Japo udereva sio fani yangu, lakini ktk hali kama hiyo: Kuwaonyesha kuwa umegundua lina matatizo ya gia, na kuishia kuwaelimisha juu ya madhara ya kuendesha gari likiwa ktk hali hiyo pamoja na kuwashauri nini kifanyike (Kama una ziada ya ufundi - tengeneza kwanza badala ya kuendesha, vingnevyo omba aletwe fundi kwanza); yawezekana ndio kufaulu kipengele hicho cha usaili. Madhara yanaweza kuwa ni kuharibika zaidi kwa gari, ajali na kupoteza/kuathiri nguvukazi na mali, kufunguliwa mashtaka na/au kulipishwa kwa kuendesha gari likiwa ktk hali hiyo....... Hivyo, kama dereva usingeweza kuendesha gari kama hilo kwa kuchelea kumsababishia hasara muajiri wako.