Nina Masters nataka kufanya PHD

Nina Masters nataka kufanya PHD

Kidogo ulitaka kumkaribia Bashite.

KUSOMA SANA NI UOGA WA MAISHA.
hii kauli wengi sana wananiambia, lakini mimi huwa siipendi haina uhalisia. Mimi nimetumia jina la mtu mwingine ambaye alikuwa mtoro shuleni, sidhani kama ni kosa kisheria.
 
Mabashite kumbe mpo wengi!
Elimu ina changamoto zake ndugu yangu. si bora mimi nakesha nasoma ili nipite, je wale wanaonunua mitihani na madesa huko kwenye mavyuo? hao nao wapo kundi gani? tena hao ndiyo wengi.
 
Kiukweli pesa sina, maisha yangu ni ya upweke sababu muda mwingi natumia kusoma, maana akili yangu nayo haishiki kwa urahisi, yaani ni kwa mbinde mno siyo kama wengine anasoma kidogo tu kamaliza, mimi ni kukesha na vitabu.

ahaaa eti kwa mbinde mno. Pole

nimegundua wewe una akili ya kawaida. Na unatumia nguvu nyingi kusoma. Phd sio mchezo na vile umesema hauko vizuri kujielezea mmmh utapata ugumu.

Nina mtu wangu wa karibu anaosoma phd yuko nondo tangu primary hadi hapo alipo ni kichwa kweli kiasi kwamba akipiga hata serengeti 5 tu anashusha material si mchezo, vitabu anavyosoma ni kuanzia kg 10+ wewe utaweza?

Kwann usifanye kazi au kutafuta mtaji ufanye biashara?
 
Uko OK. Ila PhD inatakiwa uwe vizuri kichwani. Hujatumia cheti cha mtu.
 
Nakupongeza kwajitihada ulizonazo katika kutafuta elimu. nakushauri hata PhD soma. utapata na utaweza hata ukiisoma miaka nane ni kawaida tu
 
Uko OK. Ila PhD inatakiwa uwe vizuri kichwani. Hujatumia cheti cha mtu.
cheti cha mtu hapana, tatizo langu ni kichwa siyo kizuri - yaani ni usongo usiku na mchana kusoma!! hii ndiyo changamoto ambayo nimekuwa nayo toka nikiwa secondari - ni kukesha kukesha na mimi
 
Nilimaliza Darasa la saba, nikafeli - nikarudia shule nyingine nikapita.

Nikaenda Secondary, form four nikapata div IV ya point 26 nikachaguliwa chuo cha ualimu wa primary- nikagoma kwenda. nikaja DSM kwa mjomba wangu kutafuta maisha.

Nikajiunga na Certificate ya Materials Management mwaka mmoja (chuo nakiweka kapuni) - nikamaliza vizuri, Matokeo yakafaa kujiunga na Diploma.

Nikaomba admission ya Diploma Miaka 2 chuo kingine tofauti sababu nilitaka kusomea uongozi wa biashara (Business Administration), nikamaliza na pass.

Nikatafuta kazi lakini sikubahatika kupata kwa urahisi, nikaona bora niendelee kusoma tena, nikaomba chuo hicho hicho kufanya Bsc in Business Administration miaka 3, nikamaliza na GPA ya kawaida baada ya supplementary 2 nikachomoka na gentleman pass kama wanavyoiita.

Nikatafuta kazi sikupata, ila nikafanya kazi ya muda ya kufundisha secondary miezi 6 nikaona mizinguo tu, nikaona nirudi shule tena, nikaenda chuo kingine (Jina Kapuni) nikaomba nifanye Masters in Public Administration, sikupata sababu kwanza pass zangu hazikuwa za juu kwenye Degree yangu na pili Masters nayoomba ni tofauti na Degree yangu.

Nikaona isiwe shida, nikaomba Postgraduate Diploma ya Public Administration Mwaka mmoja, nikamaliza - nilivyomaliza tu nikaunga Masters in Public Administration - nikamaliza baada ya kukamatwa kamatwa mara kibao.

Sasa nataka kufanya PHD, ila kuna muda huwa najishtukia kuhusu elimu yangu, ndiyo maana nimeona niweke hapa ili mnieleze kama ipo Genuine na mimi naweza kujiita msomi wa nchi hii yaani Mwanazuoni?
Consult Prof Bashite
 
Yaani mkuu mpaka una masters lakini kujiamini kunakosekana? Basi hiyo elimu haitakusaidia bora ujikalie tu home ujigegedee mama yoyo basi! Huko unakoenda ni aibu tupu! Ona akina Mwakyembe na ma-PhD yao wanavyojivua nguo, hapa Tanzania hakuna mwenye PhD aliyeonekana kuwa na busara bora uishie masters uanze kusaka maisha.

Unawajua wote wenye Phd? Tafakari kabla ya kusema/kuandika. Pole sana.
 
komaa na kitabu mbaba ila tambua umri unaenda..
 
Nilimaliza Darasa la saba, nikafeli - nikarudia shule nyingine nikapita.

Nikaenda Secondary, form four nikapata div IV ya point 26 nikachaguliwa chuo cha ualimu wa primary- nikagoma kwenda. nikaja DSM kwa mjomba wangu kutafuta maisha.

Nikajiunga na Certificate ya Materials Management mwaka mmoja (chuo nakiweka kapuni) - nikamaliza vizuri, Matokeo yakafaa kujiunga na Diploma.

Nikaomba admission ya Diploma Miaka 2 chuo kingine tofauti sababu nilitaka kusomea uongozi wa biashara (Business Administration), ni kamalizia na pass.

Nikatafuta kazi lakini sikubahatika kupata kwa urahisi, nikaona bora niendelee kusoma tena, nikaomba chuo hicho hicho kufanya Bsc in Business Administration miaka 3, nikamaliza na GPA ya kawaida baada ya supplementary 2 nikachomoka na gentleman pass kama wanavyoiita.

Nikatafuta kazi sikupata, ila nikafanya kazi ya muda ya kufundisha secondary miezi 6 nikaona mizinguo tu, nikaona nirudi shule tena, nikaenda chuo kingine (Jina Kapuni) nikaomba nifanye Masters in Public Administration, sikupata sababu kwanza pass zangu hazikuwa za juu kwenye Degree yangu na pili Masters nayoomba ni tofauti na Degree yangu.

Nikaona isiwe shida, nikaomba Postgraduate Diploma ya Public Administration Mwaka mmoja, nikamaliza - nilivyomaliza tu nikaunga Masters in Public Administration - nikamaliza baada ya kukamatwa kamatwa mara kibao.

Sasa nataka kufanya PHD, ila kuna muda huwa najishtukia kuhusu elimu yangu, ndiyo maana nimeona niweke hapa ili mnieleze kama ipo Genuine na mimi naweza kujiita msomi wa nchi hii yaani Mwanazuoni?
Kwa chuo makini ukichukua hizo sehemu nilizoweka nyekundu hawatakupa admission, hata barua ya referee inaweza ikawa ngumu (Labda Open University yetu ingekuwa inafuata nadharia ya Open education, lakini Ndalichako na Uncle Magu hawataki hili). Ni vizuri ukajithamini unataka PhD ili iweje, na hata kama utapata "chuo" kikakupa admission msuli wake utauweza au utapoteza muda tu. Sikushauri. Pili nafikiri masters peke yake haikufanyi uwe mwanazuoni ingawa wanaweza kukuita msomi-lakini kwa jinsi ulivyo unga unga inaleta shaka.
 
Back
Top Bottom