ndugu yako
Senior Member
- Mar 30, 2013
- 193
- 97
Katika kipindi nilichokuwa nasoma O-level katika shule fulani hv mkoani Iringa nilibahatika kusoma na binti fulani hv, ki ukweli alikuwa mzuri wa sura na tabia, nilitokea kuvutiwa naye na mara moja nilianza kumtongoza japo nilikuwa mdogo ki umri nlijaribu kadri ya uwezo wangu lakini sikufanikiwa hadi namaliza form four, baada ya hapo tulipotezana na kila mmoja akaenda alipokujua kwa ajili ya kuendelea na form five & six, tulipomaliza form six nilibahatika kukutana na mmoja wa mashoga zake hapa Dar na nikamuomba anipe namba ya simu ya huyo binti na kwa bahati nzuri nikapata ile namba na taratibu nikarudisha mazoea na katika stori za hapa na pale nikagundua kumbe advance alisoma Mwanza na alisoma darasa moja na binamu yangu na kikubwa zaidi walikuwa marafiki wakubwa, hiyo haikunipa tabu mi nikaendelea na pilika zangu na mwaka juzi mwezi wa tano tukawa wapenzi rasmi, wakati huo tunakuwa wapenz wote tulikuwa tunasoma (ndo tulikuwa tunajiandaa kufanya UE ya first year ya last semister) vyuo tofauti, mimi nilikuwa nasoma chuo fulani hv hapa Dar wakat mwenzang yeye alikuwa anasoma chuo fulan hivi huko Arusha, mapenzi yaliendelea na yanaendelea hadi sasa hivi lakini nina matatizo kadhaa katika mapenzi yetu haya ambayo yananiumiza kichwa na sijui chanzo ni mimi au ni yeye mwenzangu, na haya matatizo nisipoyapatia ufumbuzi wa kudumu naamini yatahatarisha mapenzi yetu, matatizo yenyewe ni kama yafuatayo:-
1) mapenzi yetu ni ya distance love, mimi kwa sasa naishi Dar na yeye anaishi Songea, wote ni magraduate & jobless hatujaonana tokea mwezi wa tano mwaka huu (before, boom lilikuwa likitusaidia nauli za kutembeleana) na kila mmoja kammiss mwenzie, sasa nifanyeje ili walau pamoja na umbali wote huu binafsi nijilinde nisimsaliti mwenzangu na yeye ajilinde asinisaliti mimi?!
2) pamoja na kuwa natambua umuhimu wa kusikilizana katika mapenzi binafsi huwa najihisi nina haki zaidi ya kusikilizwa na sijui ni kwanini labda ni kwa sababu mimi ni mwanaume, but huyu mpenzi wang anamisimamo yake ya ajabu ajabu, naweza kusema kitu akakataa kabisaa bila sababu ya msingi au naweza kumwambia kitu akaniambia HAPANA na ikawa HAPANA kweli hata nifanyeje siwez kumbadilisha, hii hali yake inanikera sana nahisi kama vile ana jeuri, dharau na kiburi
3) kwenye mapenzi kuna kukorofishana kwa hapa na pale, kuwa na migogoro ya hapa na pale nadhani ni jambo la kawaida, sisi tunapokuwa kwenye hali hii huyu mwenzangu huwa hata hajisumbui kuweka mambo sawa ikitokea mimi nikikausha, tunaweza kumaliza hata mwezi bila utatuzi wowote hii ni kwa kosa lolote hata yale ambayo yeye ni chanzo, mpenzi wangu ni mgumu mgumu wa kuomba msamaha jaman, kwake yeye neno "am sorry" ni mtihani mzito kweli.
Mwisho, Ki ukweli toka moyoni nampenda saana huyu mpenzi wangu na naamini pamoja na hayo mapungufu yake na yeye ananipenda kweli kweli, lakini pia naamini katika ndoa,mimi binafsi sitaweza kuishi na mwanamke mbishiiii, jeuri, mwenye kiburi na asiyeweza kuona kosa lake na kuomba msamaha, NATAMANI KUACHANA NA HUYU MPENZI WANGU, lakini nashindwa kuachana naye kwasababu kwanza naamini nitaumia saaana kwa sababu bado nampenda saaana, pili kwa kuwa huyu mpenzi wangu ni shoga mkubwa wa binamu yangu na namheshimu sana binamu yangu naogomba kuachana na shoga yake coz najua nitamuumiza sana huyu ndugu yangu, na tatu naona aibu kuachana naye coz kuna baadhi ya ndugu zake nafahamiana nao na huwa nawasiliana nao kwa sana tu sasa najiuliza kama nikiachana na ndugu yao sijui hawa ndugu zake nitawaambiaje kwa sababu mbali na kuwa shemeji zangu ni rafiki zangu wakubwa.
Wadau, naombeni ushauri wenu nifanye nini ili kama ni kuachana na huyu mpenzi wangu niachane naye bila kuwaathiri wasiohusikia na kama ni kuendelea naye nifanyeje ili niendelee naye bila kuumia na kusononeka moyoni?
SHUKRANI.