Nina milioni 45, nifanye biashara ipi kati ya hizi?

Bank ipi iko vizuri,niliyokuwa nayo ni nzuri kosa nililofanya ni kununua daladala za kufufua sababu pesa ilikuwepo nimejikuta imeishia garage japo zimesimama lkn pasua kichwa zinakula Pesa kama jini mfilisi unarekebisha hiki kinaibuka hiki naona tafilisika japo wazoefu wanakwambia ndio gari zilivo vumilia zitatulia zikishajivubua magonjwa yote hata sisi tulianza hivo hivo.Unagusa services ya pump ukicheki imeliwa laki nani hapo nikipiga sawa na mifuko ya cement kadhaa,Mara gari imekamatwa,najikuta natoa tu
Kweli kabisa! Sina hamu na gari mi! Nimepaki coastal mayai! Nataka mteja tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hauko serious ndugu, eka mia5 kwa mtaji wa 45m?!! Mara ujenge frem ufungue hardware kwahiyohiyo 45m? Yaani ununue kiwanja, ujenge frem (na godown/stoo) then bado ubaki na mtaji wa hardware?!!

Biashara ndugu zinaendana na uzoefu, interest, na kiwango chako cha subira. Nahisi unapenda sana biashara ya magari, kama vipi fanya research upande huo uwekeze huko, huenda nafsi yako itakuwa na amani. Humu kila mtu ataponda kitu hata asichowahi kukifanya au alichokifanya akafeli, kisa tu alifeli yeye au nduguye basi ashaiona haifai, anashindwa kujua kwamba haimfai yeye inamfaa mwingine.

Biashara ya kilimo kwa wanaoijua wanapata pesa na kila mwaka utawaona wanajenga magodown ya kuhifadhi mazao yao. Salum Sumri alikuwa na fleet kubwa mno ya mabasi lakini ameona nibiashara kichaa ameamua kwenda kulima, kama hili halikufikirishi basi hakuna kitachokufikirisha.

Mtihani mgumu kabisa ulionao nduguyangu ni KUANZISHA BIASHARA, hapo ndiyo pesa hufa, na usipokuwa makini kweli hiyo pesa itakufa. Angalia sana ushauri wa humu ndani, wengi humu ni waajiriwa wasio na uzoefu wowote na biashara zaidi ya uzoefu wa kwenye keyboard na failed attempt zao katika biashara waliweka watu wengine wasimamie sababu wanabanwa na kazi. Wengine ni wanafunzi tu ambao hata kuuza karanga hawajawahi.

Kama hiyo pesa unategemea mkopo nakushauri usichukue kwanza, anza na yakwako ikuze taratibu.
Kwa trekta kujilimia plus kuwalimia wengine nazungumzia kulima si chini ya ekari 500 hadi 1000 kwa msimu mazao yenye low risk mfano kunde,alizeti,mtama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma tena ulichoandika, 20 anunue eneo, 25 ajenge, pesa yake imeshaisha tayar anafunguaje hizo biashara 3!!!
Vipi hii idea Katika 45 toa 20 nunua site 25 jenga frem 10 zipangishe 7 kisha 3 zifungue business moja ya hardware,pili spea za pikipiki tatu duka la nafaka baada ya miezi 3 kalikopee bank hilo eneo 40m mpe muhindi akupe tata mpya ya mkataba tafuta ruti dume za nje ya mji zinazolaza 250000 kwa siku upate kulipa bank na kwa muhindi yaaani uchukue risk kubwa (unabet maisha) hasara roho potelea mbali.Hapo vipi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hauko serious ndugu, eka mia5 kwa mtaji wa 45m?!! Mara ujenge frem ufungue hardware kwahiyohiyo 45m? Yaani ununue kiwanja, ujenge frem (na godown/stoo) then bado ubaki na mtaji wa hardware?!!

Biashara ndugu zinaendana na uzoefu, interest, na kiwango chako cha subira. Nahisi unapenda sana biashara ya magari, kama vipi fanya research upande huo uwekeze huko, huenda nafsi yako itakuwa na amani. Humu kila mtu ataponda kitu hata asichowahi kukifanya au alichokifanya akafeli, kisa tu alifeli yeye au nduguye basi ashaiona haifai, anashindwa kujua kwamba haimfai yeye inamfaa mwingine.

Biashara ya kilimo kwa wanaoijua wanapata pesa na kila mwaka utawaona wanajenga magodown ya kuhifadhi mazao yao. Salum Sumri alikuwa na fleet kubwa mno ya mabasi lakini ameona nibiashara kichaa ameamua kwenda kulima, kama hili halikufikirishi basi hakuna kitachokufikirisha.

Mtihani mgumu kabisa ulionao nduguyangu ni KUANZISHA BIASHARA, hapo ndiyo pesa hufa, na usipokuwa makini kweli hiyo pesa itakufa. Angalia sana ushauri wa humu ndani, wengi humu ni waajiriwa wasio na uzoefu wowote na biashara zaidi ya uzoefu wa kwenye keyboard na failed attempt zao katika biashara waliweka watu wengine wasimamie sababu wanabanwa na kazi. Wengine ni wanafunzi tu ambao hata kuuza karanga hawajawahi.

Kama hiyo pesa unategemea mkopo nakushauri usichukue kwanza, anza na yakwako ikuze taratibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ardhi tz sio lzm ununue unaanza kwa kuingia ubia mtu anatoa ardhi yake mimi nalima kikipatikana tunagawana na sio kununua ardhi.Wengi wanamapori wanatafuta wa kuyalima hata bure.Pana jamaa ana eka elf 3 zimekaa tu kusini vipi ukizilima zote mazao uhakika mfano karanga,kunde,choroko,dengu,mtama,alizeti,kisha unaexport?
 
Nimekuelewa sana mkuu! Point yangu ni hii . nimekupangisha ww unanipa 1.8m kwa 6mths!...ni bora nifungue kiwanda nisage unga hyo 1.8 naweza ipata kwa tons chache sana za mahindi tena mapema tu!
Haijalishi nampngisha boss gan lakini thaman ya pesa ndo naiona hairidhishi!..
ushaambiwa real estate ni kwa ajili ya backup mambo yakigoma huko kwenye ma tani ya unga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chukua tractor mkuu haswa brand za New Holland au Case za 4WD ukajichimbie moro turiani uko hukosi 17-19m kwa msimu ambao ni kama miezi mi5 ila iwe mpya sio used na wewe utalima mashamba yako pia kuongezea kwenye hela ya trekta...
hizo assemble wapi.Nilipendelea johndeer hp75 kwa idea ya good tractor tupeane uzoefu
 
Mawazo maziri wadau, ushapewa mawazo mengi mazuri ni issue kufanya implementation tu na commitment, yangu hayajaongelewa na mtu na ni juu ya ulinzi wa unachotaka kukifanya ifuatavyo:

Sifaham imani yako ie Muslim, Christian au vinginevyo, najua una imani (Spiritual faith)

Physical world inatawaliwa kwa kias kikubwa na Spiritual world, hapo unachopanga, ulimwengu wa kiroho unaangalia, mwingine unataka ukusaidie (Mungu wa kweli) lkn mwingine unataka ukuangamize (mungu mwingine)

Unaweza kupata mafanikio na ulinzi kupitia aina mbili nilizozitaja hapo juu za mazingira ya kiroho, faham kwamba ktk kila hali yyte ya kiuchumi kuna nguvu ya kiroho nyuma yake inayokusukuma ie kufanikiwa au kufeli kote huletwa na hali ya kiroho.

Usijeanzisha biashara yyte ile popote pale iwapo una uhakika kwamba huna ulinzi wowote spiritually (Iwe ni wa MUNGU wa kweli au wa mungu shetani) na ndo mana unaweza kuniambia ulianzisha biashara ya magar ikafeli, uliingia kweny ushindani, na wengi wana ulinzi wao, kaa ukijua ukiingia bila ulinzi lazima utafeli tu.

Nakusihi kabla hujaanza biashara yyte jiwekee ulinzi kwanza, vinginevyo unaweza kufa kabisa watu wakakuondoa dunian ili tu usiwe mshindani wao.

Usipojiwekea ulinzi utakufa na pressure tu, Mungu wa kweli na akusaidie kuelewa.
 
Uoga
Bana likasi, Hiyo pesa 45m ukiweka benki ya biashara kama fixed deposite kila mwezi unapewa 480,000 riba wakati unasubiria paka pale mazingira ya biashara ikae vizuri nchini, lasivyo uwezekano wa kupoteza mtaji ukiwa unaanza biashara mpya nimkubwa sana kipindi hiki cha JPM, labda kama unaendeleza biashara ulio kua nao....lakini jambo muhimu kipindi hiki sio faida ila ni kulinda mtaji wako

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namba 1 hutojuta,frem ndio mpango.
Wasalamu,kwa kuuza daladala zangu mbili sababu ya usumbufu wa kissing garage,plus mkopo nawezapata kama m45 nipo na mawazo kama matano hivi,ushauri muhimu ili nisiangamie maana pesa ikishapotea hairudi unabaki na majuto na maradhi ya moyo tu.

1. Nitafute eneo nijenge frem za kupangisha hapa takula hadi uzeeni shida utapata kodi itakayokusaidia kula na sio kukua haraka kibiashara lkn ni ya uhakika yaani ufi njaa.Mungu akijalia wawezazifungulia biashara zako kadri utakavyo na maisha yakaenda.

2. Ninunue trekta mpya zero kilometer katu sitonunua chombo cha moto used nchini tena kwa hasara nilizopata za kushinda garage kuliko kushinda barabarani.Trekta ni tegemeo ni johndeer,Massey,case,deutz ukitanguliza 45 anakupa inayobaki na riba ndani ya mwaka kwa mnyama deer miaka miwili yaani,zinauzwa kati ya 55m hadi 65m plus jembe.Niingie pori nikachane mbuga nalimia watu nami nalima yangu mazao tegemeo ni karanga,alizeti,mtama,mhogo,viazi,mahindi,mpunga nategemea kulima ekari 500 kwenda juu mashine Yangu nguvu yangu nasimamia mwenyewe iwe jua au mvua ni kula mbuga tu.

3. Nimpe muhindi 45m anipe tata marcopolo ya mkopo zero kilometa nikae mlangoni nipige ndefu sio daladala yaani ruti za nje ya mji nauli isiyo chini ya elf 15 yaani kupakia kwa foleni mfano moro ifakara,mbagala kusini,kambi popote.

4. Niagize fuso mnyama au scania kipisi nikae mwenyewe naenda shamba kununua mizigo mixer mfano viazi chips,ndizi,miwa,nyanya,vitunguu,ngombe,mbuzi,nk chochote kiuzwacho sokoni nakujauza bei ya jumla narudi shamba tena kwa kusomba mizigo ya duka kurudi shamba.

5. Nifungue kiwanda cha kusaga chupa na mifuko ya plastic kisha nauza viwandani.

6. Ninunue shamba nipande miti niendelee na umasikini wangu nisubirie miaka 10 hadi 15 niwe milionea baada ya kuvuna miti.

Naombeni idea kwa kuangalia risk,faida,mda,usalama wa fedha,uhakika wa kuishi, stress,nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom