Nimuachaje D?

Nimuachaje D?

Carlssin

Member
Joined
Oct 22, 2017
Posts
44
Reaction score
70
Greetings!

Nina-date wasichana wawili, lakini mmoja(let me call her M) nampenda sana kuliko mwingine (let me call her D). Japokuwa D ndio nilianza kuwa naye kabla ya M, sipo tayari kumpoteza M kabisa, na pia sitaki kuwa-date wote wawili at a time. Kwa sababu za kimazingira... kuna hatari kubwa ya M kuja kugundua kuwa nina mahusiano na mtu mwingine, na hilo litakuwa ni doa kubwa sana ambalo I'm pretty sure! ndio utakuwa mwisho wetu, me and M.


Kabla ya D

Sikuwa na msichana ninaye-date naye, na sikuwa nahitaji mahusiano kabisa huo wakati. Nilifahamiana naye kama rafiki na pia jirani yangu. Mazoea yazidi pale nilipogundua kuwa ni shabiki mwenzangu wa Real Madrid na Man Utd, tulikuwa na mengi ya kuzungumza tulipopata wasaa wa kuwa pamoja. Mazoea yalizidi mara dufu kiasi kwamba tukawa tunachat hadi usiku wa manane. (To recap the story) Tuliishia kuwa wapenzi bila hata kumtongoza.


Me && D

Kama kwa ufupi nilivyowasimulia mazingira yaliyotuingiza kwenye mahusiano, D baada ya kuwa na mimi, aliniona mimi ndiye ninayemfaa na akaamua ku-break up na boyfriend wake (kwa mujibu wake: alidai kuwa uhusiano wao ulikuwa unayumba sana wakati huo). Tofauti na nilivyomtarajia, hajawahi kuniomba pesa hata ya vocha, lakini nikiona anauhitaji, na kama ninayo, huwa namtumia na huwa anashukuru sana. Pili, huwa anajitahidi sana kuwa honest and faithful kwangu. Kiufupi, D amekuwa msichana mwema kwangu, na tuna mwaka sasa hatujawahi kugombana kabisa katika huu uhusiano wetu. D anatumaini kubwa sana la kuja kuolewa na mimi hapo baadae. Tofauti na D, deep down my heart, mimi sipo serious kwenye haya mahusiano kama ilivyo kwa upande wake.


Me && M

Nikiwa nina-date na D... M, fully won my attention, nilijitoa kwa kila kitu kuhakikisha namuweka kwenye ngome yangu, nilimtongoza almost mwezi mzima kabla ya kunikubalia. Ana sifa zote mbili za D ( nilizotaja aya ya hapo juu ), na ana sifa za ziada pia. Tatu, M, ni mcha Mungu sana huyu binti na ana upendo sana kwa watu hata asiowajua. Nne, she is so intelligent enough to challenge me frequently. Fifthy and last, uzuri wa muonekano wake ni zaidi ya D. She kills me in all angles. All in all, me & M, tunaishi vizuri sana, tuna malengo makubwa sana, na baadhi tushaanza kuyatekeleza.


My Problem

Kwa hali iliyopo sasa, D ni msichana ambaye kiukweli anahitaji mwanaume ambaye yupo tayari kuwa naye kwa malengo ya muda mrefu, anahitaji kupendwa sana, maana ni aina ya wale wasichana ambao kwa sasa wanazidi kutoweka hapa nchini. Lakini mimi nimependa kwingine na sitaki kumpotezea muda wake akiwa anategemea kuja kuishi na mimi hapo baadae.

Tangu nilipoingia uhusiano na M, nimekuwa nikisubiri sana D anikosee kosa lolote dogo, ili iwe nafasi ya kuachana naye, lakini wapi! hakuna anachonikosea. Unfortunately, huwa nakosa ule moyo wakumuacha ghafla bin vuu, maana najua madhara yatakuwa ni makubwa sana kwa upande wake, may be na mimi pia.

Nataka hili tatizo litatuke haraka sana, kabla M hajagundua, sitaki liende taratibu maana naweza kumkosa ninayempenda sana, maana muda unavyozidi kwenda ndio naona ukuta unaotenganisha haya mahusiano mawili unazidi kubomoka.

Nimuachaje D?


Asante kwa kuvumilia taaluma yangu dogo ya uandishi.
 
Mkuu kwa jinsi huyo D wako alivyokupenda na kujinyenyekeza na kuwa na matumaini makubwa ya wewe kumwoa na kuanzisha familia yenu nk nk halafu uje umwache simply because she's not as intelligent as M,her beauty is not as good as that of M?

Halafu huyo M umesema ni mcha Mungu na hajui kuwa uko na D,sasa whenever you break up relationship with D mkuu ujiandae kwa msiba na hapohapo ujue M atajua na atajua kwamba wewe ulimfanya yeye awe sababu ya kifo cha D hivyo hatoona sababu ya kuendelea kuishi na wewe.
Na utakapo wapoteza hao wawili kwa style tofauti mzimu wa D utakutesa maisha yako yoteee na hautabaki salama.

Chakufanya hapo ni kumwacha M kwakuwa amemkuta D na hili litayaokoa maisha ya D na ya kwako pia.

Wanaume sometimes tuwe na huruma jamani.
 
Mkuu kwa jinsi huyo D wako alivyokupenda na kujinyenyekeza na kuwa na matumaini makubwa ya wewe kumwoa na kuanzisha familia yenu nk nk halafu uje umwache simply because she's not as intelligent as M,her beauty is not as good as that of M?

Halafu huyo M umesema ni mcha Mungu na hajui kuwa uko na D,sasa whenever you break up relationship with D mkuu ujiandae kwa msiba na hapohapo ujue M atajua na atajua kwamba wewe ulimfanya yeye awe sababu ya kifo cha D hivyo hatoona sababu ya kuendelea kuishi na wewe.
Na utakapo wapoteza hao wawili kwa style tofauti mzimu wa D utakutesa maisha yako yoteee na hautabaki salama.

Chakufanya hapo ni kumwacha M kwakuwa amemkuta D na hili litayaokoa maisha ya D na ya kwako pia.

Wanaume sometimes tuwe na huruma jamani.
His feelings are on M,

Nilikuwa na jirani yangu mwanaume handsome, mcha Mungu, msafi, yai lake kama la Oxford Kwa kweli nilimpenda lakini yeye hakuwa na feelings na mimi ki- vile lakini alitaka tu ngonoke. I refused to let my self that low.
Nilifanikiwa kumpata mtu ambae alikuwa serious. That is what I needed. Relationship ikipokuwa strong sasa ninakutana na jirani nikamfahamisha mchumba. I could feel his discomfort.

Baadae aliniomba nimfikirie kwani muda huo na yeye anataka kusettle down. 💃🏾 I was gone
 
His feelings are on M,

Nilikuwa na jirani yangu mwanaume handsome, mcha Mungu, msafi, yai lake kama la Oxford Kwa kweli nilimpenda lakini yeye hakuwa na feelings na mimi ki- vile lakini alitaka tu ngonoke. I refused to let my self that low.
Nilifanikiwa kumpata mtu ambae alikuwa serious. That is what I needed. Relationship ilipijuwa strong sasa ninakutana na jirani nikamfahamisha mchumba. I could feel his discomfort.

Baadae aliniomba nimfikirie kwani muda huo na yeye anataka kusettle down. 💃🏾 I was gone
Great people do not sell themselves cheap.... I can feel his frustration.
All the best mkuu.
 
Katika mizania yangu, nikikupima wewe mleta mada, naridhika ubaki na D na kumwacha mara moja M.
Ninaamini D Ana thamani kubwa sana kwako kuliko M. D anakupa kile alichonacho Bila kuacha chembe ya Shaka nyuma yake. Alikuthamini na kukupa uzito wa pekee. Tofauti na M.
Spirit aliyo nayo D kwako huweI kuipata kwa M. Na maumivu atakayopata D akiachwa yatakurudia kwa M.
 
Nilitaka nikushauri lakini uliposema tu kuwa wewe na D ni mashabiki wa Manyumbu United. Ushauri wangu nikausitisha.

Mwambie D kama yupo tayari kuhamia Liverpool nimchukue mimi.
Unaweza kuhana kabila, unaweza kuachana na mpenzi wako lakini si mapenzi ya timu uipendayo
 
Ngoja nikwambie kitu kaka Mungu fundi sana kinachokusumbua kwa sasa ni tamaa tu frust me. Hapo mke ni D na kwakweli umefanikiwa kutueleza hadi udhaifu wa D ika hujadiriki hata kidogo kutuambia udhaifu wa M. Ninauzoefu na hizi mishe M atakumwaga machozi na hutakaa uamini na utakavyo piga u-turn kurejea kwa D utakuwa usgachelewa sana na utakosa bara na pwani. Nenda kwenye maharusi katizame wanawake wanaoolewa they are very sasa wewe unataka wa kukuchallenge subili. Wanawake warembo sana ni mtego unaowamaliza majank wengi na wewe unataka kuwaonesha wana wa kitaa kuwa unajua kuchagua poa sisi watazamaji hatuna neno.
Ni mimi kaka wa D
 
Changamoto ya mahusiano ni hatari sana,maana ndio inayoathiri mfumo mzima wa maisha.

Watu wanapoteza maisha kwa kujiua ama kuuawa,wanajeruhiwa,wanakuwa vichaa,walevi wa kupindukia kisa katendwa na aliyempenda,aliyemjali,aliemthamini,aliyejitoa kwake na kumwamini kuliko kawaida.
Yaaani haya mambo yananoga uyasikie tuu kwenye mitandao kama hivi watu wakiomba ushauri,.lakini yasikukute,.
 
Back
Top Bottom