Nimuoe dada yangu?

Sijaelewa hapo. Ina mana ulipokuwa sekondari uliweza kumfanyia mpango huyo mpenzi wako na kumsomesha? Au ni wazazi wako ndo waliwasomesha we na mpenzi wako? Ufafanuzi hapo plz mkuu!
 
Maisha ni yko na si ya dada!!!angalia moyo wako,mawifi ni kawaida yao,usipokuwa mwangalifu unaweza chukua hatua ambayo kimsingi siyo sahii kwa ajili ya dada!!!!Mke ni wako bwana jidai naye!!
 
Waite dadazako esp huyo anayependwa na wazazi mwambie umebadili nia sasa unata kumwoa yeye tena uwe serious akibisha mwambie basi ntamwoa huyo ambaye humtaki, wanawake wanambwembwe kweli kwenye kuingilia mapenzi ya ndugu zao
 
<br />
<br />
nimempeleka shule mwenyewe ili kupunguza gape la kielimu pia sikua na mpango wa kuoa baada ya kumpa mimba hivyo nilitaka aendelee jupunguza vidato katika safari ya kuelekea kuoana bahati nzuri ni mzima kichwani
Angalia sasa usimdandiedandie ukamjaza tena ukamharibia malengo yake ya kuongeza elimu ili apunguze gap kati yako naye.
 
Khaa sasa dada yako wa nini wakati tayari una mtu wako? angalia nafsi yako inavyokutuma kama umeridhia kuwa naye huyo mtu wako na unaona kwa uchunguzi wako anafaa basi endeleaaaaaaa
 
Khaa sasa dada yako wa nini wakati tayari una mtu wako? angalia nafsi yako inavyokutuma kama umeridhia kuwa naye huyo mtu wako na unaona kwa uchunguzi wako anafaa basi endeleaaaaaaa
Dada kwa maana anamuingilia sio amuoe yeye
 
kuna usemi wa kiingereza usemao ASK YOUR HEART BEFORE U TELL HIM/HER GOODBYE usemi huu unanipa wakati mgumu sana katika kufanya maamuzi magumu.Naombeni ushauri juu ya hili lifuatalo:mwaka 2005 niliingia kwny mahusiano na binti wa kihehe yaliyopelekea yeye kupata ujauzito baada ya miezi 5.2006 nijiunga kidato cha tano mbeya hadi 2008 nilipohimu f 6. Baadaye nilimfanyia mpango wa kurudia shule ambapo arudia drs7 na kufaulu vzr kwenda sekondary.2008 nilijiunga na chuo kikuu na hadi kufikia mwaka wa pili wa masomo mambo yalikua shwari.Baada ya hapo nilianza kupokea simu kutoka kwa dada zangu zikishusha tuhuma nzito zinazohusu wifi yao baada ya kurudi kutoka chuo nimefanya uchunguzi na kugundua si za kweli na zinalenga kutusambaratisha.Mmoja nikamtania juu ya adhima ya kubariki ndoa mwakani akasema nikimwoa atajing'ata kidole hadi kikatike ila wazazi wanamkubali sana kiasi cha kumlipia hata michango ya shule.Nifanye nn juu ya hawa

Naona tuna tofauti kubwa sana na wewe kwenye masuala ya mahusiano na nadhani ushauri wangu hauwezi kukusaidia. Kwa ufupi mimi sijawahi na sitawahi kujadiliani na dada zangu kuhusu masuala yangu ya mahusiano na jinsia inayofanana nao. Mila na desturi yangu hairuhusu kabisa hayo mambo.
 
Kwanza hongera kwa hatua ulizozichukua kufanikisha kwenda shule na kuendelea na masomo baada ya kujifungua.
Kuhusu tuhuma za dada yako: jaribu kuongea nae huenda kuna chuki binafsi au kuna jambo ambalo ameligundua na pindi utaongea nae kwa undani huenda akakueleza na wewe ulitafakari uone lina mashiko au ni wivu wa mawifi...huenda hawajapatana hivyo mbinu za kuhakikisha maelewano kati yanu yanakuwa mabovu, kama wazazi wanamkubali na hawajasema neno lolote hasi kuhusu huyu binti basi huyo dada yake analo lake binafsi kwa maslahi yake binafsi. huyu dada yako umewahi kumpa sapoti kwenye masomo au je yeye amefikia kiwango gani cha elimu? angalia upande wa pili wa shilingi....huenda hafurahishwi na ushirikiano anaopewa na wazazi wako/wenu wakati yeye dada hapewi.
 
Back
Top Bottom