That woman is a killer. Achana nae! wapi wengi wenye akili timamu.
Watu hukusoea mno kusema
'sijui kama nitaweza penda mwingine'
ukishajifunga hivyo utateseka mno....
rule ya maisha..ni moja tu
ukiona mtu anakutesa move on..
mkuu nashukuru kwa haya. lakini hebu nikueleze kitu kidogo nilitaka nikiweke siri ila sasa naona sina jinsi n naomba sana sana hunijui sikujui nishauri kwa utashi wako wote.Tatizo lako la kwanza ni kujiona huwezi k'kupata yeyote unaemtaka'
sasa kwa kuwa huyo alijitokeza na wewe ukaona umebahatika kumpata..
kumbe huyo ni kicheche tu kama vicheche wengine...sanasana angekusummbua kwenye ndoa
kuhusu kumuelewa..nani aliekuambia tunatakiwa kuwaelewa watu woote tunaokutana nao????
wengine wao wenyewe hawajielewi,why wewe uumize kichwa kuwaelewa?
just move on..tafuta mwingine....fast
Hakuna kitu kibaya kama kuishi kwa kutegemea uwepo wa mtu flani hasa mpenzi wako... .
kwanza pole sana mkuu,pili mbona kutoa mimba ni kama fashion karne hii? Sio kitu cha kushangaa saana ila wengi wanatoa kwa sababu ya matatizo ya aidha aliyempa hiyo mimba ameikataa au sababu nyingine nyingine zinazojulikana. Cha kujiuliza ni kwamba iweje aende kuitoa hiyo mimba ilhali wewe ulishakubali kuihudumia?
Kuna kitu kimefichika hapo,mtafute na ujaribu kuongea naye vizuri na kama majibu yake yatakuridhisha basi uamuzi ni wako umrudishe ndani ama la.
Huyo alikuwa ana KUCHEZEA tu, Mungu atakupa mwingine ambaye mtaISHI naye mkiCHEZA pamoja kwa uzuri.
Kabisa. Aachane nayr haraka sana. Unawezekana kabisa mimba aliyotoa sio ya jamaa yetu.
Cha muhimu ndugu yangu zingatia kazi na Mungu atakuonyesha mwingine. Huyu hakufai kabisa. Ni kawaida kwen maisha
Pole sana ndugu, ila usikate tamaa pambana sana tu, saka hizo hela hadi zianze kukusaka zenyewe tafuta mwanamke wa kuoa Mungu atakuonyesha, utampata tu, ila kwa huyo binti mi naona achana nae tu ile mimba sidhani kama ni yako, labda ungekaa nae uongee nae umsikilize kinagaubaga, ushauri wangu kwako ni
USIKATE TAMAA PAMBANA TU. yo in my prayers ndugu.
Kwanza Pole Sana Mkuu, nilivyoeelewa ni hivi:
Huyo mdada analiwa mzigo na wanaume wenzio huko kwao kwa kuwa hana njia nyingine ya kupata mkwanja.. Anafanya hivyo ili kujikimu, kumbuka ushamzoesha maisha mazuri kutokana na juhudi zako kazini.
Kwa Upande wa kutoa mimba sijafikiria kiundani sana, ila acha nikwambie kitu, kulea mimba ni kazi sana.. Kumbuka tayari anamtoto, mbaya zaidi amemlea kwa miaka 4 mwenyewe kabla ya kukutana na wewe, hivyo anajua machungu na Karaha zote za kulea... Kuna uwezekano hataki kushika mimba hiyo kwa sasa kwakua hataki kukumbuka magumu na mabaya yaliyotangulia..
Pia tukiangalia kutokea ktk angle nyingine inawezekana anakuepusha na lawama za kudumu.. Kuna uwezekano ukawa siyo ujauzito wako kwa kuzingatia kua muda mchache baada ya kurudi kwao amekua tayari kushiriki tendo la ndoa na wanaume wengine, hii ni kusema kwamba ana uzoefu wa mambo hayo, so pia inawezekana pia ulipokua nae alikua pia anagawa pembeni..
Ushauri wangu ni huu; Unajua alievaa kiatu ndiye ajuae msumali unachomea wapi, wewe binafsi ndiyo unafahamu nafasi ya huyo malkia ndani ya nafsi yako..
Hayo ni matatizo ya kawaida tu katika maisha ya ndoa hasa katika kizazi hiki cha digital bila kuzingatia kabila la shemeji yetu.
Kaa chini muyazungumze wewe na yeye.. Atakavyokua anarespond hoja ma mitazamo yako utajua usuke au unyoe..
WANAUME TUMEUMBWA MATESO
amina.
Lakini je naweza kufanya vipi ili nisione ugumu wa kutafuta mwanamke mwingine hasa nikiangalia niliwah kupooza miaka 6 iliyopita na uume wangu umeanza kusimama miaka 2 iliyopita. nilijifungua kwa huyu na kumweleza ukweli wote na alikubali hali yangu. kiukweli wajua hali ya ulemavu ilivyo, kwahiyo nilifarijika sana kupata mtu kama yeye. sasa je niambie nitafanyeje?