Hapana sijakosea unajua sisi mkopo kupata kwa kipindi iki kidogo ilikuwa ngumu kwahiyo ukipata nafasi ya kuchukua ilikuwa bora maana kila mtu alikuwa anawaza lake kutokana na janga la CovidUnunue bajaj 2 au boda boda 5 alafu hela inayobaki je?
Ulikosea mkuu kuchikua mkopo huku huna cha kufanyia.
Tatizo ninapoishi nina eneo dogo sana kwahiyo naona kama ntaingia Gharama kubwa kununua eneo lingine ndugu .na pia swala la kujenga nyumba ni ngumu maana sina eneo ntakuta naishia katikati na hela ya kumalizia itanishinda hivyo itabidi nisubilie baada ya miaka mitano nimalize mkopo ndo nikope tena kumalizia nyumbaFuga kuku
WA nyama
Na kuku wa kienyeji..
Ila unaweza Jenga nyumba na ukauza ni sure bussines kipindi hujaiuza unapangisha
Utakuwa umenisaidia sana ndugu maana naona Giza mbele yangu mpka nawaza nimchukue kijana kijijin nimpeleke NIT fasta apige kozi ya miezi 4 nimuingize barabarani apambane maana madereva wa DSM kidogo wanahitaji mtu ambae ni mzoefu kwenye biashara maana sisi tunaotaka kuanza inakuwa changamoto kwelikweliNtakutumia link za dala dala uchague moja!
Bajaj, utalia, boda boda, utaomboleza...Kuku, sikushauri.. Ndugu yangu wa karibu anafuga.. Inabidi uwe na uzoefu kabla hujazamisha pesa ndefu.
Dala dala ikija, katia bima kubwa.
Used 1998 NISSAN CIVILIAN BUS/KC-RYW40 for Sale BH241062 - BE FORWARD
Milioni 45 ushindwe kujenga na kumaliza?Tatizo ninapoishi nina eneo dogo sana kwahiyo naona kama ntaingia Gharama kubwa kununua eneo lingine ndugu .na pia swala la kujenga nyumba ni ngumu maana sina eneo ntakuta naishia katikati na hela ya kumalizia itanishinda hivyo itabidi nisubilie baada ya miaka mitano nimalize mkopo ndo nikope tena kumalizia nyumba
Ndugu sisi watumishi wa serikali maisha yetu asilimia kubwa tunategemea Mikopo maana ukisema ujichange uje kupata 45 mil karibia miaka kumi na marejesho yetu sio cash in hands Bali wanakata moja kwa moja kwenye payslip kwahiyo ni swala la kawaida na ndo maisha yetu nduguSio uchawi, lakini naona ukienda kuanguka.
Mmechukua mkopo bila kuwa na plan.
Halafu ni risk sana kuanzisha biashara kwa kuutegemea mkopo 100β
Mna uzoefu na biashara gani?
Kwa usalama wa hiyo pesa kama una kiwanja ni heri ujengee nyumba upangishe.
Neno langu si sheria. Zaidi labda wataalamu waje
Ukitaka dala dala ikulize, upate gari mbovu au nzee, uwe na bima ndogo, upate ruti mbaya au dereva mbaya.. Uwe mvivu kutengeneza gari au uwe unakomaa sana kuwa lazima kipande litimie.Usijichanganye hata kidogo kununua daladala....utalia.
Ukinunua daladala basi we uwe konda mpk pale utakapoona pesa yako atleast imerudi.
Zingatia nnayokwambia, yalishanikuta.
Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app