Wadau nawasalimu. Nimepata kazi huko, na naomba anayejua juu ya maisha ya huko na mengine yakunisaidia kuzoea nchi ambayo sijawahi kufika. .
1.Matarajio yangu hiyo kazi uliyopata hujaipata kupitia mawasiliano ya internet maana ukishuka tu uwanja wa kimataifa wa Murtala Mohamed huwa kuna bango limeandikwa "beware internet fraud" upande wa kushoto kwenye lango la kutokea.Hata ubalozi wa Nigeria wanapotaoa viza kabla ya kutoa huuliza huko unakoenda au huyo mwenyeji wako mumejuanaje ni kwa kupitia internet au? Sababu watu wengi wamepata matatizo kupitia hili
2.Wanigeria kwa ujumla ni watu wa dini sana.Wote waislamu na wakristo. .Usishangae ukiwa kwenye basi au ndege au kituo cha basi au airport mtu kuona anaanza kusali kwa sauti bila kujali watu waliopo.Kama ni marafiki utawapata makanisani na misikitini.
3.Wizi wa kutumia silaha na wizi wa mifukoni kule kiwango kidogo mno.Matukio ya ujambazi ni nadra kuyasikia.Unaweza kuta mtu kakaa sokoni,stendi nk anafanya biashara za pesa za kigeni akiwa na mamilioni ya pesa za kigeni na za nigeria kakaa anauza lakini hakuna mtu wa kumvamia wala kumfuata kumpora akifunga biashara jioni.Ukiwa mgeni unaweza ogopa kubadilisha kadola mia kako nakutoa wasiwasi badilisha tu wala usiogope.Mara ingine hata madreva taxi huwa na mapesa kibao ya kigeni kwenye buti anakubadilishia hapo hapo
4.Wizi na utapeli mkubwa wanigeria huufanya nje ya nchi yao au kumtapeli mtu kwa njia ya internet lakini utapeli wa ana kwa ana nchini si rahisi sana.
5.Ndani ya nchi wanigeria ni wakarimu sana ila hawababaikii sana wageni toka nchi zingine.Wengi wao wameasafiri nje sana kwenye nchi za jirani na nje pia wana ndugu wako nje wengi kwa hiyo usije nyanyua mabega sana kama wewe kutoka Tanzania ni kitu kikubwa sana.
6.Wanawake na wanaume wote wako aggressive na bullying usitarajie kama ni mwanamke au mwanaume utapata mwanamke au mwanaume mpole mpole na wa kukunyenyekea kama wanaume na wanawake wa Tanga.Lugha laini laini na macho ya kurembua mwisho utaviona uwanja wa ndege wa Dar es salaam
7.Mabosi wa kinigeria hupenda kunyenyekewa mno kupita kawaida hivyo anza kujipanga mapema.Kule kazi ni shida kwa hiyo mtu akiipata na akiwa Bosi anajiona ni kama Mungu mtu na anataka kila aliye chini yake alijue hilo.Bosi wa kinigeria mchukulie kama baba yako au mama yako utakaa vizuri kazini.Akipita msalimie ila usimpe mkono wewe kwanza yeye ndie akupe.Kama ana mizigo mkononi mwombe kama unaweza msaidia kubeba.Be very humble.Utaishi vizuri na watakupenda.
8.Wanigeria ni waongeaji sana na hupendwa kusikilizwa.Kwa hiyo wewe hata uwe kidomo domo jitahidi kutokuwa mwongeaji sana utembee na plastic mdomoni kuziba kidomo domo chako.Uwe unaongea maneno machache uwaache wenyewe wabwabwaje
9.Kwa ujumla wanigeria wengi wana hela na wanapenda maisha mazuri.Hivyo usishangae kuona bei za vitu ziko juu kuliko kwetu kuanzia nyumba za kupanga,bei za vitu nk
10.Kosa kubwa usijethubutu kufanya ni la kudharau chochote cha mnigeria.Hawapendi hata kama ni kweli.Hata ukiona wanakiongelea usijitie kuchangia hawapendi mgeni kuwakosoa! Hata wakikukaribisha kwao na kukulisha chakula kibaya na kukulaza pabaya onyesha shukrani ila kimoyo moyo ujiapishe kuwa hujirudi kula na kulala pale tena!!!
11.Kiwango cha uchapa kazi ni kikubwa.Wanafanya kazi sana.Hivyo jitahidi usiangalie masaa bali maliza kazi za watu
12.Usijionyeshe kuwa una pesa wanapenda sana dezo hata kama wanazo.Wao wagumu kutumia pesa kutoa ofa lakini kwa kutaka ofa kwa wengine ndio wenyewe.Kwa ujumla ni wachoyo!!!
13.Usiogope kutumia usafiri wa mabasi,taxi nk wala kutembea popote ila vizuri wakati wote uwe na passport yako.Kuulizwa kitambulisho na askari barabarani hasa kama unasafiri kutoka jimbo moja kwenda jingine ni kitu cha kawaida.
14.Penda kuvaa mavazi ya kinigeria ili usionekane kunguru katikati ya njiwa.Ukivaa kinigeria watakuwa wanakuchukulia kama mnigeria kumbe mbongo!!!!
15.Vyakula vingi kama hutaki vya kinigeria nenda supermaket ziko nyingi utapata hivyo unavyovipenda.
16.Wazee wa Nigeria wana heshimika mno tena sana.Kama uko jirani naye au mnaishi nyumba moja hakikisha unawaamkia vizuri na kuwaheshimu.