Nimrudie au nifanye nini?

Bk boy

Member
Joined
Nov 18, 2022
Posts
19
Reaction score
17
Hello wana JF, twende kwenyee mada husika.

Naitwa Bk, nilikuwa kwenye mahusiano na mwanachuo wa chuo fulan, tulianza mahusiano toka mwezi wa 4, tulidumu kama miezi miwil halafu akaenda field tukatengana kwa muda, mimi nikiwa Moshi yeye yupo Arusha.

Baad ya miezi miwili akawa haeleweki, yaani hajibu kwa wakati, mara asipokee simu. Basi nikaamua kuachana naye kwa amani. Baad ya miezi kadhaa mbele anakuja leo hii ghafla anataka turudiane.

Je, nifanyaje na nina mpenzi mwingine?

Ushauri wenu kwangu.
 
Kijana wa chuo, unaandika hovyo kuliko mimi wa darasa la 7C.
Ajabu kabisa. Hawa ndio wanakwenda School of Law, 90% wanafeli, halafu wanasingizia wakufunzi kuwafelisha, kumbe uwezo wao ndio mdogo. Elimu ya Tanzania kwa sasa imekuwa majanga. Unakutana na mhitimu wa Chuo Kikuu lakini uwezo wake wa kiakili hauna tofauti na aliyeamaliza Kidato cha Nne aliefeli.
 
Usiangalie nyuma, wapenzi kama hawo wanarudishaga maendeleo nyuma, wanakuziba kukutana na mpenzi Mpya kwa sababu ya kurudia rudia ulikotoka.
 
Hakuna kulamba matapishi mkuu chapa ilale😅
 
Nliwahi kusema law school ni div 3 waliofeli ,Raia wakabisha kinoma😅😅😅
 
Sasa unauliza nini dogo, mtu ana kukaushia wewe unataka jibu gani tena zaidi ya kuelewa kuwa umepigwa kibuti? Halafu unayo pic nyingine bado unalialia wewe vipi?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…