"Nina Haraka"

"Nina Haraka"

b5-click

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2012
Posts
2,194
Reaction score
2,114
Imepita miaka 17 tangu nikutane na kupotezana na huyu Dada.

Pia ni miezi kadhaa toka niondoke nchini na kwenda Moja ya nchi za Afrika Magharibi kikazi, nimerejea nyumbani mwisho wa wiki iliyopita na nimeripoti kazini jumatatu ya Jana, tukio ninaloenda kukuhadithia limetokea Leo hii na muda huu, "Muda wa Lunch"

Mimi hupenda sana inapofika muda kama huu kutoka katika chumba cha ofisi yangu na kwenda kupata Misosi na Kuzimua kidogo konyagi ndogo au Ganja, kisha hurejea kazini kuhudumia taifa hili lenye wananchi maskini kama Mimi, sasa Leo mchana nikapata taarifa za mgahawa unaokimbiza sana hapa mjini kwa sasa nikaona isiwe shaka ngoja niende zangu hapo nikapate Msosi, sikuwa peke yangu nilikua na moja kati ya watu wangu wa karibu ambaye ndiye alinipa habari za mgahawa huu.

Mara baada ya kufika tukapokelewa na muhudumu mmoja mzuri sana, mzuri kiukweli, kwa bashasha akatukaribisha na kutuhudumia, muhudumu huyu sura yake si ngeni sana machoni pangu, Ila sikumbuki nilikutana nae wapi.

Mungu si athumani, yeye alinikumbuka na kunitambua kisha akaanza kunikumbusha jinsi nilivyo-mfatilia sana enzi hizo akiwa bado mbichi, hapa ndipo kumbukumbu zangu zikarejea sawasawa, miaka 17 iliyopita huyu binti alinitesa sana tena sana (maana nilikua namzimia kinoma) wakati huo mimi nilikua nasoma stashahada yangu na yeye alikua ni mtoto wa mkuu wa chuo nilichokua ninasoma,

Kilichonifanya niandike Uzi huu ni jinsi binti huyu alivokuwa akinijibu miaka hiyo ya 2000 kila wakati nilipotaka kuongea nae, yeye alinidharau sana na kupenda kunijibu SINA MUDA.. Leo naona kapata muda, Hakika maisha ni duara, Leo na Mimi nimemjibu sina muda ila kama ana yeye ana Muda anitafute (nimemuachia namba), na naona kasha nitumia SMS

Ninawashauri jambo wadada, kuweni makini na tambueni kuna kesho (Japo Haifikagi), Maringo na nyodo ni hulka yenu ila mnapaswa kuwa makini.
 
kwanza huyo binti anaakili sana kwa kipindi hicho alikua mdogo ulitaka akukubali tu kisa unamtaka? imagine umepanda maua nyumbani kwako yamechanua lakini kila mpita njia anachuma bila kuzuiliwa je hayo maua yataendelea kuchanua? alijitunza kwakua wewe kwa sasa unahela na msomi ndio unataka kutumia kiboko hicho haya endelea
 
pasha kiporo acha kuzingua
Hahah haa, siwezi kukiacha napenda sana kuivunja amri ya sita ya binaadam kwamaana Mungu alivotuumba Me na kuwafanya Ke hakumaanisha tuchekeane, alitaka tuifaidi dunia kwa uasili wake kando na starehe za kutengenezwa na binaadam, ndio maana nimempa namba.
 
Imepita miaka 17 tangu nikutane na kupotezana na huyu Dada.

Pia ni miezi kadhaa toka niondoke nchini na kwenda Moja ya nchi za Afrika Magharibi kikazi, nimerejea nyumbani mwisho wa wiki iliyopita na nimeripoti kazini jumatatu ya Jana, tukio ninaloenda kukuhadithia limetokea Leo hii na muda huu, "Muda wa Lunch"

Mimi hupenda sana inapofika muda kama huu kutoka katika chumba cha ofisi yangu na kwenda kupata Misosi na Kuzimua kidogo konyagi ndogo au Ganja, kisha hurejea kazini kuhudumia taifa hili lenye wananchi maskini kama Mimi, sasa Leo mchana nikapata taarifa za mgahawa unaokimbiza sana hapa mjini kwa sasa nikaona isiwe shaka ngoja niende zangu hapo nikapate Msosi, sikuwa peke yangu nilikua na moja kati ya watu wangu wa karibu ambaye ndiye alinipa habari za mgahawa huu.

Mara baada ya kufika tukapokelewa na muhudumu mmoja mzuri sana, mzuri kiukweli, kwa bashasha akatukaribisha na kutuhudumia, muhudumu huyu sura yake si ngeni sana machoni pangu, Ila sikumbuki nilikutana nae wapi.

Mungu si athumani, yeye alinikumbuka na kunitambua kisha akaanza kunikumbusha jinsi nilivyo-mfatilia sana enzi hizo akiwa bado mbichi, hapa ndipo kumbukumbu zangu zikarejea sawasawa, miaka 17 iliyopita huyu binti alinitesa sana tena sana (maana nilikua namzimia kinoma) wakati huo mimi nilikua nasoma stashahada yangu na yeye alikua ni mtoto wa mkuu wa chuo nilichokua ninasoma,

Kilichonifanya niandike Uzi huu ni jinsi binti huyu alivokuwa akinijibu miaka hiyo ya 2000 kila wakati nilipotaka kuongea nae, yeye alinidharau sana na kupenda kunijibu SINA MUDA.. Leo naona kapata muda, Hakika maisha ni duara, Leo na Mimi nimemjibu sina muda ila kama ana yeye ana Muda anitafute (nimemuachia namba), na naona kasha nitumia SMS

Ninawashauri jambo wadada, kuweni makini na tambueni kuna kesho (Japo Haifikagi), Maringo na nyodo ni hulka yenu ila mnapaswa kuwa makini.
bosi yana huyo ukiweka ndani mbona hupati tabu maana hata kuwa mpole zaidi ya pilitoni,kama una mke potezea
 
Kiongozi, mbona sioni mantiki ya kutaja safari zako za nje ya TZ kwenye hii posti yako?

Nategemea UTAKAPORUDI KUTOKA Europe ndio utatupa mrejesho wa kilichofuata.......
 
.......Muda wa misosi ni kawaida yako kuzimua Konyagi na ganja....
Sawaaa....nitarudi jombaa...
 
Kiongozi, mbona sioni mantiki ya kutaja safari zako za nje ya TZ kwenye hii posti yako?

Nategemea UTAKAPORUDI KUTOKA Europe ndio utatupa mrejesho wa kilichofuata.......
Maisha yetu yamepata kuingiliana ktk vipindi viwili tofauti, tukiwa na hali tofauti tofauti, lakini hii yote ni kuonyesha upendo unatakiwa usimame bila kujali hali za maisha.
 
Kwahiyo ulitaka ukutane naye amekuzidi kipato ndio umuone bado bora?!
Mimi nilimuona na bado namuona bora, ila kinyume chake yeye sasa nahisi ananiona bora, wakati nampenda haswa alikua ananiona famba.
 
Back
Top Bottom