Una bahati sana ndugu ila kuwa makini magari mengine si magari hayo ni majini yanatafuna pesa kuliko kipato chako utakopa hadi uje kustuka na wewe utamuuzia mtu elfu 20
Mkuu kupaki usafiri nje ya nyumba ni kitendo cha ujasiri si wote wanapata hiyo fulsa.
Utani na masihala hapana.Mwaka ndio unaishia hivo na kiukweli malengo yangu yakukusanya angalau laki 2 nimeyafikisha sina budi kujipongeza kwa hilo.
Sasa nahitaji kausafiri kwani nimechoka kutembea kwa miguu,kuna jamaa anataka kuniuzia hiace na amesema ataniuzia kwa laki 2 na nusu.hiyo gari ya mwaka 1975 haina viti ila si mbaya ntachonga hata vya mbao kwa kuanzia na kama mambo yataenda vizuri ntaifanya daladala.mlango wa abiria haufungi ila nayo si hoja abiria atakae kaa mlangoni ataushikilia na kupata punguzo la nauli.sasa wadau bei hiyo ni sawa au jamaa anataka kunigonga sana?na je route ipi italipa vizuri kwa hapa dar iwapo nitaamua kuifanya daladala?
Ushauri tafadhali!
ongeza laki tatu upate hiyo..ni kama mpya but mint condition,hehe,haina michubuko,charge ya battery haisumbui,warranty week moja..breki ndiyo inahitaji marekebisho kidogo..utapewa na huyo mrembo kwa ajili ya training nusu siku.
![]()
Kabisaa....kutofunga sio issue hata kidogo afadhali ingekuwa haufunguki, abiria wangegoma kupitia dirishani. kuhusu route kwa dar, piga mbagala kwa nyoka hadi kingugi.
hahahaha hiyo route ni kiboko kuna tetenasi za kufa mtu yani usiende kule usiku kama we mgeni maana utadhania unapishana na boda boda kumbe kibus kina taa moja hafifuu.
miaka kama 6 iliyopita niliwahi shuhudia tochi ile ya chuma imefungwa na mpira kwenye side mirror ya dereva ikitumika kama taa ya kuongozea gari nilichoka kabisa. :faint2:
Je huko naweza kupata kwa bei nzuri kidogo? Tatizo umbali na nishati imepanda bei mkuu.
Miss chagga Tyta anataka kunichonganisha na traffic na hivi wamepata big braza mpya watanimaliza.
ongeza laki tatu upate hiyo..ni kama mpya but mint condition,hehe,haina michubuko,charge ya battery haisumbui,warranty week moja..breki ndiyo inahitaji marekebisho kidogo..utapewa na huyo mrembo kwa ajili ya training nusu siku.
![]()
Ila huko inaonekana abiria watakua si wabishi so itakuwa rahisi kuwapanga kwenye gari na kuwapa kazi ya kushikilia mlango.