Ninafanye nini nioe?

lukatony

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
637
500
Habari!wapendwa naomba ushauri kidogo,kwa umri nilionao napaswa niwe na familia,am above 30yrs.Nimekuwa kwenye relation za kudumu yapata tatu sasa lakin zote zimeishia kuparaganyika mwishoni.
Ya kwanza iliparaganyika Sababu mi niliamua kusitisha mahusiano baada ya kugundua Ana mahusiano mengine na ambayo kiukwel may b yalichangiwa na umbali uliokuwepo baina yetu,we stayed with her for 3yrs,mkakati ukiwa kuja kuoana lakin wakati sasa tukielekea huko ndipo nilipogundua Ana mahusiano kayaanzisha recently,alikanusha pamoja na uthibitisho mwingi,ok sababu nilikuwa nampenda nilishindwa kumuacha,baadaye nilipogundua mchezo unaendelea na yule mtu wake nikaamua kumuacha.
Wa pili yeye tulikaa miaka miwili,alipomaliza Chuo na kupata kazi sehemu nyingine haikupita hata mwaka nikanyanganywa nikakubali
matokeo,nikaanza upya pamoja na kwamba tulishapanga mpaka kuoana mitakuwa mwezi wa ngapi,nikapiga konde Nikakubali matokeo.
Wa tatu ndo huyu sasa tunaelekea kuachana baada ya miaka miwili naye.Maana kapata kazi nzuri in a private company na mkoa mwingine na kwa sababu she is graduate na alikuwa hana kazi ka accept qickly.
Sasa nijuavyo Kuna kila dalili za Kuachana huko mbeleni.
Kwa nini nasema hivi?Scenario zote za nyuma zilisababishwa na umbali.
Na Sababu kubwa ni kwamba pamoja na kwamba am not handsome,cku zote napenda wasichana wazuri.
Sasa wadau nifanyeje nioe nami?
 

gwabos

Senior Member
Dec 5, 2013
112
0
Kumbe unapenda wazur..!i
bas wapo kibao kama Wema sepetu,shilole,wolper,uant ezekiel,lulu, masogange, binti kiziwi basi mwanangu endelea et.....?utapata tu!
 

kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
36,719
2,000
kiongozi, ukisema sio handsome ujue uwe na pesa... mwenzio mimi mfupi mbilikimo ila ninamkwanja..... nimeoa graduate...!
:cool2:
 

chriss makoba

Member
Oct 5, 2012
50
95
Unataft demu au mke! Maana unazungumzia uzur, na kama hoja n wazur endelea kutaft, ila bado hujapanga kuoa kimawazo ila mwil ndo unakusukuma
 

UWOGA=UMASKINI

JF-Expert Member
Dec 30, 2013
2,364
2,000
We wataka mzuri wa sura au wa moyo.wazuri wa sura ni wengi sana ila wa moyo ni wachache mno.waonaje ukiwa na mke mkali ila ni jamvi la wageni au mbaya wa sura ila anakuheshimu
 

Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
6,842
2,000
Inaonyesha unaremba mno ndo maana wanasepa.......ukisema ww siyo mzuri na unapenda wanawake wazuri maana yake hata hao uliokua nao ni wazuri ilikuwaje wakakubali kuwa na ww? kuna bindamu anapenda mwenzi wake awe mbaya? na ww ni nan alikuambia kuwa ww ni mbaya? Sema unajivuta mnoo haonekani kama ni mtu una malengo ya kuoa ndo maana wanakimbia,maana siyo kumwambia mwanamke kuwa nitakuoa ndo kunakuhakikishia kummiliki anaangalia hata mipango hiyo ipooo......we miaka mitatu bado unamwambia tu nitakuoa na bado yupo tu siku hizi wanashituka ati,ww ni mzuri tu jiamini tu maana umeshaanza kuonyesha wasiwasi hata kwa huyo mwingine eti kisa kapata kazi mkoani kwani huko mkoani hakufikiki?
 

majeshi 1981

JF-Expert Member
Dec 7, 2013
2,093
1,500
Sababu kubwa ni kwamba pamoja na kwamba am not handsome,cku zote napenda wasichana wazuri.
Sasa wadau nifanyeje nioe nami?

pole sana kamanda, mwanaume hasifiki kwa sura bali uwezo wake wa kuanzisha na kuitunza familia yake, mfuate huyo mke wako mtarajiwa hukohuko aliko, kama unakazi nzuri ya kudumu kuliko mchumba wako mshauri aache na mkae pamoja, kinyume na hapo utaibiwa tu!
 

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
12,565
2,000
umesema we stayed with her for how long?. hao magraduate watakua wwanakuacha sababu ya ngeli. kwani unaelimu gani mkuu?
 

kat.ph

JF-Expert Member
Dec 19, 2013
2,228
2,000
Distance sio sababu.... una tatizo mkuu. Pocket yako inasoma? Maana mabinti wazuri bila hela utaishia kuwaita shemeji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom