Nina Changamoto kubwa sana wadau inanisumbua... ushauri wenu muhimu

Hellow Jukwaani...

Kwa mara nyingine ninawasalimia. Wadau nina changamoto kubwa inanisumbua sana. Awali ya yote nipende kumshukru Mungu kwa hapa nilipofika maana bila mapenzi yake isingewezekana.

Nakumbuka niliweka thread humu kuhusu kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha sita na baadaye akajifungua mtoto wa kiume.

Sasa changamoto iliyopo ni baada ya kufika nyumbani kwao ambao walinipiga fine ya ng'ombe watatu majike hii ilikuwa kwa ajili ya kumwachicha mtoto wao shule, wakaniambia kulipa hela laki 8 ambayo waliita ya kukubaliwa kwao (kubisha hodi) na sambamba na hilo wakaomba laki 5 kama kishika uchumba cha mwanao, mwisho wakaomba niwe nampa mama mtoto laki 3 na nusu kila mwezi kwa ajili ya kuleo mtoto na mama kabla sijamuoa. Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu nimefanikiwa kuwapa ngombe, faini ya kubisha hodi na hiyo kishika uchumba.

Tatizo nililo nalo ni kwamba tulikubaliana hiyo ya kulea niitume kwa njia ya benki ili records ziwepo pande zote mbili ila mama mtoto akawa anomba hiyo hela nikawa namtumia kwenye simu yake, sasa yapata kama miezi 7 tangu tukubaliane... nimekuwa nikimtumia kwa njia hiyo na meseji nazitunza.

Juzi ndugu zake wakawa wameanza madai mapya wanataka rist za benki nikawaeleza kuwa nimeshamtumia kwa njia nyingine, wanadai eti hiyo hawaitambui, nikawa meseji za malipo bado hawatambui, ivi ni halali kweli? Nimetuma hela almost kila month bado wanaona sijafanya kitu? Nitawezaje kumtelekeza mtoto wao mm?

Kiukweli niliwaza sana ikabidi cha kwanza nimtoe kabisa hata huyo mama mtoto kwenye mipango ya kumuoa, naona kama familia yake hatutaeleawana maana wanafanya kama biashara sasa, nilichoamua kukifanya ni kutafta namna ya kurudiana na mchumba wangu ambaye nilimsaliti kwa huyu.. ingawa na yeye amekuwa na misimamo mikali huwa hanitaki tena na hatiweza kurudiana.

Ebu wana jamvi tushauliane, niache tu kutoa hizo pesa maana silaha yao kubwa imekuwa ni kunishitak ili nifungwe? Au nifanye nin, imekuwa kero kwangu.

NB: mama mtoto yuko kwa wazazi wake, walimkatalia mpaka nilipe mahari na taratibu zingine zifuate.

Nawatakia weekend njema.
Wewe msukuma eeh?
 
We nawe mzembe sana pesa zote hizo unagawa tu kizembe namna hiyo piga chini familia nzima form six ni mtu mzima kabisa sijui uliogopa nini
 
Malipo ya usaliti, pambana na hali yako chozi la mchumba wako litakuandama mpaka ukome ukomae
 
Mimi siwezi jikomit kwenye mambo ya hell
Eti kutuma 350 kwa mwezi huyo ana nini kipya
Kuna wazazi baba anlipwa 250,000 tu ana mke asiye na Kaz namtoto
 
Hellow Jukwaani...

Kwa mara nyingine ninawasalimia. Wadau nina changamoto kubwa inanisumbua sana. Awali ya yote nipende kumshukru Mungu kwa hapa nilipofika maana bila mapenzi yake isingewezekana.

Nakumbuka niliweka thread humu kuhusu kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha sita na baadaye akajifungua mtoto wa kiume.

Sasa changamoto iliyopo ni baada ya kufika nyumbani kwao ambao walinipiga fine ya ng'ombe watatu majike hii ilikuwa kwa ajili ya kumwachicha mtoto wao shule, wakaniambia kulipa hela laki 8 ambayo waliita ya kukubaliwa kwao (kubisha hodi) na sambamba na hilo wakaomba laki 5 kama kishika uchumba cha mwanao, mwisho wakaomba niwe nampa mama mtoto laki 3 na nusu kila mwezi kwa ajili ya kuleo mtoto na mama kabla sijamuoa. Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu nimefanikiwa kuwapa ngombe, faini ya kubisha hodi na hiyo kishika uchumba.

Tatizo nililo nalo ni kwamba tulikubaliana hiyo ya kulea niitume kwa njia ya benki ili records ziwepo pande zote mbili ila mama mtoto akawa anomba hiyo hela nikawa namtumia kwenye simu yake, sasa yapata kama miezi 7 tangu tukubaliane... nimekuwa nikimtumia kwa njia hiyo na meseji nazitunza.

Juzi ndugu zake wakawa wameanza madai mapya wanataka rist za benki nikawaeleza kuwa nimeshamtumia kwa njia nyingine, wanadai eti hiyo hawaitambui, nikawa meseji za malipo bado hawatambui, ivi ni halali kweli? Nimetuma hela almost kila month bado wanaona sijafanya kitu? Nitawezaje kumtelekeza mtoto wao mm?

Kiukweli niliwaza sana ikabidi cha kwanza nimtoe kabisa hata huyo mama mtoto kwenye mipango ya kumuoa, naona kama familia yake hatutaeleawana maana wanafanya kama biashara sasa, nilichoamua kukifanya ni kutafta namna ya kurudiana na mchumba wangu ambaye nilimsaliti kwa huyu.. ingawa na yeye amekuwa na misimamo mikali huwa hanitaki tena na hatiweza kurudiana.

Ebu wana jamvi tushauliane, niache tu kutoa hizo pesa maana silaha yao kubwa imekuwa ni kunishitak ili nifungwe? Au nifanye nin, imekuwa kero kwangu.

NB: mama mtoto yuko kwa wazazi wake, walimkatalia mpaka nilipe mahari na taratibu zingine zifuate.

Nawatakia weekend njema.
Pole sana brother.
Siku nyingine unatakiwa uombe ushauri kabla ya kulizwa namna hiyo.

Kifupi yaani wewe ni boya kabisa, yaani umetapeliwa na unaendelea kutapeliwa kipuuzi kabisa. Mwanaume hupaswi kuwa hivyo.

Ngoja nikufafanulie taratibu hapa hapa.
1/Kitendo cha wewe kumtia tu mimba huyo binti, ndugu zake walipaswa wakubembeleze au kukushinikiza umuoe huyo binti bure bure, yaana hata senti tano usingedaiwa.

2/Kitendo cha wao kukudai pesa na wewe kukubali kuwapa hizo pesa, maana yake walikuona wewe ni limbukeni na wewe ukakubali kuwa ni limbukeni. Katika zama hizi za ugumu wa maisha, hakunaga hizo mambo za kulipa pesa za kubisha hodi, kupigwa faini, Mahali nk. Kwa sasa kuna kitu kinaitwa Asante tu kama una senti mbili tatu basi unajitutumia na kukubali udaiwe milele lakini hutalipa na msichana unapewa bure na kiasi cha kuanzia maisha unapewa na hao hao wakwe zako.

USHAURI WANGU.

1/Katisha huduma kabisa, hicho ulichotoa mpaka sasa ni kiasi kikubwa sana. Usilipe chochote tena. Hutapoteza chochote. Hakuna kumuonea huruma mtu, kila mtu apambane na hali yake sasa.

2/Katisha mawasiliano na hao ndugu zake huyo msichana na pia katisha kabisa mawasiliano na huyo msichana uliyemzalisha mtoto. Potezea mazima. Ukiendelea nao ipo siku wanaweza hata kukufirisi au kukuangamiza kabisa.

3/Usiwaze kabisa kutaka kumuoa huyo msichana uliyemtia mimba na wala usijaribu kabisa kutaka kumuoa huyo mchumba wako wa zamani. Kwanini? Wote hao hawana nia njema na wewe. Wanakutumia tu kwa faida zao. Ukiwaoa watakuja kukutesa sana, wameshajua udhaifu wako na watautumia kama silaha ya kukutesa, kukutumikisha na kukufadhaisha. Achana nao kabisa.

4/Tafuta msichana mwingine kabisa wa kuja kumchumbia na kumuoa. Tengeneza ukurasa mpya wa maisha yako ili uishi kwa Amani na Furaha. Mabinti wazuri na warembo wametulia fresh kabisa wapo mtaani kibao. Tulia tu, chagua mmoja na usonge zako mbele.
 
Pole ila ulisahau kuwa karma never lies ,she always keeps receipt.... Unalipwa usaliti uliomfanyia mwenzako....
 
Mtoroshe binti huyo kwao watakosa pakuanzia akiwa kwako unawachiaje mboga wakati umewapa ng'ombe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom