Nina mashaka na huyu mwanamke

NAKAZIA KWA HERUFI KUBWA!!
 
[emoji3][emoji3][emoji3] subiri waje wakuambie unahukumu, kwani wewe ni mtakatifu? Kuna kaka mmoja tulikuwa tynafanya kazi wote eti siku hiyo anatuambia eti yeye na girlfriend wake walikuwa wanapiga magoti pamoja wanaomba Mungu awape mtoto, na walipata mapacha. Nilicheka nikasema Mungu huyu kweli anajua kuchukuliana na akili za sisi waja wake. Huwa namuelewa sana Abiud Misholi na wimbo wake ule anaimba ' Ni wewe Mungu pekee wastahili cheo hicho'. Kuna muda wanadamu tunafanya mambo ya ajabu lakini tunachukulia kawaida eti Mungu anasamehe daah ningekuwa mimi ni Mungu hakika nisingevumilia huo ujinga.
 
Hakuna ushiikina wala uchawi hapo. Ondoa wasiwasi kabisa mkuu wala usiyafikirie hayo mambo yatakuathir kisaikolojia. Bado una safari ndefu sana na huyo binti na ni vibaya kuanza kuingiza wasiwasi au mashaka juu yake.
 
Bwana wewe hebu jifanye hujui kitu kwanza ukiendelea kumchunguza kwa karibu ujiridhishe,kama ni kwel kuna uhusiano na shirki achana na huyo mwanamke.Mtu akishaingia kwenye ushirikina hata kwa nia njema baada ya muda atabadilika tu!!
 
me nadhani,rudia tena kufanya utafiti..kama ni ushirikina atakuwa anarudia mara kwa mara...ukimkuta tena,mkamate red handed...hapo maamuzi yatakuwa ni yako
 
Kaona unasuasua kakutana wa wajanja wamemfundisha mbinu... Kabla hajaharibika zaidi na kama unampenda kwa dhati... Ongea naye kwa upole na makhaba.. Mweleze ubaya na athari wa kitu alichofanya kisha mhakikishie ndoa..
Mtu akishaanza ibada za kikwetu ngumu sana kumtoa japo inawezekana kwa nguvu sana, bora umshauri atafute uelekeo mwingine ndio njia rahisi.
 
Oga maji kuwa zezeta akuendeshe umuoe uachane na wengi magonjwa yakuache ufurahia maisha nyie wawili. Over
 
Unawekewa dawa Mzeiya shtuka
 
Kwa sisi wakristo, ndoa ni ya Muda wote wa maisha. Huoni ni vema kwamba nijiridhishe kwa kila kitu kabla sijaamua kuingia huko?
Mstiri mtoto wa watu acha kutafuta sababu. Mtu mpaka anakuhangaikia hivyo ni ww ndio huenda unayataka, anakupenda halafu unataka kujifanya kichwa ngumu.
 
Naelewa hali hii. Hata kama ni ndoa, siwezi tu nikafanya hivyo ndani ya mwaka mmoja tangu nijuane nae. Kuna mengi inabidi nijiridhishe. Hususani katika kipindi ambacho nipo nae. Hayo ya kufanya mapenzi na mengine yapo katika njia hiyo hiyo.

Pengine nisingeyaona haya niliyoyaona leo, nisingeweka huu uzi.

Mapenzi sio msaada mpaka mtu useme amejitolea. Ni maelewano ya watu wawili nadhani wakiwa timamu kabisa. Na ndio maana sio kila mahusiano yaishie kwenye ndoa.
 
Uwa mnasali pamoja baada ya kusali mnazini pamoja sasa uwa mnasali nin? Km sio kumukebehi Mungu acheni unafiki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…