Nina imani kubwa na uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa. Hongera Rais Samia kwa uteuzi huu

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Dkt. H.G. Mugala, Mchambuzi wa Masuala ya Siasa na Utawala.

Awali ya yote ninampongeza Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi huu alioufanya, nimepitia jina moja baada ya jingine ikiwemo wateuliwa wapya na wale ambao wanaendelea kubakia katika nafasi zao, hakika nimeona kuwa kuna sura ambazo zinakwenda kuwajibika ipasavyo katika majukumu yao kulitumikia Taifa hili kutokana sifa za uongozi na uwajibikaji wao , kwa kuwa ni waadilifu na uzoefu wa kutosha.

Pia, ninawapongeza waliomshauri Rais kufanya uteuzi huo , kwa kuwa una mwanga unaoakisi matarajio ya maendeleo ya wananchi walio wengi katika maeneo yao.

Walioteuliwa hawa walioaminiwa na Rais SAMIA ni matarajio ya wananchi katika kuhakikisha wanatatua changamoto na migogoro iliyopo katika maeneo yao pamoja na kuhakikisha maendeleo anayoyataka Mhe Rais SAMIA kwa watanzania yanafikiwa. Hivyo pasi na shaka yoyote yajayo yanafurahisha.

Wito wangu kwa Watanzania tutoe ushirikiano wa kutosha kwa wateuliwa hao pindi wakapoapishwa kuanza kutekeleza majukumu yao katika mikoa yetu ili kuendana na maono ya Rais SAMIA ambayo haswa yanalenga kuendelea kujenga ustawi wa maendeleo ya Taifa letu.

Mungu ibariki Tanzania
 
Mwanaume wa kweli Huwa ha sifu sifu vitu kama hivi;-

Ungeimba wimbo huu;-

Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"!!
 
Back
Top Bottom