Nina haja nawe kila saa

Nina haja nawe kila saa

Mtu wa Mungu naomba nikutie moyo katika vita unavyopitia maishani. Mungu ameruhusu hivyo vita maana anajua njia ya pekee ya wewe kuendelea kuimarika katika maisha yako ya imani na mahusiano yako na Yeye ni kwa njia ya hivyo vita na hizo changamoto unazopitia maishani.

Kumbuka siku zote uwapo vitani, haijalishi hiyo vita ni kubwa kiasi gani, si kubwa ukilinganisha na vita vilivyo mbele yako katika siku za usoni. Vita vya jana vinakuandaa kwa ajili ya vita vya leo na kadhalika vita vya leo vinakuandaa kwa ajili ya vita vya kesho.

Wakati Daudi akiwa peke yake kule nyikani na kondoo za baba yake, alitokewa na dubu na simba. Daudi angeweza kukimbia maana kw a kweli ukilinganisha dubu na simba na Daudi, Daudi asingekuwa kabisa na uwezo kwa namna ya kawaida kukabiliana nao. Lakini Daudi katika ushuhuda wake kwa Sauli alisema kuwa Mungu alimwokoa na kinywa na makucha ya Dubu na Simba.Ushuhuda wa vita vyake vya jana vilikuwa kianzio vya vita vyake vya leo. Daudi aliandaliwa na vita vyake dhidi ya dubu na simba kukabiliana na Goliati maana Mungu aliyemwona alipokabiliana na dubu na simba alikuwa na uhakika kabisa kuwa ni Mungu atakayemwona atakapokabiliana na Goliati.

Usidharau vita vyako vya leo maana vinakuandaa kwa ajili ya vita kubwa zaidi kesho. Mungu anaikuza imani yako kupitia vita vyako vya leo ili iwe imara vya kutosha kwa ajili ya vita vyako vya kesho.

Usikubali kunyong’onyeshwa na pito lolote la leo.

Chukulia kama ni maandalizi kwa ajili ya mapito makubwa zaidi kesho.

Endelea kumwamini Mungu katika lile ulipitialo leo.

Katikati ya vita unavyopitia ukihakikisha haya unayafanya kwa uaminifu na nidhamu ya hali ya juu utu wako wa ndani utazidi kuimarishwa katika hali hiyo unayopitia.

Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele. 2 KOR. 4:16-18 SUV
Ubarikiwe mkuu!!
 
Yesu nakuhitaji vivyo kila saa niwezeshe mwokozi nakuujia .??

Nimekosa nguvu kila saa matatizo.
Hayaishii huwezi ukasema nipo sawz sasa ukafurahi unaletewa jingine hadi mtu anachoka eti
Katika Wagalatia 6:5,
Imeandikwa,

"Maana kila mtu atauchukua, mzigo wake mwenyewe."

tafadhali,
beba mzigo wako kwa imani bila manung'uniko.

Lakini pia imeandikwa Mt. 11:28,
"Njooni kwangu ninyi nyote na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha." Imani yako kwa Mungu, ikutue mizigo yako kwa uaminifu, maneno na vitendo vyako mwenyewe.

Hata kwenye ile Zaburi 23:1 inayosema,
"Bwana ndie mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu "

nadhani kama waKristo, inafaa kutumia biblilia kama formula ya kujiondoa kwenye mikwamo ya kimwili na kiroho.

Ni muhimu sana kua makini,
maana laumu zetu zinaweza kutuvunja moyo na kutukatisha tamaa wenyewe.

Daima,
pale unapokua dhaifu ndipo yafaa uwe na nguvu zaidi 🐒
 
YESU ANAABUDIWA KWENYE kurani kwamba ni Mungu na hakufa bali alipaa mbinguni.
Surah An-Nisā (4:157–158)
وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ ... بَل رَّفَعَهُ ٱللَّهُ إِلَيْهِ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمًا

“Wala hawakumuuwa, wala hawakumsulibisha, bali iliwadhihirikia hivyo tu. Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwake...”
 
Sasa hapo wapi waliposema anaabudiwa?
 
YESU ANAABUDIWA KWENYE kurani kwamba ni Mungu na hakufa bali alipaa mbinguni.
Surah An-Nisā (4:157–158)
وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ ... بَل رَّفَعَهُ ٱللَّهُ إِلَيْهِ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمًا

“Wala hawakumuuwa, wala hawakumsulibisha, bali iliwadhihirikia hivyo tu. Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwake...”
Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwake sio Alijinyanyua kwake , labda kiswahili kinakupa taabu

View: https://www.instagram.com/reel/DYzDbUIozsh/?igsh=eTNxMm1sMXM2YTlu
 
urudi ukachapwe kiboko 🍆 na mwl wa madrasa ili akukumbushe kusoma vzuri 💩

  • Yohana 17:3: Katika maombi yake, Yesu anamtambulisha Mungu pekee: "Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma."
  • Marko 10:18: Yesu anajibu: "Mbona kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ni Mungu."
  • Hesabu 23:19: Agano la Kale linaweka wazi asili ya Mungu: "Mungu si mtu, hata akasema uongo..." Yesu (kama mwanadamu) hawezi kuwa Mungu.
 
Hallelujah YESU Kristo ni Mungu, ndani ya dakika chache umemkiri YESU kwa kulisoma neno lake.
Hapo ndipo mnapo shindwa akili na wakristo
 
Back
Top Bottom