Nilimaliza Darasa la saba, nikafeli - nikarudia shule nyingine nikapita.
Nikaenda Secondary, form four nikapata div IV ya point 26 nikachaguliwa chuo cha ualimu wa primary- nikagoma kwenda. nikaja DSM kwa mjomba wangu kutafuta maisha.
Nikajiunga na Certificate ya Materials Management mwaka mmoja (chuo nakiweka kapuni) - nikamaliza vizuri, Matokeo yakafaa kujiunga na Diploma.
Nikaomba admission ya Diploma Miaka 2 chuo kingine tofauti sababu nilitaka kusomea uongozi wa biashara (Business Administration), nikamaliza na pass.
Nikatafuta kazi lakini sikubahatika kupata kwa urahisi, nikaona bora niendelee kusoma tena, nikaomba chuo hicho hicho kufanya Bsc in Business Administration miaka 3, nikamaliza na GPA ya kawaida baada ya supplementary 2 nikachomoka na gentleman pass kama wanavyoiita.
Nikatafuta kazi sikupata, ila nikafanya kazi ya muda ya kufundisha secondary miezi 6 nikaona mizinguo tu, nikaona nirudi shule tena, nikaenda chuo kingine (Jina Kapuni) nikaomba nifanye Masters in Public Administration, sikupata sababu kwanza pass zangu hazikuwa za juu kwenye Degree yangu na pili Masters nayoomba ni tofauti na Degree yangu.
Nikaona isiwe shida, nikaomba Postgraduate Diploma ya Public Administration Mwaka mmoja, nikamaliza - nilivyomaliza tu nikaunga Masters in Public Administration - nikamaliza baada ya kukamatwa kamatwa mara kibao.
Sasa nataka kufanya PHD, ila kuna muda huwa najishtukia kuhusu elimu yangu, ndiyo maana nimeona niweke hapa ili mnieleze kama ipo Genuine na mimi naweza kujiita msomi wa nchi hii yaani Mwanazuoni?