Nina double life

Nina double life

Ishawahi kutokea huku,ukakesha.

Then usiku ulifuqta wakati umelala,umeamkia kule,what happened?

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
Sina kazi za kukesha. Lakini siku moja nilisinzia kwenye basi nikiwa naenda Mbeya. Nikaota kuwa nimeenda swimming nikiwa na mke na mtoto, halafu mtoto akazama. Niliporukia kwenye pool kumwokoa nikavuta maji yakanipalia nikakohoa sana nikazinduka nikajikuta kweli nimepaliwa na mate na ninakohoa.
 
Kwenye hiyo ofisi ya kuuza pikipiki ndio kuna hiyo computer ?!
Ndiyo. Ni ofisi kubwa ina show room kubwa sana yenye pikipiki za aina mbalimbali zaidi ya 2,000 for display only. Kuna vitengo vingi vya sales, marketing, accounts, workshop ina mafundi wa aina mbalimbali, pia kuna godown kubwa lenye parts mbalimbali za pikipiki ambazo wanaoagiza kutoka nje ya nchi wanafungashiwa kwenye mabox wanatumiwa na kwenda kufanyia assemblying kwao. Kuna yard kubwa ina makontena mengi yaliyojaa parts za pikipiki ndani ya mabox for export.
 
Mkuu hauna disorder yoyote...sio MPD au chochote kinachoendelea kwenye maisha yako ni bahati kubwa sana na wanayo watu wachache

Unaishi kwenye dimension mbili tofauti...kwa wakati mmoja ambayo huwa hairuhusiwi au sio rahisi..unaishi kwenye future ndotoni na unaishi maisha ya sasa hv in reality..

Dimension huwa haziingiliani mpaka ufe ndio unaenda kwenye dimension nyingine..zako unaziishi kwa wakati mmoja

Ushauri kuna watu wanafanya utafiti kuhusu dimensions na time travel watafute nafkiri utakua tajiri kabisa, kingine from today pay attention sana kwenye ndoto inaonekana technology inayotumika ni cutting edge...jaribu kuchukua maarifa uyalete kwenye maisha ya kawaida pay attention

Swiss nafkiri na sweden wanafanya sana tafiti pia soma online kuhusu dimensions uko gifted
Asante kwa ushauri, nikipata muda nitaingia chimbo google nisome kuhusu hiyo ya dimensions uliyoniambia.
Kuhusu kuchukua maarifa ya ndotoni hilo jambo naona lina ugumu sana. Sina control yoyote ya nitakachokutana nacho nitakapoenda kulala usiku wa leo na kuendelea na ndoto. Nilishawahi kupanga kufanya hivyo, lakini mipango yote niliyofanya kabla ya kulala iliishia pale nilipolala, nilipoanza kuota yakawa mambo mapya kabisa ni sikuwa na kumbukumbu yoyote. Nilipozinduka ndipo nikakumbuka nilichopanga kabla ya kulala na kwamba sikukitekeleza!
 
Alafu kwani usiku hushtukagi hata kwenda haja ndogo hv,vipi ukiwa safarini una drive bila kulala au msibani? Je? Mkeo unakutana nae kimwili saa ngapi? Maana inaonesha ukilala umelala kwani akuhamshagi au kukushtua kama saa 8 hv au sita, response yako inakuaje? Je? Uliwah kumsimulia mke au wazazi wako Hilo tukio? Je? Walikushaur nini?.
Huwa sishtuki kwenda haja ndogo. Mke wangu tunafanya kabla hatujalala, na siyo kila siku. Siku hizi tunafanya mara moja kwa wiki, hasa hasa wikiendi, wakati mwingine mchana (tuko over 50), lakini yule wa ndotoni ni daily maana katika ndoto ni kijana. Kushtuka usiku huwa inatokea kama ajali, mfano siku moja katika ndoto niliota nimeteleza kwenye tiles nikaanguka halafu mlinzi akanidaka kabla sijafika chini, na hapohapo nikazinduka usingizini nikakuta mke wangu ananitingisha mabega kuniamsha! Nilipomuuliza kunani akasema amesikia kishindo nje, nilipotoka kuangalia nikakuta kuna mgomba jirani na dirisha ulikuwa na ndizi kubwa ulikuwa umevunjika, nadhani sababu ya upepo au kuelemewa. Nimeshasimulia mahali pengine kilichotokea siku moja niliposinzia kwenye basi. Na kuna ile siku niliyoota kuwa AC imelipuka ofisini tukatoka mbio kugombea mlango nikajigonga kwenye mlango wa kioo nikazinduka usingizini, kumbe kiuhalisia ni tubelight ya nje (imefungwa kwenye ukuta wa nyumba) ilipasuka kwa kishindo!
Kuhusu kusimulia niliwahi kusimulia siku za mwanzoni, baadaye nikaona naonekana kituko nikaacha. Hiyo ndoto nilianza kuota kuwa niko chuoni nasoma. Niliacha kusimulia pale nilipopata girlfriend humo ndotoni, nikahisi hiyo simulizi itamkwaza mke wangu, kwahiyo kuanzia hapo nimebaki na ndoto yangu.
 
Ndio maana nimesema baada ya kumsoma zaidi nimehisi ana matatizo mawili. Schizophrenia au DID na asilimia kubwa nimeiweka hapo kwenye Schizophrenia
Sina hiyo schizophrenia wala chochote kinachofanana hivyo. Sina hizo hallucinations au sijui sauti za maruweruwe wala chochote. Nafanya shughuli zangu mchana kama kawaida na nina afya nzuri, usiku nikilala naendelea na ndoto yangu.
 
Hichi ndio nilikuwa nakifikiria ingawa sikutaka kutoa conclusion yangu kwasababu sio rahisi kuweza kuishi kwenye dimensions zaidi ya moja at a go, huwa ni nadra sana kutokea kitu kama hicho.

Nikipata muda nitaelezea vizuri nilivyoweza kuitambua hiyo concept kwa upande wangu.
Naomba maelezo zaidi mkuu, it sounds interesting
 
Hichi ndio nilikuwa nakifikiria ingawa sikutaka kutoa conclusion yangu kwasababu sio rahisi kuweza kuishi kwenye dimensions zaidi ya moja at a go, huwa ni nadra sana kutokea kitu kama hicho.

Nikipata muda nitaelezea vizuri nilivyoweza kuitambua hiyo concept kwa upande wangu.
Naomba unitag, ukija kuelezea

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom