heheheheh pole mwaya....kama ulikuwa umekasirika heri umwhairisha mnaweza kuboana bure....
Ila ungemuuliza saluni alikuwa anaenda kufanya nini, kama kuset sawa....kama kusuka mngepanga siku nyingine...
Ila nae atakuwa kajifunza
Nilishajifunza wangu nikimwambia tuna "mtoko" huwa naweka masaa mawili ya ziada ya tahadhari.We acha tu akitoka bafuni sijui ndiyo aanze mbwembwe kwenye dressing table utachoka.Jifunze kuvumila mkuu.
Sangita ndio nini?
ni aina ya nywele zinazosukwa kwa masaa 12 au siku 2 ukizubaa.
Zile za kimasai
labda alianza jana, akajua leo saa 6 atakuwa kamalizwa, kumbe where.
tehe tehe tehe.............aliniambia anasuka rasta za wevu na leo ndio anamalizia....................Lakini mzoefu wa hiyo mambo kwa nini hakukadiria vizuri!!!!!!!!
Uvumilivu mwingine una mwisho......Ngoja ajifunze kwanza.......Biashar ya kutiana vidonda vya tumbo siiwezi
hivi unajua mambo ya saluni za akina mama?
Hasa kama unasukwa??
Akija mteja wa kuset, unayesukwa unawekwa kando, anaseiwa kwanza, hapo muda unaenda tu.
Mie haya yalinipata mno enzi hizo, alikuwa naongea hadi mdomo unataka kuchomoka.
Matokeo yake, nikiona na mtoko naye, kama sijasuka sisuki ng'o, ntapiga hata twende kilioni.
Nilitiwa ndimu nikawa na adabu hadi kesho, hadi naingia kaburini.
Unanicheka sio!!!!
Hujakosea kabisa siyo vizuri kulea ugonjwa, action speaks louder than words. Mie ndo zangu hizo na nimeishaona matunda yake, yaani wife amechelewa sana ni 30 minutes tena hapo ni mtoko usiokuwa na haraka otherwise atanikuta kwenye eneo la tukio nalamba bia. Na nikiishatangulia kwenye venue hata asipokuja ni pouwah tu coz east west home is the best.
Inaudhi sana masaa 5 na bora angesema mapema kuwa atachelewa. Picha niliyopata ni kama hajali hivi.