Nimwacheje huyu mama?

Nimwacheje huyu mama?

umukagame

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2014
Posts
1,044
Reaction score
675
Habari za wakati huu wakubwa

Naileta kwenu mnisaidie nimshauri huyu kijana

Anasema yeye ni mfanyakazi mwajiriwa serikalini, ana miaka 33 mwaka mmoja uliopita alianzisha mahusiano na mwanamke mmoja mtu mzima 40yrs ambaye kicheo yeye ni mkubwa wake kazini. Baada ya kuwa nae akaja kugundua huyu mama ni mke wa mtu ana watoto 3 ila haishi na mume mumewe anaishi dodoma kikazi.

Baada ya kugundua hayo mwanaume akamwambia kama umeolewa tuishie hapa maana me nataka niwe na mtu ambaye nitakuwa na malengo naye.

Bi mkubwa akawa hataki kila jamaa akitafuta mwanamke mwingine mama yule anamwaribia jamaa anaachwa. Ikafikia wakati mama yule anamtisha kijana hadi kumuua na kwa kuwa yeye ni mkubwa kazini wakati mwingine anaanzisha visa huko kazini ili kumtisha kijana.

Kijana kapata gal mwingne keshamtambulisha kwao na wanapendana wana malengo ya kufunga ndoa ila bi mkubwa bado anamwaribia.

Kijana kaniomba ushauri je amripoti huyu mamma kwa menejiment ofisini au amtafute mume wa huyu dada amwambia ujinga anaomfanyia mkewe au aachane vipi na huyu mama. Mama kapagawa yupo radhi hata kuua ili asikose penz la huyo kijana

Ushauri wenu wakuu nitamshauri jamaa vzuri mkinipa mwongozo.
 
Naona akihatarisha ajira yake, unapoamua kuanzisha mahusiano Kazn na mwanamke aliyekuzidi cheo lazima ujue kuna hatari mbele! Akilazimisha atapigwa hata uhamisho aende chaka so chakufanya aendelee kumdinya tu kwa masharti! Akijaribu kwenda kwa mmewe ajue anatengeneza Bomu na akiripoti utawala wataangalia nani ana impact kazini, hapo ndio uhamisho utakapomuhusu unless awe tegemeo hapo kazini!

Sent using kidole gumba
 
Wakitangaza vita we andaa silaha. Kama yupo radhi kuua kwanini uyo jamaa asimuwai ??, Na kama hawezi atoe taarifa Kwanza Kwa wakubwa kisha Kwa mumewe af awe mkali na mwenye msimamo asifagilie ujinga ujinga wa uyo bi mkubwa.Yaani siku akimletea ujinga tena wa kumtishia ye amkate makofi ya kufa mtu ujinga ataacha.
 
Sasa Hapo Kuna Tatizo Kweli?
Jamaa Ampe Masharti Mama, Hoja Ije Wazae Kwanza Bila Kujari Kama Kaolewa Uone Mama Atakuwa Mpole

Mengine Hakuna Ushauri Ila Ajiongeze Kidogo
Elimu Siyo Cheti Ni Ujuzi
Mama kuna kipind alibeba mimba akamwambia dogo wamsingizie mumewe baadae akaichoropoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza mwambie mumewe ili asiuawe maana km yupo radhi kuuua atauwa mumewe ili uishi nae lkn pia chukua tahadhari washirikishe watu wazima hapo kazini wamwelekeze. Ht mpnz wako pia mwambie ukweli
 
Unafanya mchezo na wanawake wewe, kwa taarifa yako anaweza akakubali kuzaa nae na akambambikia mumewe huyo mtoto.
Sasa Hapo Kuna Tatizo Kweli?
Jamaa Ampe Masharti Mama, Hoja Ije Wazae Kwanza Bila Kujari Kama Kaolewa Uone Mama Atakuwa Mpole

Mengine Hakuna Ushauri Ila Ajiongeze Kidogo
Elimu Siyo Cheti Ni Ujuzi
Aachane nae tu ila azingatie kufanya kazi kwa weledi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akilazimisha sana mwambie amuombe tigo kila siku, sidhani kama atavumilia mkito huo.
 
Mwambie jamaa aendelee na mipango kma kawaida huyo ni wivu tu unamsumbua atafka mahal atazoea

Akiendelea kumsikiliza atamchelewesha
Sisi ndo tuna control wanawake na sio wanawake watucontrol sisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwambie huyo dogo aache utoto,
yeye akianzisha mahusiano mapya huyo mama anajuaje mpaka amuharibie??
 
Back
Top Bottom