Ninakwazika sijui la kufanya nisaidieni jamani

NgomaNzito

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
559
26
Mi naomba ushauri

Ninakwazika sana na sijui la kufanya, nina mdogo wangu msichana anaishi mkoani na huwa ananitembelea mara kwa mara, pia nina Boss wangu ambaye imetokea akamuona mdogo wangu bila hata kujua wamekuwa na uhusiano ye akisafiri au mdogo wangu akija Dar wanawasiliana na uhusiano huo wa kimapenzi unaendelea, sasa mimi wananificha ila kuna mtu ambae mdogo wangu anamsimulia na ye ananiambia, mimi nimeolewa na ninaheshimu ndoa yangu sana na Boss wangu ameoa na mke wake ni rafiki yangu sana sana tu.

Uhusiano wao mi siupendi kwani sijui unaweza kuni affect kwa kiasi gani kikazi na pia mke wake ni rafiki yangu. Wao wanadhani mi sifahamu kwa hiyo wanafanya vitu vyao kwa siri ili nisijue.

Naomba ushauri nifanyeje? Je ninyamaze tu kimya?
 
Usinyamaze, utaonekana unabariki jambo hilo chafu!

Huyo bwana ni mkware na mharibifu sana!

Kama alishaoa, basi uhusiano wowote nje ya matrimonial house yake ni kinyume na sheria.

Sasa, fikiria, anayemkwaza huyu bosi na kumvurugia ndoa yake ndo mdogo wako, too bad!

Mwite mdogo wako umkanye kabisa, na umwambie kuwa umegundua kuwa anapokuja Dar kumbe anakuja kuonana na bosi wako!..Mpige marufuku kabisa asikanyage kwako ili KIKOMBE HICHO UKIEPUKE, na umwambie kuwa kama atakusemelea kwa bosi wako, basi na avunje undugu..!

hAJATULIA KABISA HUYU MDOGO WAKO!
 
6149b7abd06d9c3ebe4808d75defffac.jpg
 
Usinyamaze!
Huyo bwana ni mkware na mharibifu sana!
Kama alishaoa, basi uhusiano wowote nje ya matrimonial house yake ni kinyume na sheria.
Sasa, fikiria, anayekmwaza na kumvurugia ndoa yake no mdogo wako, too bad!
Mwite mdogo wako umkanye kabisa, na umwambie kuwa umegundua kuwa anapokuja safari za Dar, kumbe anakuja kuonana na bosi wako!

Well said
 
Mi naomba ushauri

Ninakwazika sana na sijui la kufanya, nina mdogo wangu msichana anaishi mkoani na huwa ananitembelea mara kwa mara, pia nina Boss wangu ambaye imetokea akamuona mdogo wangu bila hata kujua wamekuwa na uhusiano ye akisafiri au mdogo wangu akija Dar wanawasiliana na uhusiano huo wa kimapenzi unaendelea, sasa mimi wananificha ila kuna mtu ambae mdogo wangu anamsimulia na ye ananiambia, mimi nimeolewa na ninaheshimu ndoa yangu sana na Boss wangu ameoa na mke wake ni rafiki yangu sana sana tu.

Uhusiano wao mi siupendi kwani sijui unaweza kuni affect kwa kiasi gani kikazi na pia mke wake ni rafiki yangu. Wao wanadhani mi sifahamu kwa hiyo wanafanya vitu vyao kwa siri ili nisijue.

Naomba ushauri nifanyeje? Je ninyamaze tu kimya?

...haraka sana ongea na mdogo wako umkanye huo wembe anaouchezea na jinsi makali yake yatavyowakata nyote wanne!
 
Usinyamaze, utaonekana unabariki jambo hilo chafu!

Huyo bwana ni mkware na mharibifu sana!

Kama alishaoa, basi uhusiano wowote nje ya matrimonial house yake ni kinyume na sheria.

Sasa, fikiria, anayemkwaza huyu bosi na kumvurugia ndoa yake ndo mdogo wako, too bad!

Mwite mdogo wako umkanye kabisa, na umwambie kuwa umegundua kuwa anapokuja Dar kumbe anakuja kuonana na bosi wako!..Mpige marufuku kabisa asikanyage kwako ili KIKOMBE HICHO UKIEPUKE, na umwambie kuwa kama atakusemelea kwa bosi wako, basi na avunje undugu..!

hAJATULIA KABISA HUYU MDOGO WAKO!

nafikiri fuata ushauri huu kwanza,kisha utaleta matokeo kama ulivyowasilisha hili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom