Nimshauri Vipi wana JF..!

Nimshauri Vipi wana JF..!

jambo1

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2009
Posts
241
Reaction score
29
Heshima kwenu wakuu..!
Kuna Dada mmoja huko Mwanza amenidokeza anataka kuachana na mumewe kwani mumewe kampa mimba mwanamke wa nje.
Ni long Story but kwa kifupi ni kwamba yule mke wa jamaa anamatatizo ya kutopata mtoto and wameenda kwa wataalamu wakashauriwa na mke akapewa dawa and baada ya muda mfupi angeweza kushika mimba..!
But Mwanamume akaona kama vile anachelewa so akaamua kumtia mimba mwananmke wa nje.
Sasa Mkewe kakasirika and now anataka kuvunja ndoa na kuondoka..,japokuwa mumewe amekiri na ameomba radhi..!
Nimpe ushauri gani maana amaidokeza kwa kifupi and badae natarajia nimpigie simu kumshauri..je wadau nimmpe ushauri gani..!?
Heshima kwenu wakuu..!
 
Mwambie asiachane nae. Kwani yeye hana kosa. Atakae pata lifetime punishment ni mume wake. (punishment will be increasing as the chird grows)
 
ataachana na wangapi? avumilie tu. hizo ndio changamoto za maisha ya ndoa
 
Namshauri asiachane na hiyo ndoa kwa sababu:

1.0 Kama Mungu akimjalia kupata mtoto atakuwa na jeuri ya kuthibitisha kwa mumewe kuwa ni kosa lake la kutokuwa na subira tu.

2.0 Kama akikosa basi akubali kumlea huyo mtoto kama mumewe hamnyanyasi na maisha yasonge.

Swali la mwisho ndoa yao ina muda gani toka wafunge ndoa????
 
..ni karibu miaka minne hivi..!
 
mwambie aweke furaha yake mbele....kama anafurahia hiyo ndoa abakie,kama hana furaha asepe
..shida ni kwamba anaona kama mumewe alifanya ili ajaribu aone kama yeye ni mzima and tatizo libaki kwa mkewe and anaona kama mumewe alitumia udhaifu wake kutoka nje ya ndoa..!
 
mhm!! ninachoelewa mie ni kwamba sababu ya pekee ya kuruhusu wanandoa kuachana ni kama mmoja wao amemega/megwa nje ya ndoa takatifu. sasa kwa kuwa hilo limetokea hapa. basi ni vyema kabisa huyo maa akapaki vilago vyake na hatakuwa na lawama yoyote.

pili ni kwamba lazima ajiulize je ataweza lea mtoto wa mwengine au kushare huyo mzee? na tatu hapa jamaa kashavunja trust na hilo ni jambo gumu sana kulirudisha. so ya nini uendelee kuwa mfungwa katika ndoa yako kila siku ukiwa umejaa wasiwasi kuwa labda jamaa ana mahusiano na mwanamke fulani. paki vilago count ur losses early
 
Ni kweli inaumiza na inahitaji umakini kushauri watu ambao hujui kwa nini walipendana
::
Wasiachane maana kukimbia tatizo kunaweza kumfanya akutane na tatizo jingine ambalo litatofautiana jina ila litafanana maumivu.
::
Amsamehe,,kwani msamaha ni daraja ambalo kila mwanadam atalihitaji kulipitia ili aendelee na mapito mengine yanayomsubiri.
::
Hakuna ndoa rahisi na kuendelea kulea mtoto asie wake ni maumivu ya kila wakati,LAKINI utulivu wake unaweza kumbadili mume wake.
=
 
Wala asimuache. Kama issue ni kuproove a point, na yeye atafute kidumu cha maana, apime hiv nacho na yeye aanze zoezi. Huenda naye akapata basi.

Ndoa haihitaji ubinafsi. Huyo mwanaume ni mbinafsi. Dawa ya mwenza m'binafsi ni kuwa m'binafsi zaidi yake. Tena hata akimgundua kabla nae si ataomba radhi tu na kukiri? Ndoa za siku hizi unafanya makusudi afu unasubiria kuomba radhi na kukiri ili ifute kosa lote, as if mwenza ni damy ya mwanakondoo. Kha!
 
Mwanzaaa kunani paleee? Asimwache ila naye atafute kidume cha ukwel kuneutralise maumivu then life lisonge....
 
niwambieni kitu Ciello na King'asti hakuna maumivu ya nafsi kama kucheat kwa sababu mumeo au mkeo amecheat!
raha yake inaisha the moment mwanaume anashuka kifuani kwako au mwanamke anavaa pichu yake!kucheat uamue tu kwa nenge zako lakini kwa kulipa kisasi?uwwwwhih!wala hupati ile amani au furaha uliyoamini ukicheat utaisikia baada ya tendo!
 
Last edited by a moderator:
Mamito mie bila kuneutralise nitaweka kisasi moyon so kutoa maumivu ni kupigacounter cheating tena afumanie kabisa then tukae meza moja tuzungumze kidiplomasia....

ive been there sweetie!
so nielewe tu na hili muulize mtu yeyote mwenye kujifunza na kuruhusu wengine wajifunze kupitia makosa yake!
 
Nimekuelewa na wala sikupingi, bt wengine bila kutoa maumivu nje aseee mambo hayaendi
ive been there sweetie!
so nielewe tu na hili muulize mtu yeyote mwenye kujifunza na kuruhusu wengine wajifunze kupitia makosa yake!
 
me nakushauri usiachane naye kua mvumilivu na mjalinbu 2 kushauriana itakuaje baada ya majibu ya wataalam mlio pewa itakuaje kwani ndoa yaitaji uvumilivu mamaa ook
 
Back
Top Bottom