Wana MMU, salamu kwenu!
Hii ni thread yangu ya kwanza kwenye kwenye hili jukwaa, imenilazimu kuja kuomba ushauri kwa hili lililonikuta. Issue iko hivi,
Mwaka 2010 nilikutana na binti mrembo mmoja hapa mtaani kwetu, alikuja kukaa kwa mama yake Mdogo hapa mtaani. Binti alikuwa mrembo kweli kweli, basi kama ambavyo wanaume tulivyoumbwa nikaomba mchezo, akazingua! Nikaimba nyimbo zote za kinyakyusa lkn binti bado akadai ana boyfriend wake na anampenda sana. Nikaona isiwe shida nikaachana nae baadae akaondoka mtaani akarudi kwao mwanza na mawasiliano yakafa!
January mwaka huu siku moja nikiwa njiani natoka ofisini simu yangu ikaita, kupokea ni yule mrembo! Akaanza maneno, umeoa, nikamjibu bado! Hapo ndipo tulipoanza tena mawasiliano, nikashangaa binti mwenyewe ndiye anataka uhusiano! Baada ya kama wiki moja ya mahusiano ya kwenye simu, tukiwa tumepanga tuonanie Mkoa fulani, akaniuliza swali kama nitaweza kuoa mwanamke mwenye mtoto??
Nikamuuliza kwani una mtoto?? Akajibu ndio, wa umri wa miezi sita na aliyempa mimba kamkataa! Baada ya kunieleza hivyo nikashangaa ule Upendo wote niliokua nao juu yake ukaisha ghafla! Kichwani kwangu nikawakuta nawaza huyu binti anajisogeza kwangu Kwasababu yuko matatizoni, hasa financially! Anataka anipe majukumu ya kumlelea mtoto!
Baada ya kuwaza hivyo nikampiga chini! Tatizo eti kila siku ananipigia simu analia, eti ananipenda! Wadau hapa mnaona Upendo kweli hapa???
Au nakosea jamani, hebu niambieni, nimuoe au nimpotezee??