mbu wa dengue
JF-Expert Member
- Jun 2, 2014
- 7,655
- 9,758
Hapa ushauri namba 3 ndio wenye uhakika.Mkuu umetoa hoja nzuri mimi nakushauri kwa alternative zifuatazo za uwekezaji tumia moja au zaidi ya moja
1. Unaweza tenga million kumi kwa ajili ya biashara lakini milioni thelasini na tano kaweke kwenye treasury bond yaani dhamana za serikari, fuatilia rate BOT utaamua uweke za muda gani miaka mitano,au kumi,au kumi na tano au ishirini, ingawa mimi napendekeza za miaka ishirini. Itakufanya uwe na kipato cha uhakika wakati unatumia milioni kumi kufanya biashara nyingine ambayo ni scalable.
2.Tafuta mfanyabiashara anayenua au kuprocess mazao ya biashara, muombe awe menthor wako au mshirikiane, hapa usihofu wapo wengi Songea au Ifakakara wana mashine na godown , tumia millioni 30 nunua mazoa mwezi wa saba au wa nane hifadhi kwenye magodown yao kwa kawaida atakayenunua atasaga au kukoboa kwao uza kuanzia November.
Usitumie 15 M iloyobaki, mwakani (2021) baada ya kujifunza tafuta washirika wawili ata mimi naweza kukutafutia wachangie kiasi kama hicho unaweza nunua na kuistall mashine za kukoboa mpunga Ifakara au kusaga unga Songea inategemea utakapopenda ku specializa, I prefer Songea. Then utakuwa unaprocess na kusafirisha kwenye masoko. Pia ukivutiwa na wazo hili awali unaweza kuamua kutembelea maeneo yenye bishara za vyakula kama Moro,Ifakara,Songea na baadhi ya wilaya za Mbeya ukaone watu wanavyofanya wakati sisi tunashinda jamiiforums. Usione tabu kutumia pesa kwa kusafiri ili upate business information na kupata technical know
3. Fanya survey ya mikoa na maeneo ambayo eneo la kiwanja cha millioni kumi au kumi na mbili unaweza jenga apartment ya vyumba viwili na sitting na choo na jiko unaweza pangisha kwa laki mbili au zaidi.
Ukipata eneo jenga apartment tatu au mbili with site plan inayoruhusu expansion kwenye kiwanja kimoja. Hapa for cost efficient apartment mbili itokane na design ya nyumba moja yaani huyu mbele mwengine nyuma, zinashare baadhi ya vitu kama ukuta ma mabomba ya majo.
Idea hii ni ngumu kwa dar kwa kuwa viwanja vya million kumi ni pembeni saana ila miki kama Moshi, Tanga,Mtwara,Lindi,Mbeya,Shinyanga,Tabora,n.k unaweza fanikiwa.
All the best
Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo zingine ni pata potea,ingawa hiyo namba 1 pia ni nzuri ila inawafaa watu wenye sources nyingi za income ili awe na uwezo wa kuvumilia hiyo miaka mingi.
Sent using Jamii Forums mobile app