Bajeti yangu ni mil 5 ,je naweza kupata gari ambayo haitanisumbua wala kula mafuta sana?
Sitaki kushinda garage mara kwa mara na kipato changu cha kawaida,ntakua mara nyingi naitumia huko lushoto tanga kwa shughuli zangu za huko.Wakuu naomba kujua kama naweza kupata gari yenye sifa nzuri ,maana sina uzoefu nazo
Ipo Toyota Duet (Daihatsu storia) nataka 3.5m tu inakimbia kilomita 17 kwa lita moja ya mafuta tu.
Sent from my iPhone 4S using JamiiForums app
iko suzuki samurai jx ni ya kizamani kidogo lakini ni roho ya paka itakufaa sana huko bush na bei ni rahisi.