'Nimshaurije jamani' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Nimshaurije jamani'

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by TrueLove, Apr 24, 2012.

 1. T

  TrueLove Senior Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 124
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Habari za Hasubuhi 'The Great Thinkers'

  Naomba kuwasilisha mada hii ili niweze kupata ushauri mzuri wa kumpa Rafiki yangu ili aweze ku MOVE ON.

  Anaitwa Anitha (Sio jina Halisi), Anitha ni msichana alieajiriwa anajuhudi sana katika kazi, Anitha amepata mpenzi ambaye hawana muda mrefu sana, ila kama tunavyofaham wengi wetu hupenda mahusiano yenye faida, nikimaanisha baada ya mahusiano hayo ni nini kinafuata.

  Anitha alikutana na kijana mmoja anaeitwa Benson (Jina sio halisi) walikutana katika ofisi ya Anitha, Benson akampenda Anitha kwa muda aliokuwa katika Taasisi hiyo. Benson alikuja kikazi katika ofisi za akina Anitha na kumaliza program yao na kurudi katika ofisi yake.

  Benson alimueleza Anitha hisia alizonazo juu yake, na akamuomba Anitha ikiwezekana waweze kupanga maisha pamoja, Anitha nae hakusita kumpa Benson mawasiliano wakaendelea kuwasiliana, Walipoonana kwa mara nyingine wakaweka mambo yao sawa na wakaanza urafiki.

  Benson & Anitha walipeana Love Background, na hatimae wakaridhia kuwa pamoja, swali la kushangaza Anitha alimuuliza Benson kama ana mtoto Benson akamjibu hana, katika maendelezo ya mapenzi yao Anitha akaingia kwenye Profile ya Benson FB akaona picha ya mtoto kati ya picha za Benson.

  Anitha akampigia Benson simu na kumuuliza juu ya ile picha, Benson akakiri na kumwambia Anitha anaomba amsikilize kwa makini na amuelewe kile atakacho mwambia, Benson akamwambia Anitha ni kweli ana mtoto, na aliona ni mapema sana kumueleza ukweli kwani ndo kwanza mapenzi yao yanaanza hakutaka kumpoteza mpenzi wake huyo, Benson akamuomba Anitha amsamehe kwa kutokumuambia ukweli ial alizaa na mwanadada aliemsimulia wakati wanapeana Love background, Benson akamsisitiza kuwa anampenda sana Anitha na anaomba waendelee na mapenzi yao kwani yy Benson anampango wa kuish na Anitha.

  Swali kwa Anitha, je Benson ni kweli atakuwa anampenda? au ni walewale wanaotaka kumchezea hisia zake? na je amsamehe na waendelee na mapenzi yao? au afanyeje ila yy Anitha anampenda Benson, ameniomba ushauri mm nimeshindwa nimshauri nini, ila nimemwambia ntampa jibu baadae.

  Karibuni kwa ushauri unaojenga Jamii.

  Asanteni sana wana JF.
   
 2. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mwambie mwanaume kuzaa nje ni sifa sio aibu, mwanamke kuzaa nje ndo aibu.

  BTW; Ange kuwa Anitha dada yangu ningemuambia asirukie wanaume waongo, mana mtu muongo hawachi uwongo na mkweli hawachi ukweli.

  Mtu anaye kataa hana mtoto ambaye ni damu yake hata kama ni kwa joke afu akaja sema ukweli...atabakia kuwa muongo tu, kesho anaweza kukataa kama ana mke.
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Mimi wa kwangu ana watoto 2 tena nipo nao now
  TUNACHOANGALIA NI MAPENZI YA KWELI
  NA hiv free generation
   
 4. Geofrey_GAMS

  Geofrey_GAMS JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 564
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  its a vry difficult situation,
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  kuwa na mtoto si tatizo, ila kinachonitatiza ni kutokuwa muwazi tokea mwanzo....nina mashaka ni mangapi aliyomficha? ipo siku atasikia ana mke....
   
 6. Siri Sirini

  Siri Sirini JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 547
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Anaweza kuwa mkweli, me wa kwangu nilimuuliza kama ana mtoto akasema hana, baada ya miezi6 ya mahusiano nikagundua ana watoto 2, ila hakuweza kuoana na mzazi mwenzie kutokana na tofauti ya dini, na asa hv ni mme wangu 2na watoto 3.
  We mwambie asiwe na wasiwasi, kama amemuhakikishia kumpenda yeye anitha, ila mawasiliano na huyo mzazi mwenzake yawe ni kwa ajili ya mtoto, kumpelekea hela nk, na kama watafanikiwa kufunga ndoa amchukue mtoto ili wakate mawasiliano na mama mtoto
   
 7. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mpk umsingizie anita?
  asi useme tu jaman yamenikuta..nishaurin...

  mtoto anazuia nin?
  asi ushajua sasa umuache ili iweje?
  chek parameter nyngne za mapenz znasemaje lakin kw aili et nimemshtukia ana mtoto ndo anipend mhh....aulabda nawe aumpend?

  ashakupa sababu niliogopa kukwambia mapema...sasa unatakaje?
   
 8. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Wakati wa kuanzisha mahusiano, kuna mambo mengine ukiyaweka wazi mapema yanaweza kuvunja mahusiano. Nafikiri na hilo pia ni mojawapo. Jambo kama hilo huwekwa wazi baada ya kuzoeana na kufahamiana vizuri. Lakini pia ni muhimu kufanya uchunguzi zaidi wa kujua mwenendo wake kama ni muongo kwa asili au ni kwa hili tu kwa sababu maalum aliyeitoa na hapo utaweza kufanya maamuzi sahihi.
   
 9. T

  TrueLove Senior Member

  #9
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 124
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Okay nimekupata Smile, nitafikisha hii.
   
 10. T

  TrueLove Senior Member

  #10
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 124
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Thanx HorsePower. Hii imekaa vizuri kaka.

   
 11. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  I second that, once someone lies to you they will always lie :A S shade:
   
 12. T

  TrueLove Senior Member

  #12
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 124
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asante sana Kijino... hii itampa Faraja zaidi.


   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  True Love,

  Mwambie Anitha aende mdogo mdogo...Akiwa sober basi ataweza kukutana na mengine. Hili alichukulie kama test yake ya kwanza. Zikifika 3 au zaidi atakuwa amemuelewa vizuri Benson.

  Pia mweleze Anitha kuwa, hakuna binadamu asiye na doa, hata yeye analo (may be siyo mtoto ila laweza kuwa weakness nyingine)....!!


  Babu DC!!
   
 14. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Mtoto ni baraka,kama kweli anampenda anatakiwa tu kuhakikisha kama Benson na mzazi mwenzie mapenzi yalifika mwisho kweli au bado wanaendeleza kwa siri??kama alishaachana na mzazi mwenzie sioni cha ajabu hapo..
   
 15. WaliNazi

  WaliNazi JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 853
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  ....sema limekufikia...
   
 16. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #16
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mara nyingi wanawake kwa waume hua tunakua na list ya vitu ambavo wavitaka kwa mwenza na vile ambavo hutaki. Mara nyingi sana both sides hukimbizwa na mtu mwenye m/watoto kama one of the number one disqualifier! Hivo siwezi mlaumu Benson kwa hilo... sometimes ukweli ni muhimu ila una wakati wake.

  If anything Anitha inabidi afurahi kuweza tambua hilo haraka... atulie na aangalie the positive side of things. Kitendo cha Benson kuweka picha ya mtoto wake ambae kazaa tu huko na wala hawajaoana na huyo mamake ni wazi kua ni good dad na possibility kua yupo responsible kwa mwanae ni kubwa. Na Lingine Anitha inabidi ajue ni kua somehow yawezekana Benson alishindwa kabisa mwambia face to face lakini alitaka ajue (yeye Anitha); for kama aliweka FB na ajua wazi she accesses his account ni lazima angekua curious na kutaka kujua.

  Kingine cha muhimu cha kuzingatia ni matendo yake baada ya kutoa hio habari, Mapenzi yataendelea kama mwanzo? kama tu ataanza kulega baada ya hio habari then ina maan kafanya makusudi. Na kwamba sababu kisha pata alichotaka kwa Anitha (maybe kulala nae); anatafuta means za kuhakikisha Anitha mwenyewe anaaga kua hamtaki tena badala ya yeye Benson kusema tu Ukweli kua hamtaki tena Anitha.

  BTW unapokutana na Mwanaume yupo late 20s ama early 30s and onwards na akadai hana mtoto hata wakusingiziwa.... Kwangu personally inaweza amsha maswali mengine lukuki....
   
 17. T

  TrueLove Senior Member

  #17
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 124
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hili nalo ni jambo zuri sana, thats y tunaipenda JF coz imejaa Great Thinkers, asante sana.


   
 18. T

  TrueLove Senior Member

  #18
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 124
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Haya limenifikia lol.

   
 19. Ndetirima

  Ndetirima JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  Mwambie Anitha asikurupuke aendelee kufanya uchunguzi na kumfahamu vizuri mwenzake, huwezijua labda ana Mke kabisa na familia yake inajua mwisho wa siku asijekuonekana ameingilia ndoa ya watu. Muongo ni muongo tu, mapenzi yasimfanye kujisahau kumchunguza vizuri ili kumjua kabisa ni muhimu sana.
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mhhhh, mbona unanitisha AshaDii?

  Nawafahamu wengi tu including Babu DC ambao hawakuwahi si kuwa na mtoto bali hata kuelezwa kumpa mimba dada yeyote!!

  Una maana ungepiga chini mzee wa watu?

  Mengine uliyosema ni mswano duh!!

  Babu DC!!
   
Loading...