Nina mwaka wa 4 tangu nipige stop TV nyumbani kwangu

Kuna raha yake umetulia na madogo unaweka animation movies eg Moana, Zootopia na nyinginezo mnacheka hapo na madogo weeeeeh, kwangu mimi hii ni ratiba yangu jumamosi na jumapili ni mwendo wa animation movies na madogo yangu.
 
Hao watakuja kuwa watoto wa ajabu sana... Hutambui nje ya elimu ya darasani kuna elimu dunia..??
 
Kaka kwanza pole sana, katika dunia iliyojaa uchafu mwingi tumia njia aliyotumia Mungu kutuacha watoto wake wapendwa hapa duniani huku akitufundisha mema na mabaya na kutup nguvu ya kushinda uovu, wala hakututenga tusione technolojia maana pia ni msaada ikitumika vyema. Una nia njema sana lakini Mungu akusaidie usiendelee kutengeneza bomu hilo. Watafutie watoto ukombozi wa kweli wa roho zao ndipo hekima ya rohoni itatawala akili zao, usianze kinyume maana akili haina nguvu juu ya roho iliyopotea (corrupted spirit).
 
Kuangalia Tv ni Mambo ya kijinga na kipuuzi hasa kuangalia ligi ya Mpira wa Tz
Yaani uelewa ni kuto angalia, bila kujali unaangalia program gani?
Hata kuangalia Doccumenttary, mfano: National Geographic,
National Geographic Wild
History
Discovery Science
ID
Real Time
Travelxp
Foodies
Rai Italia
Tanzania safari channel.

Habari:
BBC World News
Al Jazeera English
Fox News
MSNBC
France 24 English
CNN na zingine.

Yaani hizi ukiondoa za michezo na burudani, huguswi na hata moja, ulafu bado unaona Watu wajinga ispokua wewe, unachekesha.
 
Nyumbani kwangu nimepigaga marufuku kitu inaitwa kutazama TV. Habari naangalia kupitia simu, watoto kila mtu ana tablet yake, huko ni video za masomo nimejaza na wakichoka kuna vitabu pia watasoma na watakuja kunifafanulia walicho jifunza.

Mpira naangaliaga kupitia mtaani ila EPL pekee, ligi ya bongo hapana.

Huwa nashangaa watu wanapo lalamika bei ya kisimbuzi imepanda, yaani mimi nilishaacha kuwachangia, hio pesa bora niweke data ninunue video za mafunzo online. Watoto nimewanunulia DVD zenye masomo mbalimbali na kila wiki nawaongezea hivyo hawana time na TV. Pia Watoto ndio sababu ya mimi kuacha kuangalia TV maana sikutaka wawe watumwa wa TV.

Kwa sasa walishazoea, ila ninacho jitahidi ni kuwatafutia video nyingi zenye mafunzo kwao, hapa nimewekeza sana.

Nilikuja kugundua TV asilimia kubwa zinaharibu watoto, haijalishi ni cartoon au nini. Watoto wanashindwa kuwa wadadisi, hawawezi kuwa creative, watoto wanashinda kutazama cartoon hakuna kitu wanajifunza pale, watoto kutwa nzima ilikuwa ni kutazama tamthilia za kiphilipino na za kihindi na za zile za kibongo ambazo nyingi sana zinaonyesha mambo ya mapenzi mapenzi tu.

Kuna watu wanadhani cartoon zinafundisha watoto, ukweli na hapana. Nikuukuulize kwenye Tom & Jerry kuna kipi mtoto anatoka nacho pale? Cartoon ni biashara tu, na zinaharibu watoto kama ulikuwa hujui. Zinafanya watoto wawe wajinga tu, kutwa nzima kusimuliana cartoon, unategea nini kama watoto wanashinda kusimuliana cartoon?

Nunua vitabu wasome, na sio tu wasome na pia waelezee walichosoma, weka DVD za mafunzo, TV watakuja kutazama wakiwa levo nyingine huko.
Nakuunga mkono sanaa

TV ndo zimesababisha watoto wengi kua magasho haswa huko boarding School watoto wakirudi likizo full kujiachia kutazama michezo isiyofaa hlf nowdayz michezo mingi inaashiria mambo ya ugasho

Since 2013 mzee alitukataza kutazama tv bcz tulikua tukirudi likizo hatusomi basi mimi mpk leo sina haja na tv kabisaaa yni mimi na simu na vitabu vyangu ila itafika hatua tv nitakua sitaki kuiona kabisaaa mana madhara yake ni mengi kuliko faida zake
 
Mm watoto wangu ruksa kuangalia hadi pilau.
Imagine mm mwenyewe naangalia pilau hapo kwenye desktop yangu ofisini.(kwenye Avatar yangu)
Kwangu ni uzwazwa kuwanyima watoto kuangalia Tv.
 
usiwanyime uhuru sana maana siku wakiupata watautumia vibaya
 
Nyumbani kwangu nimepigaga marufuku kitu inaitwa kutazama TV. Habari naangalia kupitia simu, watoto kila mtu ana tablet yake, huko ni video za masomo nimejaza na wakichoka kuna vitabu pia watasoma na watakuja kunifafanulia walicho jifunza.

Mpira naangaliaga kupitia mtaani ila EPL pekee, ligi ya bongo hapana.

Huwa nashangaa watu wanapo lalamika bei ya kisimbuzi imepanda, yaani mimi nilishaacha kuwachangia, hio pesa bora niweke data ninunue video za mafunzo online. Watoto nimewanunulia DVD zenye masomo mbalimbali na kila wiki nawaongezea hivyo hawana time na TV. Pia Watoto ndio sababu ya mimi kuacha kuangalia TV maana sikutaka wawe watumwa wa TV.

Kwa sasa walishazoea, ila ninacho jitahidi ni kuwatafutia video nyingi zenye mafunzo kwao, hapa nimewekeza sana.

Nilikuja kugundua TV asilimia kubwa zinaharibu watoto, haijalishi ni cartoon au nini. Watoto wanashindwa kuwa wadadisi, hawawezi kuwa creative, watoto wanashinda kutazama cartoon hakuna kitu wanajifunza pale, watoto kutwa nzima ilikuwa ni kutazama tamthilia za kiphilipino na za kihindi na za zile za kibongo ambazo nyingi sana zinaonyesha mambo ya mapenzi mapenzi tu.

Kuna watu wanadhani cartoon zinafundisha watoto, ukweli na hapana. Nikuukuulize kwenye Tom & Jerry kuna kipi mtoto anatoka nacho pale? Cartoon ni biashara tu, na zinaharibu watoto kama ulikuwa hujui. Zinafanya watoto wawe wajinga tu, kutwa nzima kusimuliana cartoon, unategea nini kama watoto wanashinda kusimuliana cartoon?

Nunua vitabu wasome, na sio tu wasome na pia waelezee walichosoma, weka DVD za mafunzo, TV watakuja kutazama wakiwa levo nyingine huko.
Wewe kama sio Msabato, njoo uniue. Nimekaa pale chini ya mwembe nacheza draft!
 
Yaani nimeona ajabu sana uliposema tom and jerry hazifundishi bali zinatia ujinga. tom and jerry ndio moja ya katuni bora na salama anazopaswa kuangalia mtoto kwani nia sio kufundisha bali ni kumburudisha, kumfurahisha na kumchekesha mtoto na akili yake inakuwa inatulia. kuna muda wa masomo na muda wa kuburudika na kufurahia maisha na utoto wao.

Mimi kwa muda ambao nimetumia kuangalia tom and jerry basi ningekuwa chizi na mjinga kupitiliza sasa hivi lakini hapana. tena mungu akinijaalia watoto basi nitatengeneza na theater ndogo nyumbani yenye screen kubwa ya nchi 62 ili tu kuangalia tom and jerry na watoto wangu. mateso na limit za ajabu ajabu kwa wanangu sitaki kusikia kabisa mwisho watashindwa kujitegemea sababu unawafungia na kama ni vidume watakuwa madomo zege na kuogopa watoto wa kike pia kuwa waoga wa changamoto na maisha.

Na kingine ni kwamba tablet ni hatari sana kwa watoto sababu ina access na Internet, na kama unavyojua Internet imejaa mambo machafu yote unayoyajua. na kuna uwezekano mkubwa watoto wako wanajua kutumia hiyo tablet kuliko wewe means kuna mambo watakuwa wanaangalia na wewe hutoona chochote wala kujua.
Ila kwa TV ni simple zaidi kuweka restriction na kujua wanachoangalia watoto kuliko tablet.

Na unachosahau ni kwamba kama kuhusu kujifunza tabia mbaya basi watoto watajifunza tabia mbaya tu kutoka kwenye jamii hasa kama huwafundishi kuhusu maadili mema na kuchuja jema na baya.
Huko wanakocheza wanakutana na watoto wengine ambao wana tabia tofauti na bila shaka wanaangalia tv hivyo watajifunza tu hayo mabovu bila tv. na considering jamii yote imeoza na kuharibika sasa hivi means labda wanao uwafungine ndani milele ndio hawatoathirika. Na kama alivyosema mdau kule juu kwamba umewaondolea addiction ya Tv na umewapa addiction ya tablet. way worse.
Point ni ulichokifanya sio solution bali ni kama kutia sukari baharini na utegemee chumvi ipotee, hilo haliwezekani wala halipo.

Kuna mambo ya kuwabana watoto na mengine yanahitaji uangalizi wa karibu na mafundisho tu.
Duniani tunaishi mara moja, vitu vingine ni kuwatesa watoto na kuwafanya wawe wapweke na maroboti kama unawaandaa na vita au unafuga ng'ombe.
 
Mkuu kuna aina nyingi sana za Video za mafunzo, zipo za mambo ya Arts, zipo za masomo ya darasani, zipo za watoto wakijufunza kupika na kazi zingine za kijamii na by the way huwa hawatazami tu kuna mitihani nawapa, mfano zile za Arts kuna mazoezi kwa vitendo, na kuna baadhi ya vitu kwa sasa wanaweza tengeneza kama mapambo basdhi, na vitu vingine vingine.
Naiga kwako
 
Back
Top Bottom