Nina miaka 45, nimependwa na mwanaume wa 38

Daisy Llilies

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
1,017
2,154
Nimeiangalia habari ya Kajala na Harmonise ninaona ni haya maisha yangu kabisa. Mwaka 2014 nilikutana na kaka mmoja kutoka Ghana, ni mweusi ule weusi unaon’gaa, mrefu 6”2 amepanda. Kijana huyu tulielewana tunaweza kuongea mpaka asubuhi.

Kabila ni Mghana, alisoma Marekani na Uingereza. Ni investment banker. Pesa kwake siyo tatizo kabisa. Tulifahamu tofauti za umri kati yetu, tulikuwa marafiki. Kutokana na nature ya kazi yake anasafiri sana. Zaidi ya familia yake hana marafiki wengi. Mara nyingi tulifanya picnic pamoja wakati wa kiangazi, kwenda kula dinner na vitu vingine.

Alinipeleka kwao likizo, amejenga nyumba ya vyumba vinne vya kulala. Huwa anaifunga akiondoka na binamu yake anaishi kwenye guest wing na familia yake, ndiyo kama walinzi.

Huyu mwanaume anasema amenielewa sana anataka kumuona. Miaka yangu ni 45 na mtoto wa dada yangu mkubwa ana miaka 36 nikifikiria kumletea uncle ana 38.

Sijawahi kufanya nae mapenzi, kuna wakati alihamisha £ 8,000 kwenye account yangu zinisaidie akiwa safarini. Kipindi hicho nilikua ninaongeza ujuzi.

Sina mume wala sijawahi kuolewa.
 
Scammers otherwise muwe mnafanya kazi wote bongo, kuhusu umri hakuna tatizo apo labda wewe uwe na kibase na kujifanya uko na experience,ila mkiishi kama maagizo ya vitabu vya dini na mwanamke amuheshimu mwanaume, mwanamke aheshimu ndoa yake,hapo mtakuwa poa hakuna atakaye ona gape la umri.
 
Back
Top Bottom