Njemba Soro.
JF-Expert Member
- Oct 5, 2013
- 3,246
- 5,757
Habari za muda.....
Nipo moshi kwa ajili ya sikukuu hizi ila kuna jambo nimeona niombe ushauri hapa na najua kuna watakaojifunza kitu hasa vijana.
Kuna rafiki yangu wa utotoni, shule ya msingi, sekondari na mpaka pilikapilika za maisha tulianza wote.
Tulianza na biashara ya magadi, tunatoka kijijini kwetu tunaenda kule wanaita Rongoi tunachimba magadi tunakuja kuuza kijijini, baadaye tukaanza biashara ya malimao
Tunakusanya malimao mitaani halafu tunapelEKa soko la mbuyuni tunauza bei ya jumla kwa wanaoleta dar.
Tukakuza mtaji tukaingia kwenye biashara ya mpunga, tukaenda chekereni na mabogini tukapata faida sna kwenye hiyo biashara ya mpunga na maana ni biashara ya msimu ikabidi tubadilishe biashara.
HAPA SASA JAMAA AKAKURUPUKA. Mimi niliingia kwenye biashara ya matunda, nikawa nasafirisha mafenesi, mapapai, na maembe kulingana na msimu kutoka Moshi kwenda Dar, au Mombasa, au Nairobi.
Jamaa yeye akaniambia anakuja dar kupambana na ukawa mwisho wa kuonana naye na simu ilifika kipindi hatukuwasiliana tena.
Sasa juzi nimekuja Moshi jamaa nimemkuta anakula ugoro, mbege, sigara na kila pombe jamaa anabugia. Jamaa amezeeka sana na amechoka.
Ndugu yake ananieleza jamaa alifilisiwa na wanawake wa dar pamoja na waganga wa kienyeji......
Huyu jamaa analazimisha sana nirudi naye dar lakini sioni kama ana namna tena ya kujirekebisha hasa ukizingatia naogopa sana ushirikina na ulevi. Hata yeye nikiongea naye mambo mengi anazungumzia ushirikina na anapenda sana huo ujinga.
NIMSAIDIEJE HUYU JAMAA???
1-Nimpe mtaji abaki moshi?
2-Nikubali kuja naye dar....
3-NIACHANE NAYE TU.
Naombeni ushauri....