Nina tatizo la deep vein thrombosis(dvt) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina tatizo la deep vein thrombosis(dvt)

Discussion in 'JF Doctor' started by Kyemba, Aug 10, 2011.

 1. K

  Kyemba Member

  #1
  Aug 10, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 5
  Ni mwaka mzima sasa naumwa mguu, unavimba hasa nikikaa muda mrefu kama ofisini hivi,nikilala unakuwa kawaida.Madaktari wanasema damu inaganda kwenye mishipa natakiwa kutumia anticoagulants maisha yangu yote na siruhusiwi kubeba mimba.
  ISSUE.
  Sijabahatika kupata mtoto hata mmoja na nipo kwenye ndoa, je wanajamiii kuna mtu aliwahi kuwa na ugonjwa kama huu akapata mtoto?
  Na je huu ugonjwa unatibika? Na hospitali gani wanaweza kunisaidia au nitumie nini ili nipone maana napata tabu sana.Jamani naomba msaada wenu.
   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Muombe mungu atakupa njia na utapona na kupata mtoto
  Pole dear but jali zaid afya yako kwa sasa fuata ushauri wa madr.
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  DVT huwapata watu wengi, wake kwa waume wa marika yote.Bahati mbaya wengine hupoteza maisha kwa vile hawapati mabingwa wa ku diagnose hili tatizo mapema.

  Bila hata kuingia kiutabibu kwa kutumia uzoefu, nitakuambia kuwa jitahidi sana kutokuwa kwenye position moja kwa muda mrefu hasa kuketi. Hizo anti coagulants unazotumia zinafanya damu yako iwe nyepesi sana na kukuweka kwenye hatari ya ku bleed to death pale utakapopata hali ya kukufanya utoke damu!

  Kubeba mimba siyo issue, issue ni pale unapojifungua maana damu nyingi itatoka na hospitali zetu huwa hawajali kuchukua tahadhari. Nitakushauri uwaona mabingwa wa hematology kwa ushauri zaidi kwa vile unataka kuzaa.
   
 4. B

  Baikoko Senior Member

  #4
  Aug 10, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sometimes hizo dawa za dvt za kuyeyusha damu ndio zina madhara kwenye mimba. Mimba nayo inayeyushwa kama sikosei
   
 5. doup

  doup JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Naamini kwa uweza wake Mungu lolote lawezekana, fuata ushauri wa madaktari na unaweza fanikiwa pata mtoto
   
 6. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Nenda SCOAN kwa TB Joshua! Wengi wamesaidiwa!
   
 7. K

  Kyemba Member

  #7
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 5
  Nashukuru sana wana jamii kwa ushauri nitajitahidi kuufuata.Je anticoagulants naweza ziacha

  ?
   
 8. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  ni hospitali zipi hizo unazosema?hawa mabingwa wanapatikana hospitali hizi hizi zisizojali?
   
 9. m

  menny terry Senior Member

  #9
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mama kwanza pole sana kiukweli tatizo halina dawa ya maana wasikudanganye kuwa eti kuna madaktari bingwa mabingwa.Nasikitika kukuambia hili ila ni mwaka jana mama angu mkubwa ambaye naye alikuwa na tatizo kama lako lakini akaamua kubeba ujauzito lol! Damu ilimtoka sana lakini kama ujuavyo MUNGU mkubwa akaponea chupuchupu lakini mtoto akafa baadae hali ikazidi kuwa mbaya sana ndipo tulimpeleka kwa TB JOSHUA kwa maombezi chaajabu Akapona na leo anawatoto wa nne.Kiukweli hata ukienda India hutapata tiba ya maana kwani na sisi ilikuwa hivyo.Ushauri nenda kwa TB JOSHUA kama kweli unataka kuishi au kama unataka kufa endelea kung'ang'ania hao madokta.
   
Loading...