Nimsaidieje?

sweetdada

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
517
169
Habari Wapendwa.

Nahitaji jinsi ya kumwambia huyu binti ili aelewe lakini sijui nitamwambiaje?msaada tafadhali.

Yuko kwenye ndoa anatimiza mwaka wa tatu sasa.ila kabla alikuwa akiishi na huyo mume..mume anarudi home saa saba nane hadi kumi na moja..mdada akihoji anapigwa,au jamaa anavunja glass kama tano eti kakasirika hataki kuulizwa.

mara akambamba jamaa anahadithia wenzake jinsi alivyotoka na mwanamke mwingine ila alishindwa kwenda nae faragha mana wife angestukia,alivyomhoji mwanaume akasema ooh nilikuwa nafurahisha umati.

baada ya muda harusi ikafanyika,mara binti mjamzito..bado mwanaume anarudi usiku mkubwa akiulizwa ni kipigo,siku hiyo mimba ya miezi saba anapigwa mpaka ilibidi aende hospitali kesho yake..na jamaa hakuomba msamaha,anasema tutaongea siku nyingine.
amekuwa akipigwa wee..mpaka nashindwa jinsi ya kumshauri ..mara ya mwisho nikachoka kusikiliza the same story nikamwambia aondoke amwache huyo mume..jibu nililopewa lilinichosha "mdogo wangu ,ndoa kitu kingine.usisikie ya watu"..dah

sasa imefikia point hata akinihadithia nabaki kusema pole..Je nimsaidieje mtu wa hivi?
 
Dunia hii bado kuna watu wanapiga wake zao....
Aibu sana kupiga mke
Anakuwa amepata ulabu kidogo au yupo mkavu mkavu tu
 
Anakuwa amepata ulabu ..ila ni jeuri kiasi kwamba akiwa sobber akiambiwa waongee hataki..kwahiyo mwanamke anakufa kisabuni
keshamsemea kwao lakini haijasaidia
 
Huyo ni muhuni sasa hata akiwa soba hataki kuongea. ingekuwa akiwa na ulabu ndo noma ila sasa mambo mengine magumu hata kuingilia.
ila ndo yataka uvumilivu ila saa nyingine inakuwa ngumu
 
Huyo dada alianza kupigwa hata kabla ya ndoa, lakini akakubali kuolewa na vipigo vyake! Mwache mwenzio na ndoa yake!! Ningekuwa mimi ningemwambia asinisimulie tena, maana hakuna maana ya kusimulia!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Yani alionja kipondo kabla ya ndoa na bado akaingia??Kaaazi kweli kweli!Mwenzako karidhika we unahangaika!Angalia usije ukaambiwa unamwonea wivu tu!Waache na ndoa yao...siku akitaka ushauri atautafuta mwenyewe!
 
Mie mwanaume hanipigi aisee kama hunitaki si uachane na mimi kwani lazima kuishi na wewe eti UNIPIGE?? Kwanza anaanzaje kunyoosha hicho kimkono chake?? Ashindwe na alegee
 
ndo wasiwasi wangu huo..anaweza kusema 'oo wivu na wewe olewa'..ndo mana siku hizi inabidi niseme tu polee..ila anatia huruma mana huwa anavimba macho mara masikio hata kazini anashindwa kwenda
 
Mie mwanaume hanipigi aisee kama hunitaki si uachane na mimi kwani lazima kuishi na wewe eti UNIPIGE?? Kwanza anaanzaje kunyoosha hicho kimkono chake?? Ashindwe na alegee

napenda hiyo DA,,yani msisitizo..hehehe
 
Huyo dada alianza kupigwa hata kabla ya ndoa, lakini akakubali kuolewa na vipigo vyake! Mwache mwenzio na ndoa yake!! Ningekuwa mimi ningemwambia asinisimulie tena, maana hakuna maana ya kusimulia!

Tatizo la dada zetu wanadhani kuna kubadilika! Sio rahisi kiivyo, nashauri akinadada msing'ang'anie kuolewa kabla hamjajiridhisha... Anamlilia nani sasa kama kunamtu alimlazimisha kuolewa amfuate akatoe malalamiko yake..
 
hilo jibu alilokupa ndilo linafaa.....ni kweli ndoa ni kitu kingine na usisikie ya watu...mimi sina cha kukusaidia maana huyo rafiki yako ameshakusaidia hata wewe namna ya kukaa mbali na ndoa yake lakini bado unataka kututumbukiza na sisi humo ndani.....

yakimshinda atatoka yeye mwenyewe.....
 
Kwa hakika ataishia kumuua au kumtia kilema.Wambie ndugu zake wa karibu maana likitokea la kutokea usije jilaumu kwamba kwa nini hukuwajulisha.Ujue dada wengine wana mikaka mishari kweli kweli wakisikia dada yao anabondwa wanaweza kumtia jamaa kibano asikisahau milele na huo ukawa mwisho wa kumpiga mkewe.
 
hilo jibu alilokupa ndilo linafaa.....ni kweli ndoa ni kitu kingine na usisikie ya watu...mimi sina cha kukusaidia maana huyo rafiki yako ameshakusaidia hata wewe namna ya kukaa mbali na ndoa yake lakini bado unataka kututumbukiza na sisi humo ndani.....

yakimshinda atatoka yeye mwenyewe.....

Kweli kabisa mambo ya ndoa tuwaachie wenyewe
 
Duh, ananipiga siku ya kwanza, navumilia,
Siku ya pili, nauliza umenioa uje kunipiga? Najua kwa ukorofi atanipiga tena.
Siku ya tatu, nashukuru kwa hiki kipigo kinanitosha kabisa, ngoja nitafute jinsi ya kukiepuka. Halafu ananipiga tena si nimemjibu, mwanaume hajibiwe haya.

Namuacha anaondoka, sehemu nitakayokanyaga wakati naondoka nahisi hapata ota majani tena.
Navumilia kipigo na mikono na miguu ninayo,
Kha hivi hakuna mke ***** eeh!!!
 
LD kuna ving'ang'anizi wew
 
Hii comment yako nzuri sana mdada nimejifunza kitu
 
Huyo dada alianza kupigwa hata kabla ya ndoa, lakini akakubali kuolewa na vipigo vyake! Mwache mwenzio na ndoa yake!! Ningekuwa mimi ningemwambia asinisimulie tena, maana hakuna maana ya kusimulia!

unakunywa kinywaji gani vile?
 
Back
Top Bottom