Ndio shida ya kuomba ushauri kwa watu, binadamu tumeumbwa na moyo wa huruma. Naona karibu wote wamekushauri ubaki na D sababu ya huruma ambayo binadamu kaumbwa nayo bila kuangalia furaha yako
Nikwambie kitu kimoja na pengine hata wengine pia wakitilie maanani, mambo yote tunayofanya katika kupambana na maisha mwisho wa siku jambo la msingi ni "kuwa na furaha". Katika kuifikia hiyo furaha lazima upitie magumu hivyo Mimi sioni sababu ya kuogopa wewe kumuacha D na kuwa na M sababu M Ndio furaha yako, ukija kubwagwa na M sababu ya masikitiko ya D Hiyo ni sehemu ya mapito ya kufikia kwenye furaha yako.
Achana na mambo ya karma sijui masikito furaha yako Ndio kitu cha kwanza. Muache D kwa amani aende zake kamata M upate furaha.
NB: Ukiendelea na D utamuumiza zaidi kuliko ukimuacha sababu moyo wako na fikira zako zimesha hama hazipo tena kwake hivyo utaishia kumtesa tu