Nimueleze mjomba wake?

Nimueleze mjomba wake?

maimatha

Senior Member
Joined
Mar 2, 2013
Posts
129
Reaction score
162
Natumai wazima wote.

Naomben mawazo yenu hasa wanawake mlioko kwenye ndoa
Mi nipo ndoan miez michache tu nimeolewa baada ya miez 2 akaja mtoto wa wifi yangu naishi nae hapa
Sasa Kuna vitabia anavyo ambavyo kweli kibinadamu vinanikwaza ila navumilia sababu najua tumetoka familia tofauti na tumelelewa malezi tofauti..

Vingi napotezea tu sababu najua may be utoto au!

Bint Anamika 25 tabia yake kubwa inayonikera nikuingia chumbani kwangu yeye anachumba chake lkn akiwa nashida anaingia tu haijalishi atanikutaje labda navaa wala hajali binafsi naona kitu Cha ajabu sababu tulivyokua chumba Cha baba na mama Cha kuheshim na tulikua tunaingia kwa emergency, nilimuita nikamwambia ukiwa na shida chumbani niambie au bisha hodi lkn haiajsaidia

2) tabia ya pil anafanya vitu anavyotaka yeye mfano akitaka kupika haulizi tunapika Nini anapika anavyojisikia na anavyotaka yeye unakuta hela niliyoachiwa ikiisha naulizwa Mimi nashindwa kumwambia mjomba ake napotezea tu.

Kila siku anakuja na marafiki wapya hata anitambulishi Wala siwajui napishanao tu naweza kutana na mtu jikon au chumbani kwake hata cjui Ni Nan serious nakosa Amani nashindwa nifanyeje

Kibaya mjomba wake anaamini huyu bint yuko parfect 100% hata akikosea anaogopa kumwambia so nashindwa nifanyeje
 
Bint Anamika 25 tabia yake kubwa inayonikera nikuingia chumbani kwangu yeye anachumba chake lkn akiwa nashida anaingia tu haijalishi atanikutaje labda navaa wala hajali binafsi naona kitu Cha ajabu sababu tulivyokua chumba Cha baba na mama Cha kuheshim na tulikua tunaingia kwa emergency, nilimuita nikamwambia ukiwa na shida chumbani niambie au bisha hodi lkn haiajsaidia
Miaka 25 ni mwanamke mwezio; sio binti huyo!! Kwa swala la kuingia chumbani kwako 1) Uwe unafunga mlango 2) Kama ulimuita ukamwambia na bado hasikii, kua mkali nae mama, mkaripie!! Usiruhusu mtu akuzoee namna hio. Ukianza kumchosha mumeo na maswala madogo kama hayo, yakikukuta makubwa atakua keshajichokea
 
Huyo hana adabu khabithi l'amali, mwanahizaya mkubwa aliekosa mafunzo. Mshenzi mmoja asiejua zuri wala baya, mmbwa koko aliekosa malezi ya wazazi wake.

Mwanamke kinyampera asiejijua msungo mkubwa. Uso umemparama mkosa soni mshenzi huyo.

Ndugu yangu nakusihi fanya juu chini umtimue hugo mbwa koko laa sivyo utakuja juta.
 
Aisee mkuu ukiamua unachamba kiasi hiki duh.
 
tabia ya pil anafanya vitu anavyotaka yeye mfano akitaka kupika haulizi tunapika Nini anapika anavyojisikia na anavyotaka yeye unakuta hela niliyoachiwa ikiisha naulizwa Mimi nashindwa kumwambia mjomba ake napotezea tu.... Kila siku anakuja na marafiki wapya hata anitambulishi Wala siwajui napishanao tu naweza kutana na mtu jikon au chumbani kwake hata cjui Ni Nan serious nakosa Amani nashindwa nifanyeje
Mwaaali! Mwaaaali!! Mtoto wa wifi yako ndio unamuachia hivyo? Akija mama yake (wifi yako) si ndio atakutawala kuliko maelezo. Hizo hela ukiachiwa na mumeo na wewe unazianika sio?? Hivi kwanza anaingiaje jikoni kwako as if ni nyumbani kwake??!! Unakosa amani nyumbani kwako mapema hii?? Hebu wacha masikhara
 
Huyu mtoa mada nae anaonekana kamzoesha mwenyewe chumba cha mumewe anaingiaje mtu mwengine bila taarifa,kuhusu swala la pesa anajuje inamaana akiachiwa pesa na mumewe ana mkabidhi huyo binti.
 
Hapo ni nyumbani kwako si kwake ni lazima akuheshimu. Unakosaje amani kwako? 😳Ongea naye kwa kituo na umueleze yote usiyoyapenda hutaki yaendelee kutokea hawezi afungashe virago haraka sana. Hawezi kufanya anayoyafanya nyumbani kwako. GANGAMARA!!
 
Huyo hana adabu khabithi l'amali, mwanahizaya mkubwa aliekosa mafunzo. Mshenzi mmoja asiejua zuri wala baya, mmbwa koko aliekosa malezi ya wazazi wake.

Mwanamke kinyampera asiejijua msungo mkubwa. Uso umemparama mkosa soni mshenzi huyo.

Ndugu yangu nakusihi fanya juu chini umtimue hugo mbwa koko laa sivyo utakuja juta.
Aisee..!

Acha niscreenshot kwa matumizi ya baadae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heeeey....kwani vipi Leo?
Huyo hana adabu khabithi l'amali, mwanahizaya mkubwa aliekosa mafunzo. Mshenzi mmoja asiejua zuri wala baya, mmbwa koko aliekosa malezi ya wazazi wake.

Mwanamke kinyampera asiejijua msungo mkubwa. Uso umemparama mkosa soni mshenzi huyo.

Ndugu yangu nakusihi fanya juu chini umtimue hugo mbwa koko laa sivyo utakuja juta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mtoa mada nae anaonekana kamzoesha mwenyewe chumba cha mumewe anaingiaje mtu mwengine bila taarifa,kuhusu swala la pesa anajuje inamaana akiachiwa pesa na mumewe ana mkabidhi huyo binti.
Wacha aendelee kumchekea, atavuna alichopanda. Kuna wale watani wangu mjomba na mtoto wa dada sio issue. Mungu amuepushe
 
Back
Top Bottom