Ninachotamani: Lady Jaydee na Clouds media Group wamalize tofuti zao

warumi

R I P
May 6, 2013
16,273
18,422
Najua hii ni mada ngumu kidogo lakini wazungu wanasema ‘lets address the elephant in the room.’
Kwa takriban miaka mitatu sasa, vituo vya Clouds Media Group vimeacha kupiga kazi za Lady Jaydee kufuatia mgogoro mzito uliozuka kati yake na uongozi wa kampuni hiyo. Kiukweli huu haukuwa ugomvi mdogo, ulikuwa mkubwa na ulifika hadi mahakamani. Ugomvi huu ulitawala vichwa vya habari kwenye vyombo vya habari nchini.
Sina uhakika kama kesi ilikwishamalizika, lakini ninachofahamu ni kuwa katika kesi hiyo iliyofunguliwa na kampuni ya CMG ilimzuia Jide kutowataja tena wamiliki/viongozi wake kwenye mitandao ya kijamii kama alivyokuwa akifanya wakati akitoa malalamiko yake.
Kinachoonekana kwa wengi ni kuwa Lady Jaydee aliweza kusurvive bila nyimbo zake kuchezwa na vituo vya kampuni hiyo (Clouds FM, Clouds TV na Choice FM) na vile vile kampuni hiyo imeendelea kukua bila kucheza nyimbo za msanii huyo. Kwahiyo pande hizi mbili zinaweza kuishi bila kutegemeana kwa chochote – life goes on and everyone is happy. Lakini kuna upande mmoja wa shilingi unaosahauliwa kwenye mgogoro huu ambao mimi ninauona mkubwa zaidi – mashabiki.
Lady Jaydee ana mashabiki wake, wengi sana, Clouds Media Group ina mashabiki wake, wengi sana. Na katika mashabiki hawa, wapo ambao ni mashabiki wa pande zote mbili. Shabiki wa Clouds FM ambaye pia ni shabiki wa Lady Jaydee ndiye anayeathirika zaidi hapa. Well, kuna redio na TV nyingi sana ambazo nyimbo za Jaydee zinachezwa, lakini kuna aina ya mashabiki ambao upenzi juu ya kituo kimoja cha redio au TV ni mkubwa zaidi ya unavyoweza kufikiria.
Kuna wasikilizaji damu damu wa Clouds FM ambao hakuna redio nyingine wanayoisikiliza kwa sababu wanazozijua wenyewe na katika hawa wapo ambao ni mashabiki wa Lady Jaydee. Mkanganyiko huu unawaweka njia panda Clouds FM pale ambapo mashabiki wanapoomba wimbo wake na wakanyimwa kwa sababu ya mgogoro huo.
Lady Jaydee alikuwa kimya kwa muda mrefu kabla ya Jumapili ya March 20 kuachia wimbo wake mpya, Ndindindi. Ni wimbo mkali sana na ni kama muimbaji huyo aliutumia ukimya wake kuchaji kipaji chake na kukirejesha kwenye kilele chake. Ni wimbo ambao hakuna shaka utakuwa namba moja kwenye vituo vingi vya redio, kasoro Clouds FM au Choice FM kwasababu nilizozieleza mwanzo.
Kingine hakuna anaweza kubisha ukweli kuwa Clouds FM ni redio inayosikilizwa zaidi na mchango wake katika sekta ya burudani ni mkubwa. Japo kama nilivyosema, kwamba Jaydee ameweza kusurvive bila wao, Clouds FM na vituo vyake vingekuwa na mchango mwingine tena kwake kama vilivyokuwa nao kabla hawahitilafiana.
Ieleweke kuwa, hakuna ninayemlaumu katika pande hizi mbili kwakuwa kila mmoja ana maisha yake na kama nilivyosema ‘everyone is happy’, lakini wakivaa viatu vya mashabiki niliowalezea hapo juu watanielewa.
Kuna haja ya mgogoro huu ukaisha sasa. Hakuna jambo lisilokuwa na mwisho, hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Lady Jaydee na Clouds Media Group hawana budi ‘kubury the hatchet’, kuyaacha yaliyopita na wagange yajayo.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja, Alikiba na Diamond walikuwa na mgogoro pia na vituo vinavyomilikiwa na IPP Media. Katika kipindi hicho, hukuweza kusikia nyimbo zao zikichezwa Radio One, East Africa Radio wala Capital FM na pia video zao hazikuchezwa EATV wala ITV. Lakini hivi karibuni wamemaliza mgogoro wao (mimi na wewe hatujui ulianzia wapi) na sasa mambo yamerejea kawaida.
Pamoja na kwamba sababu zinatofautiana, lakini nadhani Lady Jaydee na Clouds Media Group nao wanaweza kuuzingatia ule usemi wa wahenga kwamba ‘yaliyopita si ndwele…….
 
Ndio maana muda mwingine huwa wanasema funika kombe mwanaharamu apite..

Jide anamashabiki sawa, ila Clouds haipungukiwi kiasi chochote cha mapato yake kwa kutokujihusisha nae, ila Jide anahasara kwenye hii situation. Ajitambue, ajishushe wayamalize
 
Huwajui clauds ww,ukiwanyenyekea watakufanya kama wamekuzaa,jide aendelee na ishu zake kwani kuna ataeishi milele?kama rizki anapata kuna haja gani ya kufanywa mfunga kamba za viatu?
 
Huwajui clauds ww,ukiwanyenyekea watakufanya kama wamekuzaa,jide aendelee na ishu zake kwani kuna ataeishi milele?kama rizki anapata kuna haja gani ya kufanywa mfunga kamba za viatu?
Hakika..wamemfanya mond now kuhisi hawezi kuwa bila wao..alohombana na diva Matokeo yake aliomba msamaha tena kwa barua.huo si ujinga jamani
 
Riziki upanga Mungu. Alicho panga yy mwanadamu awezi pangua. Clouds sio wapanga mafanikio.. Jide alikuwepo na ataendelea kuwepo. .......Mara nyingine binadamu kumnyenyekea ni sawa na kutojiamini na wakati anatumia kipaji chake....... Jide songa mbele waonyeshe ata bila wao utaweza na kufika mbali..
 
Back
Top Bottom