameshaliharibu Bunge.

Hamad rashid aliongoza vizuri upinzani Bungeni. Mbowe uongozi wa upinzani Bungeni umemshinda...

We naona una matatizo makubwa sana au unajitia uchizi,mpe Sitta heshima yake bwana Sitta alillimudu bunge letu vizuri sana anayetuaribia bunge sasa hivi ni spika na naibu wake hilo lipo wazi kama wewe ni mshabiki tu na si mtaka ukweli najua utapinga hili mfano mzuri wa jana Serukamba
 
Nia na sababu ya jana Naibu spika kumuweka LAmeck awe wa mwisho na kumuambia ataongea ddk 10 kama vile yeye mwenyewe hajui anaongea dkk ngapi ilikuwa kitendo cha makusudi cha kupangilia uongo wao. Alikuwa msemaji wa mwisho kwa makusudi na bahati mbaya akaanza kuongea uongo na kila sentensi aliyokuwa anaitamka ilikuwa ni uongo. Ni dhahiri anayeharibu bunge ni CCM ikiongozwa na mjumbe wa nec Ndugai!!!
 
Tunachoshuhudia Bungeni siyo demokrasia kazini, bali domoghasia kazini. Ninalaani vikali udhaifu wa Bunge (Spika na Naibu wake), upendeleo, na lugha za kihuni za baadhi ya wabunge (wa vyama vyote) ambazo zinatufanya tuhoji kama wabunge wetu wako kutunga sheria na kusimamia serikali au wako kushindanisha nani analugha kali zaidi Bungeni.

Tunachoshuhudia Bungeni kinapaswa kisababishe maswali kwa wapiga kura kama watu hawa walioko Bungeni wanastahili kuwepo Bungeni na wapiga kura wachukue uamuzi gani dhidi yao ufikapo uchaguzi Mkuu au hata kabla. Kuendelea kuvumilia udhaifu huu wa chombo kikuu cha uwakilishi wa wananchi ni kuendelea kuvumilia udhaifu wa utawala wetu ambapo watu wanataka sifa kwa kuzungumza siyo kwa kutenda.

Spika Makinda na Ndugai wameshindwa kuongoza Bunge na sasa wanaburuza. Mpaka pale kiti cha Spika kitakapoacha upendeleo wa chama chao ndio Bunge litaongozwa kwenye misingi haki, usawa, heshima na utu. Kila mmoja akitambua wajibu wake na kwa wenzake ndio Bunge litasimama na kufanya kazi yake ya kuwawakilisha wananchi, kusimamia na kushauri serikali lakini zaidi sana kutunga sheria zenye matokeo bora kwa wananchi na mfumo wetu wa utawala.

Tunapoangalia Bunge sasa tunashuhudia udhaifu ukipewa kiti cha enzi, uzembe ukivishwa kilemba na uhuni ukishangiliwa. Tunashuhudia aibu ya taifa letu mbele ya watoto wetu. Nalaani vikali yote hayo!!

MMM

NB: Kama na wewe unajisikia kulaani vikali tuliyoyashuhudia hadi hivi sasa gonga "like" au/na andika kuunga mkono msimamo huu.

Wananchi na Hasa wanachama wa Chadema tumechoka na double standard za Serikali yetu.. Hasa katika maswala ya Mustakali wa Taifa.

Ni vizuri Mungu amepanga kuwaumbua mfano ni Juzi tu Spika alitishia kuagiza kukamatwa kwa mbunge atakayetukana imediately tukasikia Serukamba anatoa Tusi ambalo huwezi kuliandika wala huwezi kutegemea kusikia mtu kama yule analitoa hadharani....

Mimi sishangai kwani kama wanaweza kumtoboa mtu Macho, wakamng'oa Meno na Kucha bila ganzi sembuse Matusi???
 
Tunachoshuhudia Bungeni siyo demokrasia kazini, bali domoghasia kazini. Ninalaani vikali udhaifu wa Bunge (Spika na Naibu wake), upendeleo, na lugha za kihuni za baadhi ya wabunge (wa vyama vyote) ambazo zinatufanya tuhoji kama wabunge wetu wako kutunga sheria na kusimamia serikali au wako kushindanisha nani analugha kali zaidi Bungeni.

Tunachoshuhudia Bungeni kinapaswa kisababishe maswali kwa wapiga kura kama watu hawa walioko Bungeni wanastahili kuwepo Bungeni na wapiga kura wachukue uamuzi gani dhidi yao ufikapo uchaguzi Mkuu au hata kabla. Kuendelea kuvumilia udhaifu huu wa chombo kikuu cha uwakilishi wa wananchi ni kuendelea kuvumilia udhaifu wa utawala wetu ambapo watu wanataka sifa kwa kuzungumza siyo kwa kutenda.

Spika Makinda na Ndugai wameshindwa kuongoza Bunge na sasa wanaburuza. Mpaka pale kiti cha Spika kitakapoacha upendeleo wa chama chao ndio Bunge litaongozwa kwenye misingi haki, usawa, heshima na utu. Kila mmoja akitambua wajibu wake na kwa wenzake ndio Bunge litasimama na kufanya kazi yake ya kuwawakilisha wananchi, kusimamia na kushauri serikali lakini zaidi sana kutunga sheria zenye matokeo bora kwa wananchi na mfumo wetu wa utawala.

Tunapoangalia Bunge sasa tunashuhudia udhaifu ukipewa kiti cha enzi, uzembe ukivishwa kilemba na uhuni ukishangiliwa. Tunashuhudia aibu ya taifa letu mbele ya watoto wetu. Nalaani vikali yote hayo!!

MMM

NB: Kama na wewe unajisikia kulaani vikali tuliyoyashuhudia hadi hivi sasa gonga "like" au/na andika kuunga mkono msimamo huu.
Nikweli kabisa meza kuu imekuwa dhaifu kupita kiasi,wanasema kipindi chanyuma yakuwa bunge likuwa na busara na mvuto nikweli kabisa ila hii yote ni kutokana na meza kuu kuwa na busara na hakukuwa na aina ya wabunge kama aliyowataja Sugu.watoto katika familia wasipokuwa na nidhamu huwezi mlaumu mtoto inabidi umlaumu mzazi kwa malezi mabovu au shule isiyokuwa na nidhamu basi anayestahili lawama ni mkuu wa shule.Napenda kuwaasa na kuwashauri ndugu zangu na kuwaomba CDM kuwa makini na kukaa kimya kwa mashambulizi yanayo toka kwa CCM hii ni tetchnic wanayoitumia bungeni ili kudhoofisha upinzani na kuwafanya wasiwazie mambo yenye tija badala yake wafikirie jinsi ya kujibizana. Nawashauri wakae na kushauriana nilipi la kufanya na sii kukubali kutolewa nje au kutoka wenyewe.
 
Back
Top Bottom