Nimuachaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimuachaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by london1, Aug 30, 2011.

 1. l

  london1 JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2011
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 215
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 60
  Heloo wana jamii,nimekuja humu kuomba ushauri na busara zenu.Mie naishi ughaibuni na wife(mbongo pia) na watoto wawili, m/mungu kanijaalia kazi poa na elimu ya juu tatizo huyu mwenzangu hatuelewani yaani ni mbishani, mshindani, lawama kila siku, hana msaada hata wa mawazo, kutoa mambo ya ndani nje kwa saana. Nishagundua hatuwezi kuishi pamoja kwani sina raha.

  Tatizo siwezi kumwambia atoke kwani huku mwanamke hafukuzwi hata kama nyumba ya mwaname, sina pa kumpeleka na hata nikitaka kutoka itabidi niendelee kulipia hii nyumba na sina uwezo wa kulipia nyumba mbili pia nikimuachia nyumba anaweza kuleta mabwana wakati mi ndio mlipaji. Nimechanganyikiwa napenda wanangu na niko tayari kuwasupport kwa kila hali, lakini huyu mwanamke sina haja nae. Nifanyeje?

  Naomba ushauri
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kwani mkeo ni kabila gani na je mmefunga ndoa au mmesogezana hukohuko yaani mmeoana wote mkiwa nje?
   
 3. N

  Ndeonasiae Senior Member

  #3
  Aug 30, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wether wamesogezana au la, wat matters ni happiness, me naona amwambie black and white kwamba malove yamekwisha na hautaki usumbufu, ishini nyumba moja kila mtu na chumba chake mlee watoto na mkubaliane hakuna kusumbuana. open marriage.
   
 4. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ninaamini katika upendo, so bado mnayo nafasi katika nyumba yenu ya kuishi kwa furaha. Hatua ya kwanza, mwite mke wako mweleze yote ambayo huyapendi kwake, lakini ukitumia sauti ya upole na ya upendo. Naye mpe nafasi ajieleze tatizo ni nini mpaka amekuwa hivyo??!! naamini kila mmoja akidhamiria moyoni mwake kubadilika ktika yale ambayo mtakuwa mmekubaliana, mnaweza mkaiponya ndoa yenu! Na zaidi ya yote, mshirikishe Mungu katika ndoa yako. Mbarikiwe
   
 5. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  kaa nae chn muyazungumze
  pole sana.....yeye akwenda ata darasa moja kdg labda?
   
 6. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sio nimuachaje??? Ni nimuacheje??
   
 7. U

  Upanga Senior Member

  #7
  Aug 30, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Pole sana!hilo tatizo ni kubwa kdgo,cha msingi ni wote mkae na mjiuulize kwa nini mmefikia hapo,huenda ana maelezo mazuri na labda chanzo ukawa wewe,hivyo jishushe na umuelewe mwenzio then utaenda next step.
   
 8. Kadada

  Kadada Senior Member

  #8
  Aug 30, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 183
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Kabla ya yote hebu jiulize ubishani, ushindani na lawama zake zimeanza baada ya kuzaa naye hao watoto wawili au kabla ya kuzaa? ukishajua ndo utapata pa kuanzia.
   
 9. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #9
  Aug 30, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  rose hebu tunieni akili mnapomshauri mtu jambo mwanamke wa aina hii ni wa kukaa nae chini kweli?
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Pole sana mdau,,,,,hakuna sababu ya kujiuliza sana,,,,,,hebu zungumza nae mje mlee watoto hao
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  ukisha kumwoa huwezi kumwacha kwa sababu za utani utani kama hizo.........................sababu za kumwacha ni kama una ushahidi usiopingika kuwa ni mwasherati tu.............hayo mengine uliaapa kuwa utayavumilia.....................endelea kuyavumilia huku ukisali na kufunga.............ukishinda mtihani huo Muumba atakuzawadia maradufu sana................ukishindwa huo mtihani Muumba takutumia maadui zako ambao utawatumikia..........................sura zao zitakuwa murua lakini roho zao zitakufanya umkumbuke huyu ambaye umemtelekeza..........so put up and shut up as well..........................you are a man..............are you not?
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu mambo ya ndani ni ya kukaa na kuongea kwa pamoja
  Tumia muda wako tafuta sehem ambayo imetulia kaa nae muanze kuongea mambo yenu
  Bila kufokeana wala kulumbana na mweleze wazi kabisa kuwa umeenda pale mzungumze kama watu wazima na watu ambao mnapanga kuijenga familia yenu na watoto wenu
  Usikimbilie kuachana au kutengana maana hapo ni ubishani na kukutokukubaliana kimawazo na kimtazamo
   
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu mambo ya ndani ni ya kukaa na kuongea kwa pamoja <BR>Tumia muda wako tafuta sehem ambayo imetulia kaa nae muanze kuongea mambo yenu<BR>Bila kufokeana wala kulumbana na mweleze wazi kabisa kuwa umeenda pale mzungumze kama watu wazima na watu ambao mnapanga kuijenga familia yenu na watoto wenu<BR>Usikimbilie kuachana au kutengana maana hapo ni ubishani na kukutokukubaliana kimawazo na kimtazamo
   
 14. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  maji ushayavulia nguo lazima uyaoge...................
  NWY pole sana mkuu
  mvumilie!!!!!!!!!!!!!
   
 15. MASELE

  MASELE JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  bibila inasema mwanaume ni kichwa cha familia, muombe Mungu akufunulie zaidi na akuwezeshe kuchukuliana na mkeo usimruhusu shetani aharibu ndoa yako, funga na kuomba kwa kumaanisha; ila usahuri wa jinsi ngani mkeo utamuacha mimi siuungi mkono hata mara moja. angalia tatizo liko wapi kama mwanzo milikuwa mnaelewana vizuri tu iweje sasa. kitukingine epukana na ubabe na malumbano yasiyo ya lazima. kumbuka kila mtu mi wathamani sana mbele za Mungu na wewe umepewa huyo mke si kwa bahati mbaya, ila ni mpango wa Mungu aishie; Muombe mngu kaa na mkeo msali pamoja ma mzungumzie tofauti zenu, na baada ya hapo sahau yote yaliyopita jenga mji wako wewe na mkeo; bila kumuomba Mungu sisi hatuweze. omba kuongozwa na Yesu nakuambia hata kama utakuwa umelala njaa amani na furaha ndani yenu itatawala. usifikirie kumuacha mkeo hata kwa milisecond fikiria nijinsi ngani utafurahia upendo wenu wa mwazo
   
 16. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #16
  Aug 30, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Mkuu naamini umekuja kuyaona haya muda mrefu sana baada ya kuwa nae kwenye ndoa na watoto mmeshapata.
  Kama mlianza uhusiano na ukakomaa hadi ukaona anafaa kuwa mwenzi wako wa maisha,kwanini leo hii ugeuke ahadi yako na kuacha mapenzi uliyokuwa nayo juu yake?

  Kama alikuwa mwanamke mzuri hadi ukaamua kuoa huoni kuna sababu zilizomfanya abadilike na kuwa na tabia hizo uonazo hazifai? umejaribu tafakari kwanini anatoa mambo ya ndani ya nyumba? inawezekana hushauriki na huambiliki ndio maana anaamua kushauriana na rafiki na dugu zake.

  Nakushauri ujichunguze vyema na ujue sababu zilizopelekea yeye kubadilika...maana naamini binadamu yoyote anaweza badilika kama ataona hathiminiwi.

  Amini nakuambia kuachana nae sio suluhisho ila ni mwanzo wa matatizo mengi sana na watakao umia ni watoto wenu.

  Tafakari chukua hatua.
   
 17. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mimi nafikiri kama mlifuata taratibu za ndoa za kiafrika, kuna mshenga wazazi nk.Tatizo lenu lazima kwanza lifike huko na kama watakosa majibu ya matatizo yenu ndo sasa uhamuzi uwe wako maana kama wote wameshindwa kutatua hayo matatizo yenu basi tena.

  Maana hao watasikiliza pande zote mbili kuliko wewe kusema upande wako na hatujui upande wa pili kuna nini: Yawezekana wewe unashida au yeye anashida kwa hiyo kukushauri itakuwa ngumu sana bila kupata maelezo kutoka upande wa pili.Byeee
   
 18. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  London1,binafsi sina la kuongeza,wengi walioongea hapo juu wamenikausha mdomo maana waliyokushauri ni mazito,jaribu kuyasoma mara mbili mbili na ujitahidi kuyatekeleza.Yote kwa yote kumbuka you are responsible not only for your childreans welfare but also for their happiness maana wao hawakutuma application ya kuja duniani badala yake starehe yako na mkeo ndo iliwaleta duniani,usiwakwaze bila sababu ya msingi( kama kifo wakawa orphaned).
   
 19. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,726
  Likes Received: 447
  Trophy Points: 180
  Kimsingi naamini awali mlikuwa mnapendana sana na ndio maana mkafikia hatua ya kuona. But after your marriage na kupata watoto yameanza matatizo. Inabidi ukae utafakari ni nini chanzo, wapi pana tatizo,kwa nini ni mbishi, hapo awali ulikuwa unamtreat vp, kwa sasa unamtreat vp, mnapokuwa na matatizo au mmekwaruzana majibizano yenu yanakuwa ya namna gani,nani napanda juu zaidi mafarakano yanapotokea,mwenendo wako katika ndoa ukoje,wake je upoje,je huwa unafanya maombi ya kuiombea ndoa yenu?

  Ushirikishwaji wa Mungu katika matatizo yenu upo au mnaenda kibinada binadamu? Baada ya kuyatafakari hayo atleast utakuwa una majibu uanzie wapi. Pia tafuta muda maalumu, mtoke out sehemu iliyotulia,kaeni chini elezaneni kwa upole jinsi unavyojisikia kwa sasa kutokana na migongano iliyopo sasa katika ndoa yenu,kisha ombaneni msamaha muanze upya. MUNGU AWABARIKI SANA. POLE!
   
 20. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  Mwl wa kiswahili
   
Loading...