Uchaguzi 2020 Nina mashaka na idadi ya wapiga kura 2020

TOHATO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
1,170
3,775
Makadirio ya Idadi ya watu Tanzania 2020 ni Milioni 59.7.

Idadi hii imegawanyika kama ifuatavyo:

1. Walioko chini ya miaka 15 ni zaidi ya 44.8%
2. Katikati ya miaka 15 hadi 64 ni 52%
3. Walozidi miaka 64 ni 3%

Miaka inayoruhusiwa kupiga kura ni zaidi ya miaka 18 ambayo tukiangalia katika huo mgawanyo inaleta picha kuwa nusu au karibu na nusu ya Watanzania wako chini ya miaka 18.

Hivyo kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi tayari tuna idadi ambayo inakaribi milioni 29[(44.8%(chini ya miaka 15)+ a waliokuwa na miaka 15-17)] ikiwa hawaruhusiwi kupiga kura.

Point yangu:

Idadi ya ambao wamejiandikisha ni milioni 29(kama nimekosea nirekebishwe) Idadi hii inaenda sambamba au kukaribiana na idadi ya watanzania halali wanao ruhusiwa kupiga kura(bila kujiandikisha).

Kwa elimu ya watanzania na majukumu yao naeza kusema, waliojitokeza kwenye kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura haikuwa kubwa kutokana na sababu kama zifuatazo

1. Kununuliwa kwa wapinzani(hivyo watu wengi kupuuzia hata swala la kuja kupiga kura)

2. Kupatikana kitambulisho ambacho kina nguvu kuliko cha kura (Kitambulisho cha Taifa kimeonekana kina nguvu sana katika maswala mengi hivyo watu wengi walokuwa wakijiandikisha kwa ajili ya kupata kitambulisho cha kura kwajili ya kazi zao, kupuuzia baada ya kupata mbadala.)

3. Mchezo mchafu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka jana(2019) huu ulipunguza kasi sana na morali kwa watu wengi.

Kwa hayo machache: Je, tunakubali kuwa idadi tulopewa ya walojiandikisha ni sawa?

Kama sio sawa basi kutakuwepo watu hewa ambao kazi yake wahusika wanaijua ni ipi.

Na kama ni kweli, basi niwapongeze sana NEC kuhamasisha watu kujiandikisha Kwenye Daftari la uchaguzi.
 
Hii hoja nina zaidi ya wiki mbili nikisema hiyo idadi ya wapiga kura 29m+ ni ya kupika, na lengo haswa ni kumtangaza Magufuli kwa kura za kishindo. Hii maana yake ni kuwa matokeo tayari, ndio maana inatumika nguvu kubwa kuhakikisha Lissu anaenguliwa, na anaposema safari hii hatuamuachia Mungu inakuwa balaa. Tukubali tukatae, machafuko ya uchaguzi huu yataletwa na NEC. wapinzani waweke pingamizi la idadi ya wapiga kura haraka iwezekanavyo.
 
Kweli inatia Shaka milioni 29 mmmmh siamini hata Mimi.

Hapa kwenye idadi ya wapiga kura ndio mchezo wote ulipo. Ingia hata kwenye tovuti ya tume hawajaweka hiyo idadi maana wanajua mchezo wote ndipo ulipo. Hata MATAGA humu mitandaoni ukiwapa hiyo idadi wote wanakimbia maana wanajua ni hiyo idadi ni uongo wa wazi.

Cc: Yehodaya, Crimea, jingalao, the tallest
 
Wapiga kura hapa hawazidi million 26

Exactly, hapo ndio bao la mkono lilipo. Kila mara ccm wanasema Magufuli atashinda kwa 90%+, wanajua kabisa hii idadi ndio wataitumia. Ingia tovuti ya tume hata idadi hawataki kuiweka, ila wanaitaja majukwaani maana wanajua uhuni wote umo humo. Wapinzani waweke pingamizi la idadi ya wapiga kura waone jinsi watu watatafutana.
 
Cdm munahofu kubwa sana ya kushindwa. Mwisho wa siku mutajikuta hata nyinyi wenyewe hapo ufipa hamuaminiani.
Kama unaona tume imekosea, lete wewe idadi yako iliyo sahihi.
 
Kuna hoja gani hapo mkuu?. Yeye aweke data zake hapa ndio tujadili.

Data ni kuwa hiyo idadi ya tume ya uchaguzi ni ya kupika. Watanzania tunakaribia 60m, inawezekana vipi watu 29m+ kujiandikisha kupiga kura? Yaani kila watu wawili mmoja kajiandikisha kura, jambo hilo sio kweli kabisa. Kama maneno marahisi watu wote wenye miaka 18 na kuendelea wamejiandikisha kupiga kura. Kama NEC ina idadi fake ya wapiga kura, hata matokeo itatangaza fake.
 
TOHATO,

Mil 29 waliojiandikisha ni uongo mtupu , ningependa Zitto na Lissu wafaye randomly uhakiki wa wapiga kura,hapo bao la mkono la masaki linaandaliwa...

Kama vituo vya kura vipo elfu 88 basi inabidi waandae Sehemu zao za kupokea matokeo ya kila kituo na kuyaandika online ,wasikae sehemu moja ,kulingana na advance ya technology kwa sasa kuna zoom meeting , kuna Telegram wanaweza wakala wakajiunga kwenye magroup na kupost matokeo nchi nzima ,kisha wakala wakisha hesabu watume fasta kwenye group na kila group liwe na mtu ambaye atakuwa ana update makao makuu! Then wapige hesabu ya jumla

"Mwaka huu hakuna kulia tena either watangaze matokeo halisi au Tunalia wote" - Benson
 
Back
Top Bottom