Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 10,176
- 16,240
Habari za wakati huu ndugu zangu
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30+ , sijaoa na wala sina mpenzi wakudumu yaani mwanamke wakuoa bado sijapata..
Nimekua nikikutana na hali ya huzuni sana na kuumia moyo au kusikia kama kulipuka ndani ya moyo wangu ninapo kutana na mazingira kama haya ndugu zangu na hali hii ilianzakunikuta miaka mitatu iliyopita baada ya kuachwa na mwanamke niliempenda sana kwa kweli
1: Nikiona na kusikia mwanamke analia napatwa na huzuni kuu moyoni na kujisikia kuumia sana kiasi kwamba naondoka eneo hilo na kama ni maeneo ninamo ishi na vaa earphone au kuweka sauti kubwa kwenye radio nisisikie chochote
2: Naumia sana kuona mwanamke akiwa anapigwa inaniuma sana moyoni mwangu
3: naumia sana kuona watu wa kigombaa hasa hasa watu wazima au wakiwa wanaongea kwa uchungu sana inaniuma kweli
4: Ninapopata taarifa za kuhuzunisha kama misiba, magonjwa kwa watu wanao nizunguka , ajali yeyote inaniuma sana nina huzunika sana
5: Moyoni wangu umekua unahuzunika sana hasa hasa pale ninapo ona mtu mzima analia kwa sauti au ninapo ona machozi ya mtu mzima na migogoro nakua na huzunika sana
6: nikiangalia movie au kusikiliza story zenye maudhui ya kusikitisha au ukorofi na patwa na huzuni kali pia
Nb.. Huzuni zinapo nijia muda mwingine zinaambatana na mwili mzima kutetemeka kama mtu aliepigwa na baridi kali na nakua naongea kwa kutetemeka sana ( kwa kung'ata meno)
NIMEHANGAIKA SANA NA WATAALAMU WA AFYA KUTATUA HILI TATIZ LAKINI KWA KWELI NAONA NAO WAMESHINDWA MPAKA WANAFIKIA MAHALI KUNIAMBIA NIWE NAOMBA SANA
Naombeni msaada ndugu zangu , nifanyeje ndugu zangu
Hili tatizo mara nyingi huwa linatokana na maisha yako ya Utotoni yalikuwaje?
1. Ulikuwa unanyanyasika sana?
2. uliishi na wazazi wote wawili? au mzazi mmoja?
3. Ulipata malezi kutoka kwa ndugu wengine?
4. Ulikuwa unafanywa kichekesho ?
Hili tatizo lako lina suluhisho ninaku PM namba ya Phycologist utampigia na utaongea nae