Nina sh. 20,000 naomba mnishauri biashara ya kufanya

Jaribu kununua na kuuza vyakula(mboga mboga) wewe langua kutoka kwa wenye mabustani kisha tembeza , waweza kuitumia kwenye matunda vilevile.

Angalia na mazingira ya huko yana fursa gani, maana vijiji vingine unakuta krbu kila nyumba wana kibustani cha mboga.

pia, unaweza kukodi mkokoteni na kuufanyia kazi kwa malipo ya kila siku.

Mengine wataongezea wajuvi wa biashara!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba ushauri nini nifanye nina mtaji wa tsh.20000 nifanye biashara gani?

Kwa kipindi hiki cha mvua (kifuku) nipo Nachingwea kijiji cha Mbondo natumaini nitapata mawazo mazuri kutoka kwenu.
Kijana hongera kwa kuwa na mawazo ya uwekezaji badala ya kutapanya

Hicho kiasi kinaweza kukuzalishia kikubwa zaidi ukitulia na kukisimamia vyema.

Ushauri kwetu sisi utakuwa mgumu kwani fursa za uwekezaji zinatofautiana toka eneo moja hadi jingine. Mfano labda utueleze kijiji chenu kina fursa zipi na watu wanapendelea nini kama matumizi yao ya kila siku.

Kwa haraka nakushauri ufungue genge na uanze kufunga vitu vidogo vidogo kama sukar, chumvi, na kuuza viberiti, mafuta nk.

Angalia vitu vyenye mzunguko wa haraka na anza na hivyo kisha utakuwa unaongeza ma kupanua biashara kadri mtaji unavyokua na wewe mwenyewe kupata uzoefu na mahitaji ya watu wanaokuzunguka.

Epuka kukopesha na usithubutu.
 
hguy platnumz kukusaidia tu namna ya kujua mahitaji ya watu na yanayotoka haraka. Angalia tu hapo nyumbani kwenu ni kitu gani mnanua kila siku au kila baada ya siku 2 au 3. Ukitoka hapo jaribu kuongea na vijana wenzio kijijini familia zao wanapendelea kununua nini san sana kama mahitaji yao ya mara kwa mara.

Ukishajua hiyo, basi tambua hiyo ni fursa, changamkia kuwasogezea karibu mahitaji yao. Kitu kingine, ongea vizuri na utoe huduma bora kwa wateja wako. Tambua wateja ndio waajiri wako, bila hao bidhaa zako sio kitu zitakuozea. Toa huduma bora lakini EPUKA KUKOPESHA.

HATARI YA KUKOPESHA ukiwa na mtaji mdogo....
1. Itapunguza mzunguko wa pesa zako kwani itashikiliwa kwenye madeni
2. Mteja aliyekopa atakwepa kuja kununua kwako kwani anajua utakata pesa ya deni na atakosa kitu anachohitaji siku hiyo. Ni mpaka siku akipata pesa ya kukulipa ndio atarudi dukani kwako.

Kama umepata hiyo 20,000 na ukawa na wazo la kuizalisha hapo tayari umeshafanikiwa. Lililobaki ni utekelezaji kwa vitendo ndoto zako ambazo zinawezekana.
 
[emoji122][emoji122][emoji122] umeongea point sana mkuu.
 
Kijana hongera kwa kuwa na mawazo ya uwekezaji badala ya kutapanya

Hicho kiasi kinaweza kukuzalishia kikubwa zaidi ukitulia na kukisimamia vyema.

Ushauri kwetu sisi utakuwa mgumu kwani fursa za uwekezaji zinatofautiana toka eneo moja hadi jingine. Mfano labda utueleze kijiji chenu kina fursa zipi na watu wanapendelea nini kama matumizi yao ya kila siku.

Kwa haraka nakushauri ufungue genge na uanze kufunga vitu vidogo vidogo kama sukar, chumvi, na kuuza viberiti, mafuta nk.

Angalia vitu vyenye mzunguko wa haraka na anza na hivyo kisha utakuwa unaongeza ma kupanua biashara kadri mtaji unavyokua na wewe mwenyewe kupata uzoefu na mahitaji ya watu wanaokuzunguka.

Epuka kukopesha na usithubutu.
pamoja mkuu
 
Back
Top Bottom