Nimsaidieje huyu binti?

Nimsaidieje huyu binti?

ydon

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2014
Posts
253
Reaction score
197
Habari wakuu,

Nimekuwa na binti katika mahusiano kwa kipindi kirefu sana (tangu akiwa form 2 mpaka sasa yupo mwaka wa 3 chuo kikuu).Aliamini mimi ndiye mume wake japo mimi sikuwahi kuamini kama yeye ni mke wangu kwa sababu sinaga utaratibu wa kuwaamini wanawake hivyo nikawa nasubiri muda uongee kama itakuwa basi nitamshukuru MUNGU.

Alivyofika kidato cha tano aliamua kwa mapenzi yake kunitunuku bikra yake( sikuwahi kumlazimisha kufanya hivyo) kutokana na imani yangu kwake nilijua naweza kumtoa hiyo bikra yake ikaja kuwa fimbo mwisho wa siku na kuanza lawama zisizo na msingi.

Mwaka 2016 niliagana nae naenda kimasomo somewhere(akiwa form five hiyohiyo) akaahidi kunisubiri kwa gharama yoyote nikasema poa MUNGU atajalia nitarudi na mapenzi yataendelea. Nimekaa kusikojulikana mpaka mwaka jana(2019). Kwa kipindi chote hicho tulikuwa tunawasiliana japo sio sana ila mimi ndio sikutaka mawasiliano ya mara kwa mara kwa kuogopa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa (kiukweli sikuwahi kuwaamini wanawake) hivyo nilijua atakuwa akijifanya kuwasiliana na mimi muda mwingi ila wahuni wanaendelea kuishi kama kawa.

Sikutaka hilo litokee nikapunguza mawasiliano ikafika kipindi mpaka ukawa unapita mwaka bila simu yoyote ila kwa kipindi chote hiki sikuwahi kuwa na mahusiano na mtu mwingine sababu sipo interested sana na wanawake kiukweli. Nilivyorudi nilimtafuta kwa simu na kumuomba nikutane nae hotelini tujadili mawili-matatu.

Alivyokuja swali la kwanza nilimuuliza kama bado ananipenda akajibu ndio tena sana ila kuna mtu kamtolea mahari anataka amuoe kwani kamsaidia mambo mengi kipindi mimi sipo na mama yake ndiye aliyemlazimisha akubali akijua mimi nshaachana nae. Mimi nilinjibu hilo kwangu sio tatizo kama umepata mtu wa kukuoa mshukuru MUNGU huenda haikupangwa sisi kuoana hapo ndipo kilipoanzia kimbembe anadai ananipenda mimi na yupo tayari kumkataa huyo jamaa aliyetoa mahari.

Kwa upande wangu sipo tayari kuona mwanaume mwenzangu anaumia kwa sababu ya mwanamke, kwangu haina tatizo kwani haya niliyategemea tangu siku ya kwanza.

Naombeni mnishauri wakuu njia sahihi ya kumuelewesha huyu mdada aachane na mimi na akaolewe na huyu jamaa yake.

Ahsante
 
A
Uandishi wa story yako Tangia mwanzo unaonyesha unayo Stamala Wajada, Endelea nayo Stamala wajada

Yaani kaza mpaka mwisho kama ulivyoweza kukaza kuanzia mwanzo
Ahsante mkuu
 
  • Wewe una kiburi,majivuno na kujiona. Ndio maana kakucheat maana unaonekana hukumuweka karibu nawe kiss kujiona (You don't give a damn). Badirika, uhusiano ni mawasiliano na Women wanapenda kuwekwa karibu! Kuona hisia za mtu kweli! Kwa silka yako hiyo baadae utakua moja ya wale wazee tunawaita Dingi Mkuda
  • Huyo gal nae kitendo cha kutaka kumkataa aliyemtolea mahali kisa wewe kimemshusha credibility! Inaonyesha si mwaminifu..Japo kua itawezekana ana hisia za kweli nawe..
In short nyote ni chupa na mfuniko..
I'm sorry kwa kutumia maneno makal
 
nimekuelewa mkuu
 
Hapo chagua moja kwenye mawili
1. Nenda kwa mama yake kimya kimya bila ya yeye kujua, mueleze kila kitu na utoe Baraka zote harusi ifanyike Kama kawaida, kisha binti aitwe mbele yako na myamalize.
2. Kimbia mbali sana, badili namba na kata mawasiliano Kama ulivyofanya ukiwa masomoni walau mpaka harusi iishe, na uweke nia Kama mwanaume kuwa hutoingilia mahusiano Yao tena. Kuwa jasiri
 
sasa kama hauko interested na wanawake,ulimuita hotelin ili umfanyaje?
Nilimuita kujua msimamo wake kwa sasa kama bado ananipenda au la, kwa sababu huwa sina utaratibu wa kupeleka wanawake kwangu mpaka nitakaekuja kuoa.
 
Hapo chagua moja kwenye mawili
1. Nenda kwa mama yake kimya kimya bila ya yeye kujua, mueleze kila kitu na utoe Baraka zote harusi ifanyike Kama kawaida, kisha binti aitwe mbele yako na myamalize.
2. Kimbia mbali sana, badili namba na kata mawasiliano Kama ulivyofanya ukiwa masomoni walau mpaka harusi iishe, na uweke nia Kama mwanaume kuwa hutoingilia mahusiano Yao tena. Kuwa jasiri
Nashukuru sana mkuu, kiukweli siwezi kuingilia mahusiano yao hata kidogo.
 
Mhitimu wa chuo, mbona msala mdogo tu!

Mtu ameshatolewa hadi mahali! Wewe unataka uingilie nini tena wakati unasema hauko interested na hayo mambo?

Hiyo ya kutolewa mahali, tayari ni ticket ya kukuchomoa kwenye hayo mahusiano.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nimebariki ila namshangaa anataka akatishe ndoto za huyo mtoa mahali eti kisa nimerudi.
 
Kama
since form 2 mpaka chuo kikuu
afu unasema hukuwa na mpango wa kumuoa why ulimuweka by ur side sasa ??
sometimes wanaume tuwe hofu ya Mungu kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
kama umesoma vizuri nimesema nilikuwa tayari kumuoa ila sikuwahi kumuamini. Kwa hiyo kama ungefika muda wa kuoana bila tatizo lolote ningeoa tu mkuu na ndio maana sikuwahi kuwa na mahusiano mengine tofauti na yeye.
 
Back
Top Bottom