Nina wapenzi wawili nimuoe nani kati yao?

Mashakamnyaka

New Member
Jun 25, 2021
1
5
Habari zenu ndugu zangu.

Nakuja kwenu na Id mpya ili niweze kuwa muwazi kwenu nipate msaada. Naona karma inaninyemelea na sielewi nifanye nini ndugu zangu.

Mimi ni kijana wa miaka 31. Sijaoa lakini nimekuwa na girflriend wengi kwa wakati mmoja bila wao kujuana.
Shida yangu ni hii: Katika wasichana wote niliowahi kuwa nao, kuna huyu msichana A. Kwa kweli tumekaa naye kwenye mahusiano zaidi ya miaka 5. Tangu nikiwa chuo. Msichana huyu sijapishana naye umri sana. Nimemzidi kwa miezi kadhaa. Ila amekuwa akiniheshimu kwa muda mrefu, akinijali tangu sina kazi hadi sasa.

Ila niseme ukweli ndugu zangu. Huyu msichana kwanza mguu wake mmoja ni mfupi mwingine ni mrefu, hivyo anakuwa kama anachechemea fulani. Licha ya hayo mapungufu ya kimaumbile, ni mtu mwenye elimu yake, mzuri sana (kwa macho yangu), hanitegemei kwa chochote hadi pale mimi ninapoamua kumnunulia kitu au kumtoa out. Otherwise hata mimi muda mwingine ananipiga tafu.

Shida ni kwamba sasa nimepata mtu mwingine ambaye nahisi tunaweza kuendana zaidi ya A. Ingawa simjui vema msichana huyu maana ni mwanafunzi wa chuo ambaye nimemzidi miaka zaidi ya 7. Tupo mikoa tofauti. Yeye ni tegemezi kwangu kwa kila kitu. Na kiukweli mara nyingi tunagombana sana na tumeshaachana mara kwa mara sababu ya huyu msichana A ambaye naye imefikia hatua kuwa sasa nichague jambo moja. Kumuacha ama kuendelea naye pasipo mimi kuwa na wasichana wengine. Jambo ambalo kwangu ni gumu sana.

Nimejaribu mara kadhaa kuongea na A na at the same time nakuwa na B kwa simu. Jambo ambalo A amekuwa mkali na sasa ninashindwa kuwa huru hata kuongea na B.

Kiukweli B naona ni msichana mdogo na pia kabila letu ni moja hivyo ninapata amani sana kuwa nitaweza kuwa na huyu binti kuliko kuwa na A. B anamaliza masomo mwaka huu na tunategemea mwakani tuanze safari ya kukaa karibu ili kujuana na hàtimaye tufunge ndoa.

Migogoro hii kwangu imekuwa kero na nimemtamkia maneno mabaya sana A ambaye amekata tamaa nami kabisa. Hanipigii tena simu na kiukweli najihisi kama nipo mwenyewe inspotokea ninapata changamoto fulani.

Naombeni ushauri wenu wadau. Je nipo sawa ama nimeyumba?
 
Habari zenu ndugu zangu.

Nakuja kwenu na Id mpya ili niweze kuwa muwazi kwenu nipate msaada. Naona karma inaninyemelea na sielewi nifanye nini ndugu zangu.

Mimi ni kijana wa miaka 31. Sijaoa lakini nimekuwa na girflriend wengi kwa wakati mmoja bila wao kujuana.


Naombeni ushauri wenu wadau. Je nipo sawa ama nimeyumba?
nyie ndo mnasababisha tuendelee kuwachukia wanaume?? sasa km ulikuwa huna mpango nae kwann ukamlead on kwann
 
Kwa hio kasoro ya A ni mguu mmoja kuwa mfupi so unaona sio type yako kutoka nae wala kuishi nae kwa sasa maana umeshakaa nae for five long years.

Kama humpendi muache tu maana utamuumiza sana mbeleni pia hakikisha huyu denti anakupenda sawasawa maana hawa watoto hawakawii kukuacha kwenye mataa akipata mwenye hela kukuzidi.

"Jini likujualo............."
 
Nimekoma kusoma hapo kwa mschana wa pili uliposema tuu, ni Mwanachuo.

Mwanachuo sio mtu wa kumuamini, uwezekano wa kubadirika huko mbele ni mkubwa. Usikute umri wake bado ni under 25.

Oa huyo mdada unaemzidi miezi tuu.

Halafu usikute huyo denti, una msomesha kwa namna moja au nyingine.
 
Ni hivi nigga Luke Shaw ana mguu mmoja mfupi.

Garrincha ana mguu mmoja mfupi.

I mean mguu mfupi siyo ishu haizuii kufanya vitu vingi so wewe ulipofikia ni ile unaona dhambi kumuacha ila unatafuta sababu ya kumuacha.

As a man naelewa ila kiukweli umenizidi umri ila nimekuzidi uzururaji so nakuhakikishia kwamba kama unataka ndoa yenye utulivu huyu Shemeji wa kwanza huyu ndiye wa kuoa. Unajua wanandoa angalau mkikaa muwe na stori zinarelate mfano wewe na A mnaweza kupiga stori kukumbushana wakati Pepsi inauzwa shilingi 150 ila huyu mpya mna hata stori mnazoweza kushea?

Choose wisely bro. Huyu mpya ni fine sawa lakini ukimuweka ndani nakuhakikishia soon utakua unajuta kurudi home hii ni kwakua kuishi pamoja ni zaidi ya kumegana.
 
B ndo anakufaaa,baada ya mwaka tunaomba mrejesho,
Japo kila siku mnatunanga wanawake et hatuna sifa za kuolewa,ila leo tuangalie kwa huyu hivi na sisi tukisema wanaume waoaji wanapungua kila siku mtakasirika?

Imagine at 31 mtu anakuja kuomba ushauri wa kipuuzi namna hii ???
Nichukue nafasi hii kumpongeza A kwa kuwa na moyo wa kipekeee maana mimi navozijua akili zangu siwezi endelea date na mtu wa aina yako(maisha yangu yote sitokuja kugombania mwanaume)
 
Back
Top Bottom