Nilivyotaka kumuua ndugu yangu

Nilivyotaka kumuua ndugu yangu

kiroka

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2018
Posts
407
Reaction score
1,945
Ndio nilitaka kumuu ndugu yangu, maisha yetu tulizaliwa kijijini mzee alifariki miaka mingi iliyopita. Bro alitangulia mjini kutafte pesa kweli akafanikiwa akanibeba nikaja mjini akaniweka kwenye biashara moja niwe msimamizi, biashara ikaenda vizuri sana ikawa inasomesha watoto shule nzuri nzuri apa mjini na kusaidia ndugu wengine kijijini na biashara hii niliianzisha mimi nilimkuta akiwa na wazo na mtaji kiasi nilipambn mtaji ukakua mambo yakawa super

Kimbembe kikatokea bro akasingiziwa kesi ya mauaji akakamatwa apo ndo sekeseke nilivoanzia. Kwanza mtu aliea uawa brother hamfahamu kwa sura kisa tu eti rafiki yake bro alikua na ugomvi na marehemu rafiki yake brother akakamatwa na rafiki yake wa karibu ni brother kwa hyo brother akaunganishwa

Huyo marehemu alikua ni jirani yake rafiki yake brother alipojenga lkn brother na huyu rafiki ake wanakutan kazini mambo ya maadui uko nyumbn kwa rafiki yake yeye hayajui ndo ikatokea huyo jamaa akauawa kwenye pombe polisi kufanya uchunguzi wakamkamata rafiki yake bro na brother nae akaunganishwa eti anajua kila kitu balaa

Tukaanza mapambano ya kumtoa jamaa kama inavojulikana kesi za mauaji hazina dhamana na mimi ndo nikawa nahodha wa jahazi kumtoa jamaa pambana kila kona hakuna kitu. Miezi sita ikaisha jamaa bado yupo magereza honga kila mtu lakini wapi. Moyo ulikua unaniuma saana siku mwamba akiletwa mahakamani na lile karandika la magereza nilikua najisikia uchungu saana damu nzito aisee nikawa najiona mbona bado cjapambana vya kutosha inakuaje jamaa anateseka hivi na mimi nipo. Kila weekend nikawa naenda gerezani kumuona wakati namkuta jamaa kakonda kawa mweusi tii. Nikajikuta nikitoka kumuoana gerezani au akiletwa mahakamani mwili wote unapoa hata kusex nikawa siwezi mkunyenge hausimami kabisaa

Biashara ikaanza kuyumba kwa kasi mahitaji yakaongezeka na uwezo wa biashara kujiendesha ukashuka na pia kipindi kile ndo serikali ya awamu ya 5 imeshika hatamu na vyuma kukaza mauzo yakawa yako chini sana ikabidi nianze kupunguza matumizi ili biashara isije ikafa na pesa nlizokua natoa hapa na pale ndo ikawa balaa

Ilivofika miezi kama nane au tisa ivi hakuna kinachoeleweka nikaitwa kijijini kwetu nikawakuta ndugu upande wa baba na mama kwa maana wajomba zangu na baba zangu wakubwa na mashangazi nikawekwa kiti moto kwann nimeshindwa kumtoa jamaa na hajaua nikajaribu kuwaelezea hali halisi ndo hawaelewi utafikiri Mimi ndo nlimuweka ndani.

Nikapewa wazo la kwenda kwa mganga na lazima nitii kwa vile jamaa alivyokua anateseka nikajisemea potelea mbali ntanyaje huu ndo uanaume. Nilikua tayari kwa lolote kusudi tu jamaa atoke, nikarudi mjini nikamshirikisha ahemeji angu mke wa jamaa akakataa kata kata yeye akasema haamini ivyo vitu yeye na maombi maombi na yeye

Kuna mganga nikaunganishwa nae yupo mtwara huyu mganga niliunganishwa nae na jamaa yangu aliekua anaona ninavohangaika sharti nikatakiwa niende na viatu vya jamaa nikaona hyo rahisi nikaenda nyumbn kwa jamaa nikamkuta shem kalala kuna masandals ya jamaa nikaiba bila hata shem kujua

Asubuhi na mapema nikapanda gari za mtwara nikafika mtwara mjini nikapanda hiace za kwenda kijijini nikafika kijijini saa mbili usiku nikafika kwa mganga nilitak anifanyie dawa zake usiku ule ule kesho yake niondoke akakataa akasema ametoka kuzika waganga wakishika maiti kwa siku hyo harusiwi kutibia mtu kwa hyo mpaka kesho yake usiku

Inaendelea...

Asubuhi kulivokucha siku ya kupewa tiba nikaamka na homa kali kutapika kuharisha kwnye mji wa watu nikajiona nafia mtwara kwa mganga, yule mganga akanipa dawa ninywe kufika jion nikawa nimepata nafuu kiasi lkn kwa sababu ya kutapika mchana mzima mwili uliishiwa nguvu na usiku huo ndo nlitakiwa nikafanyiwe dawa na zile sandals za brother nlizobeba

Ikafka saa mbili usiku akaja jamaa msaidizi wa mganga safari ya kwenda kilingeni ikaanza tulipanda baiskel moja wote watatu Mimi mganga na msaidizi wake. Safari ilikua ya masaa mawili na baiskel tulipofik mwisho tukaegesha baiskel sehemu tukaanza kupita chochoro mpk eneo la tukio. Niliyoyaona huko siwezi sema umu ila hii dunia ina mengi nilianza kuogopa nikatak kugairi mganga akaanza kunitisha juu ya madhara ntakayopat ikiwa sitafuatish anachosema. Nilichojifunza kila mti ni dawa kuna mambo ni mengi watu hatujui tu. Baada ya mganga kumaliza mambo yake kurudi kijijini

Tulifika alfajiri Kijiji nikaanza kujiandaa kurudi mjini kwa jinsi nilivochoka nikala usingiz kidgo nlivoamka nikaagana na mwenyej wangu kurudi mjini kufika mtwara gari zote za kuja dar zimeishaondoka nikaunga unga na gari za mizigo mpaka nikatoboa

Mganga alinipa masharti kwanza siku ya jamaa kuletwa nihakikishe Mimi ndo mtu wa kwanza kushkana mikono na hakimu wa kesi yake na pili kuna dawa nimpe jamaa aweke mfukoni na zile sandals nikaziweke kwenye kona ya nyumba kijijin kwetu nikafanikiwa kufanya yote baada ya miezi miwili jamhuri wakasema hawana nia ya kuendlea na shauri jamaa akaw huru

Baada ya kutoka vitu ving vikawa vimeyumba nikampa taarifa zoote za kila kitu na jinsi nilivopambn na vingine nlimficha akiwa gerezan nisije nikampa msongo zaidi akashukuru saana tukatiana moyo na tukapnga mikakati mipya ya kumove on.

Baada km wiki mbili ivi sijui mkewe kamwambia nini akaanza kubadilika tofaut na ninavomjua akaanza kunifokea bila sababu jamaa akawa mkali hafai nikimpigia simu hapokei na hanitaft kitu ambacho hajawahi kufanya ivo

Pale ofisini ninaposimamia akamleta shemeji ake mdogo wa mke wake akaanza kuniendesha yaani alimtuma kwa dhumuni la kunitoa pale kazini. Nikaona isiwe tabu nikamfata jamaa nikamuuliza ndugu yangu shida akasema hakuna. Nikaona dharau pale ofisini kwa shemej ake zimezidi nikaanza kujiandaa kuondok kwenye ofisi ile nikapambane kivyangu

Nilishaanza kusikia maneno kutoka kwa rafiki zake kua mimi nmemfilisi wakati yupo gerezani na hataki kufanya kazi na Mimi tena ila Mimi na yeye tukikutan hanionesh chochote.siku moja nikamtuka huyo shemeji ake makusudi maneno aliyonipa nikapata picha halisi alaf jamaa nae ananipigia kuonesha kukasirika sana akanitemea maneno mbovu saaana ndo nikapata uhakika wa yale maneno ya rafiki zake waliyokua wakinambia

Nikakaa pale pale ofisini nikiwa sina kazi ya kufanya majukumu yote akawa anafanya shemeji ake. Nikampigia ndugu yangu kua nataka kutoka pale nikahangaike mbele kwa mbele japo nlikua nishatolewa kwa akili pale ofisini bro akanambia powa

Nikaanzisha biashara yngu inayofanan na ile ya kwake wateja wengi waliokua wananifahm wakaanza kuja kwangu. Hapo ndo nlikua nimetangaza vita maneno yakaanza eti wakati jamaa yupo gerezani mimi nilitaka apotelee uko ili nichukue mali zake na ile safari ya mtwara nilienda kumpoteza kabisa.

Na kwa vile kijijini jamaa ndo anajulikana ana pesa watu wengi wakaamini yale maneno nikawa nanyooshewa vidole Mimi mpk wale wajomba zangu walionishauri niende kwa mganga wakanigeuka. Mama nae akatuita tuzungumze yaishe bi mkubwa akaonesha km yupo kwa mwanae na mama ndo ilikua karata yangu ya mwisho lkn nilishangaa mama angu mzazi kuonesha km haniamini na inawezek yale yanayozungumzwa kuna ka ukwel flan

Kijijini kote ikawa habari ni sisi na jamaa kubwa ni Mimi.

Nikarudi mtwara kwa mganga nikamwambia kila kitu akasikitika saana akaniuliza unataka nini nikamwambia nataka kumuua jamaa ili yatimie mganga akaniuliza unatak kumuua ndugu yako nikamjibu ndio. Mganga akanambia nikimuua ndugu yangu na aman sitapata maisha yangu yoote akanishauri ni kunipa maneno mazito roho ya kuua ikanitoka.
 
Usingepokea ushaur wang saiv usingekuw hapa
 
Back
Top Bottom