Nimsaidieje huyu binti?

Nimsaidieje huyu binti?

Habari wakuu,

Nimekuwa na binti katika mahusiano kwa kipindi kirefu sana (tangu akiwa form 2 mpaka sasa yupo mwaka wa 3 chuo kikuu).Aliamini mimi ndiye mume wake japo mimi sikuwahi kuamini kama yeye ni mke wangu kwa sababu sinaga utaratibu wa kuwaamini wanawake hivyo nikawa nasubiri muda uongee kama itakuwa basi nitamshukuru MUNGU.

Alivyofika kidato cha tano aliamua kwa mapenzi yake kunitunuku bikra yake( sikuwahi kumlazimisha kufanya hivyo) kutokana na imani yangu kwake nilijua naweza kumtoa hiyo bikra yake ikaja kuwa fimbo mwisho wa siku na kuanza lawama zisizo na msingi.

Mwaka 2016 niliagana nae naenda kimasomo somewhere(akiwa form five hiyohiyo) akaahidi kunisubiri kwa gharama yoyote nikasema poa MUNGU atajalia nitarudi na mapenzi yataendelea. Nimekaa kusikojulikana mpaka mwaka jana(2019). Kwa kipindi chote hicho tulikuwa tunawasiliana japo sio sana ila mimi ndio sikutaka mawasiliano ya mara kwa mara kwa kuogopa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa (kiukweli sikuwahi kuwaamini wanawake) hivyo nilijua atakuwa akijifanya kuwasiliana na mimi muda mwingi ila wahuni wanaendelea kuishi kama kawa.

Sikutaka hilo litokee nikapunguza mawasiliano ikafika kipindi mpaka ukawa unapita mwaka bila simu yoyote ila kwa kipindi chote hiki sikuwahi kuwa na mahusiano na mtu mwingine sababu sipo interested sana na wanawake kiukweli. Nilivyorudi nilimtafuta kwa simu na kumuomba nikutane nae hotelini tujadili mawili-matatu.

Alivyokuja swali la kwanza nilimuuliza kama bado ananipenda akajibu ndio tena sana ila kuna mtu kamtolea mahari anataka amuoe kwani kamsaidia mambo mengi kipindi mimi sipo na mama yake ndiye aliyemlazimisha akubali akijua mimi nshaachana nae. Mimi nilinjibu hilo kwangu sio tatizo kama umepata mtu wa kukuoa mshukuru MUNGU huenda haikupangwa sisi kuoana hapo ndipo kilipoanzia kimbembe anadai ananipenda mimi na yupo tayari kumkataa huyo jamaa aliyetoa mahari.

Kwa upande wangu sipo tayari kuona mwanaume mwenzangu anaumia kwa sababu ya mwanamke, kwangu haina tatizo kwani haya niliyategemea tangu siku ya kwanza.

Naombeni mnishauri wakuu njia sahihi ya kumuelewesha huyu mdada aachane na mimi na akaolewe na huyu jamaa yake.

Ahsante

Nachoona hapa ni kwamba unampenda sana huyo dem, lakini ww ni ile aina ya wanaume ambao mnaamin kuonesha hisia kwa mwanamke ni udhaifu, yaaan unajifanya dont care ilihali u care a damn lot yaan, afu una arrogance fulani hivi ambayo ndo imekupelekea kumkosa huyo dada, it might be true huyo dada anakuelewa vibaya sana, ila you are not good for her! Mwanamke anahitaj kuwa taken care emotionally naww hilo umefail! Hakuna namna sahihi zaid ya namna uliyoitumia kumpotezea kipindi uko hukooo unapodai masomoni!

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nilimuita kujua msimamo wake kwa sasa kama bado ananipenda au la, kwa sababu huwa sina utaratibu wa kupeleka wanawake kwangu mpaka nitakaekuja kuoa.
Jiamini bro, Afu huyo mwanamke achana naye coz unaogopa kuchapiwa na kama umesoma vyuo vya Bongo utaelewa nasema nini,haya mambo yanahitaji mtu uwe mjanja sio kutanguliza hisia utaumia.
 
Habari wakuu,

Nimekuwa na binti katika mahusiano kwa kipindi kirefu sana (tangu akiwa form 2 mpaka sasa yupo mwaka wa 3 chuo kikuu).Aliamini mimi ndiye mume wake japo mimi sikuwahi kuamini kama yeye ni mke wangu kwa sababu sinaga utaratibu wa kuwaamini wanawake hivyo nikawa nasubiri muda uongee kama itakuwa basi nitamshukuru MUNGU.

Alivyofika kidato cha tano aliamua kwa mapenzi yake kunitunuku bikra yake( sikuwahi kumlazimisha kufanya hivyo) kutokana na imani yangu kwake nilijua naweza kumtoa hiyo bikra yake ikaja kuwa fimbo mwisho wa siku na kuanza lawama zisizo na msingi.

Mwaka 2016 niliagana nae naenda kimasomo somewhere(akiwa form five hiyohiyo) akaahidi kunisubiri kwa gharama yoyote nikasema poa MUNGU atajalia nitarudi na mapenzi yataendelea. Nimekaa kusikojulikana mpaka mwaka jana(2019). Kwa kipindi chote hicho tulikuwa tunawasiliana japo sio sana ila mimi ndio sikutaka mawasiliano ya mara kwa mara kwa kuogopa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa (kiukweli sikuwahi kuwaamini wanawake) hivyo nilijua atakuwa akijifanya kuwasiliana na mimi muda mwingi ila wahuni wanaendelea kuishi kama kawa.

Sikutaka hilo litokee nikapunguza mawasiliano ikafika kipindi mpaka ukawa unapita mwaka bila simu yoyote ila kwa kipindi chote hiki sikuwahi kuwa na mahusiano na mtu mwingine sababu sipo interested sana na wanawake kiukweli. Nilivyorudi nilimtafuta kwa simu na kumuomba nikutane nae hotelini tujadili mawili-matatu.

Alivyokuja swali la kwanza nilimuuliza kama bado ananipenda akajibu ndio tena sana ila kuna mtu kamtolea mahari anataka amuoe kwani kamsaidia mambo mengi kipindi mimi sipo na mama yake ndiye aliyemlazimisha akubali akijua mimi nshaachana nae. Mimi nilinjibu hilo kwangu sio tatizo kama umepata mtu wa kukuoa mshukuru MUNGU huenda haikupangwa sisi kuoana hapo ndipo kilipoanzia kimbembe anadai ananipenda mimi na yupo tayari kumkataa huyo jamaa aliyetoa mahari.

Kwa upande wangu sipo tayari kuona mwanaume mwenzangu anaumia kwa sababu ya mwanamke, kwangu haina tatizo kwani haya niliyategemea tangu siku ya kwanza.

Naombeni mnishauri wakuu njia sahihi ya kumuelewesha huyu mdada aachane na mimi na akaolewe na huyu jamaa yake.

Ahsante

Wee jamaa nilikukuona bonge la mwanaume uliposema kuwa sijawahi kuwaamini wanawake... Mwisho ukaja kuonyesha uboya wako tena... Sasa kama ulikuwa huna shida nae ulimtafuta wa nini?
Kama kumgegeda ulishamgegeda hana jipya huyo wee kausha kimya wala huna sababu ya kumtafuta.
Mwanamke ukishamgegeda yeye ndio akutafute sio wewe kidume bwana.
 
N
Jiamini bro, Afu huyo mwanamke achana naye coz unaogopa kuchapiwa na kama umesoma vyuo vya Bongo utaelewa nasema nini,haya mambo yanahitaji mtu uwe mjanja sio kutanguliza hisia utaumia.
Nashukuru mkuu.
 
Wee jamaa nilikukuona bonge la mwanaume uliposema kuwa sijawahi kuwaamini wanawake... Mwisho ukaja kuonyesha uboya wako tena... Sasa kama ulikuwa huna shida nae ulimtafuta wa nini?
Kama kumgegeda ulishamgegeda hana jipya huyo wee kausha kimya wala huna sababu ya kumtafuta.
Mwanamke ukishamgegeda yeye ndio akutafute sio wewe kidume bwana.
Ndugu yangu nadhani hukunielewa vizuri, nilimtafuta nilivorudi kujua yupo upande gani kwa sasa kwa sababu kipindi chote hicho hatukuwahi kugombana kwahiyo isingekuwa vyema kumpotezea kimya.
 
Hebu subiri kwanza, vipi kuhusu wanaume wenzio uko interested nao?
 
Kuna vitu navipa kipaumbele zaidi ya mahusiano ya kimapenzi mkuu. Ndicho nilichomaanisha
 
Back
Top Bottom